Maisha plus! On tbc1

Wi-Fi

JF-Expert Member
Aug 30, 2011
2,091
1,378
Habari wana JF,

Binafsi kabisa napenda sana ichi kipindi cha Maisha plus (Masoud Kipanya) akiwa kama founder wa kipindi hichi.
Napenda sana hatua hii ya usahili (interview) kwa kweli najifunza kwamba watanzania wengi tunakosa maarifa ya vitu vidogovidogo na pia hatuna ujasiri kabisa wa kujieleza kwa kifupi upeo wetu wakufikiri na kupambanua mambo(IQ) ni mdogo sana, yani ukiwa unaangalia kipindi hichi unabakia ukicheka tu..

My take:
Nafikiri itakuwa vyema kutumia muda wetu kukuza uwezo wetu wakufikiri na kujua mambo mbalimabli ya kiuchumi, kijamii na hata kisiasa ikiwa ni kwa kusoma na kujifunza kupitia nyenzo (materials) mbalimbali kama magazeti, vitabu na majarida mengineyo na pia kwa kutumia internet (google) vizuri hii itaweza kutanua elimu yetu na uelewa wa vitu mbalimbali.

Swali kwako:
Maisha plus kwenye hatua hii ya usahili(interview) inakufundisha nini juu ya watanzania walio wengi? na nini kifanyike kukuza IQ zetu?
 
Back
Top Bottom