Maisha magumu Tanzania chanzo chake nini?

Naytsory

JF-Expert Member
Nov 3, 2011
2,192
791
wanajamvi nisaidieni, je ni kupuuzwa kwa mawazo ya wataalam?, Kutothaminiwa kwa wataalam? Nchi kuongozwa na wanasiasa ambao ambao hawathamini taaluma? Tanzania tunatumia fedha nyingi kusomesha wataalamu wengi ndani na nje ya nchi lakini matunda hayaonekani kwenye nyanja za kiuchumi, kisiasa na kijamii. Tunachoshuhudia ni ufisadi na uwizi wa rasilimali zetu unaofanywa na hao tuliowasomesha kwa kodi zetu. Watanzania wangapi walisomea uhandisi na wengine uchumi lakini matunda yao yako wapi? Na kama hawana faida au hawathaminiwi kwani kuharibu fedha zetu? Nafuu waalimu na madaktari ambao kazi za zinaonekana. Kwanini kadri wanavyokuwa wengi hali inakuwa mbaya kuliko jana na juzi?
 
chanzo cha maisha ya watanzania kuwa magumu ni watanzania wenyewe kwa kutegemea kuwa serikali ambayo iko kwa ajili ya kuwaibia kuwa kuna siku itabadilika na kuwaletea maendeleo. mtanzania popote pale ulipo maisha yako na familia yako yanakutegemea wewe na si mwingine akija mtu kutoka serikalini anataka kukusaidia mwambie akawasaidie wengine maana anatka kukuibia.
 
Lakini inaonekana hawa wataalam wana mgomo baridi kwani hata kazi za kitaalam wanasiasa ndiyo wanaofanya maamuzi na watu hao siyo wataalam wa fani hiyo. Hapo unategemea nini? Kwa upande wa watanzania wengi kutambua si rahisi.
 
soma post yangu nani anamiliki uchumi wa tz na nini ni athari zake...iko hapa jf upata jibu katika taswira nyingine kabisa inayohusu uchumi na uongozi
 
ni vijana wa taifa letu kujifanya wajuaji sana muda wote kuhangaika na mitandao ya siasa badala ya kuhangaka na mitandao ya KIJASIRIAMALI, MNAJIFANYA MNAJUA SANA MAMBO YA SIASA ETI OH PINDA HAFAI, JK HANA LOLOTE JIULIZE WEWE KWENYE ACCOUNT YAKO UNAMILIKI NINI?
 
Back
Top Bottom