Maisha Club imeungua moto!!

Jamani mi nina mtazamo tofauti na wenzangu, naona kama vile matukio ya moto yanapangwa..... Mi sidhani kama kweli itilafu za umeme ndio chanzo cha matatizo hayo kusema kweli.

Naona wafanya biashara wamejanjaruka kiasi cha kwambawanataka kulipwa na bima wajenge kitu kikali zaidi kama yule jamaa wa Paradize Bagamoyo.

Napenda kumpa pole huyo mama mwenye ukumbi na hongera pia kwa kufanikisha dili yake.....................

watu hamkosi la kusema ;loh
 
Lakini pia kwa wenzetu wa clubs na mahoteli lazima wabadirike ktk ujenzi. Unakuta mtu kawekeza kwenye sakafu kuta na vifaa vingine lakini ukiangalia paa ni nyasi au makuti, je, kweli ikitokea ajali ya moto nani alaumiwe? kwa nini vigae visitumike?
 
Mimi niliwah kuandika humu JF na narudia tena japo binafsi sina nyumba yangu binafsi au ya biashara lakini nawauliza hata sisi wenyewe members hapa JF, ni nani ana fire extinguisher hata moja nyumbani kwake na familia wanajua kuitumia??

mie binafsi sina hiyo FE kuitumia najua
 
okay!kumbe....?!
unadhani vingesaidia kuzima moto kama huu?au wa paradaiz rizoot?

zipo fire extinguishing systems kubwa kulingana na facility lakini pia kama mtu una mradi mkubwa ni lazima uwe na high pressure water pipes nearby ili kukabiliana na majanga ya moto. Lakini hili kwa TZ ni kama halina umuhimu ila pale yanapotokea ndo utasikia kelele zinaanza.
 
hapa bila shaka unaizungumzia HORSE-REEL,am i right?
 
mie binafsi sina hiyo FE kuitumia najua

Nashauri basi watanzania tujifunze tununue hivi vifaa huwa vinasaidia hasa pale moto unapoanza watu wakiwepo. Na ni vizuri kama mtu una watoto au mtumishi wa ndani ukawafundisha jinsi ya kuitumia.
 
Nashauri basi watanzania tujifunze tununue hivi vifaa huwa vinasaidia hasa pale moto unapoanza watu wakiwepo. Na ni vizuri kama mtu una watoto au mtumishi wa ndani ukawafundisha jinsi ya kuitumia.
hivi wewe unadhani faya eksitinguisha haikuwepo maisha?
 
mimi nasikitika sana kwasababu wakati niko chuo ndo kilikuwa kiwanja changu!:D

Pole sana mpwa. Nakukatibisha katika Nyumba Za Bwana tumwimbie na kumsifu Mungu kwa nyimbo na mapambio.
 
Ndiyo mkuu

sasa mkuu,
tatizo letu wabongo ni kwamba ni watu wa kufuata sheria.

KWA MFANO:watu wanaodraivu magari.unakuta kwenye gari kubwa,mathalani pulling,au semi.dereva anatembea na kafaya eksitinguisha kana gesi ujazo wa ml 500.na trafiki akimwambia onyesha faya-eksitinguisha anaonyesha na anakubaliwa
 
Ajali kama hii ikitokea,watu wote wanasikitika. Lakini swali moja hapa la kuuliza,ni kwamba, kuhusu hizi ajali za moto,how do we compare,for example ,wtih Kenya? Ajali za moto hapa zinatokea vipi ukilinganisha na Kenya au na nchi zingine?
QUOTE]

My friend dont even go there.... juzi supermarket ya nakumatt iliteketea mpaka majivu and its less than 100 m from the fire station. haya wiki iliyopita moto umetokea two different areas.... ndipo tukajua kuwa all the fire engines are grounded. everyone for themselves and God for us all.

we are very ill prepared for any form of disaster..uombe mungu tu yasikufike!
 
hivi wewe unadhani faya eksitinguisha haikuwepo maisha?

Tatizo la watanzanaia ndo hili....we should take what has happened at Maisha club as a lesson and try to prepare for future fire disasters!!! Mkuu mimi siongelei sana Maisha club ila naongea in general terms kwamba tujaribu kujiandaa na majanga ya moto at family level.

Nasema hili kwa sababu tunadhani kila ajali ya moto ni lazima ni moto mkubwa....lakini kuna jamaa yangu mmoja nyuma iliungua lakini moto ulianza kwenye switch socket, ukaunguza kapeti, sofa na baadaye ukafikia ceilling na wakati huo watoto walikuwa wanalia lia tu, huyu angekuwa na FE na watoto wanajua kutumia wangezima ule moto.
 
Mi sisikitiki sana kwa kuwa kilichoungua Siyo Nyumba Ya Kumtukuza Mungu.

Chrispin mbona una mtizamo finyu sana??? Vipi kuhusu
1. Watu waopotoze ajira zao (au kwa vile dada yako afanyi kazi hapo?)
2. Vipato vya madereva tax na vibajaji
3. lost government revenues in terms of tax
4. wategemezi wa dada yetu Hellen
5. Kamtaji ka dada yetu (assuming MC was not insured)
6. Uchafuzi wa mazingira
7. Sadaka walizokuwa wanatoa wafanyakazi wa MC kila waendapo makanisani na misikitini
8. Ajira ya maDj na wanamuziki waliokuwa wanatumbuiza hapo
8. Burudani waliyokuwa wanapata watu mbalimbali, ambayo pengine ilikuwa inawafanya wapumzishe akili na miili yao na hivyo kuongeza tija mahala pao pa kazi
9. n.k. n.k.
 
Jamani poleni wahanga maana walioathiriwa na janga hili ni wengi! Lakini mbona mioto imezidi sehemu za biashara siku hizi? Tulisikia ya Sea Cliff, tukasikia ya Paradise, tunasikia ya Maisha .... yaani ni kama yale ya shule za sekondari ambazo zilikuwa zinahujumiwa sasa na hapa tuseme kuna wanaowahujumu hawa wajasiria mali?
 
Chrispin mbona una mtizamo finyu sana??? Vipi kuhusu
1. Watu waopotoze ajira zao (au kwa vile dada yako afanyi kazi hapo?)
2. Vipato vya madereva tax na vibajaji
3. lost government revenues in terms of tax
4. wategemezi wa dada yetu Hellen
5. Kamtaji ka dada yetu (assuming MC was not insured)
6. Uchafuzi wa mazingira
7. Sadaka walizokuwa wanatoa wafanyakazi wa MC kila waendapo makanisani na misikitini
8. Ajira ya maDj na wanamuziki waliokuwa wanatumbuiza hapo
8. Burudani waliyokuwa wanapata watu mbalimbali, ambayo pengine ilikuwa inawafanya wapumzishe akili na miili yao na hivyo kuongeza tija mahala pao pa kazi
9. n.k. n.k.

10. mbona umesahau ni mahala pa kujipatia viserengeti boys and dada wa kitanga !!!!!ala?
 
Back
Top Bottom