Maisha bora kwa kila mtanzania inawezekana

rr3

JF-Expert Member
Mar 19, 2015
3,035
3,724
Wakuu

Hii kauli ilikuwa mojawapo ya kauli mbiu za Mh. Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Raia kwa ujumla wake waliposikia hii kauli walifurahia sana na wakajua sasa mambo murua na Rais ndio huyu. Na kiukweli ni kauli mbiu nzuri na yenye uwezo wa kuleta makubwa kama ingepewa uzito unaostahili.

Hii kauli kiukweli wananchi tuliichukulia kama kauli ya matumaini wandugu. Na nieleweke kuwa huwa sifungamani na chama chochote cha siasa bali mtu binafsi mwenye nia na njozi ya kubadilisha mwelekeo wa hili jahazi na haijalishi anatoka chama gani.

Kauli hii wote, wananchi na viongozi tuliitafsiri vibaya na wote kuna sehemu tulitakiwa tutoe mchango wetu lakini haikuwa ivyo.

Nitaanza na mapungufu ya sisi wananchi ( Nitajazia mapungufu ya Serikali na viongozi baadae )

1. Uvivu uliopitiliza. Sisi Watanzania ni wavivu kupita kiasi, kuna asilimia ndogo sana ya wanaojituma lakini kwa ujumla wake, tumebweteka. Kuna watu kazi yao ni kukaa vijiweni, kushinda majumbani na kwenye vikao vya kipuuzi bila kufanya lolote toka asubuhi hadi jioni. Kazi ni stori za mpira, majungu, umbea na kuota maisha.

Watu ni wavivu hadi wa kufikiri. Mtu anakaa siku nzima, mwezi na mwaka na bado hapati wazo la kufanya chochote na bado mtu huyo anakwambia anakunywa pombe aondoe mawazo. Yapi sasa? Matajiri wakubwa wote kuanzia na wa hapa Tanzania watakuambia " MTAJI MKUBWA KULIKO WOTE NI MTAJI MAWAZO " Ukishakuwa na mawazo mtaji pesa utakuja wenyewe.

2. Ulevi uliokithiri. Watu wanakunywa pombe sana sasa hivi, zinauzwa kwa wingi kila mahali na kuna wilaya mkoani kilimanjaro wameshalalamika kuwa wanaume wameshindwa unyumba na kazi hawafanyi. Kila kona ni pombe na nyingine wanatengeneza wenyewe.... namaanisha wanaiga za viwandani na kuweka kwenye chupa kabisa, vijana wamefanana na wazee.

Pombe sio mbaya, lakini kama pombe itakufanya ushindwe kwenda shambani, ushindwe kulea familia, ukiuza ndizi au kahawa wewe ni kwenye pombe, basi hayo maisha bora utayasikia tu.

Vijana siku hizi wanakunywa pombe toka saa kumi na mbili asubuhi tena bila kula. Watu hawa hawa ni wa kwanza kulalamikia maisha kuwa ni magumu.

3. Wahitimu wa vyuo kukosa mawazo. Mambo ya ajabu sana yanatokea siku hizi. Ni kweli kuwa elimu yetu sio, ila sasa imekuwa too much. Mtu kweli anamaliza chuo na anahangaika miaka mitano anatafuta kazi, kila anapoenda anakosa na bado anashindwa kubuni kimradi kidogo tu kama kwa mfano kufuga kuku?????????? Kuna wamama tu na baadhi ya wababa wapo mtaani hawajaenda sana skuli lakini wana miradi midogomidogo stable.

Hii inasababishwa na ulimbukeni na ujinga kwa kudhani kwasababu umeshika kalamu kwa miaka 16 au 17 basi wewe hustahili kufagia banda la kuku. sikiza nikwambie, kuku tu hawa wa kienyeji ambao hawahitaji chakula cha gharama na uangalizi mkubwa, ukiweza kuwa na kuku mia tano tu, hesabu kupata mayai 300 kwa siku, yai uza 250Tsh... 300*250= 75,000/= na soko la mayai ya kienyeji liko wazi na kuku mia tano wanaishi kwenye eneo dogo sana lililojengwa kwa mabati na nyavu tu. Kwenye 75,000/= toa 45,000/= ya chakula cha kuku na gharama nyingine zote then baki na 30,000/= * 30 = 900,000/=

Hayo hapo juu ni mahesabu madogo mno, ukiwa uko siriaz unaweza ajiri hadi graduate wenzako kwa ku-triple hayo mahesabu.

Kiukweli soko la ajira halitakaa lichukue wahitimu wote na ujue kuwa kuajiriwa ni utumwa mkubwa sana. Kama wewe ni mhitimu basi saidia nchi yako kwa kuwaza mradi unaoweza kufanya kuokana na mazingira yako, elimu ni mwanga tu, ukisoma unaelimika na kuona mambo kwa upeo mkubwa zaidi na hapo ndipo unapoweza kurudi kwenu na kufanya kitu flani, labda ukaajiri watu kumi kutoka maeneo ya kwenu na watu wakasema flani kweli ana shahada au stashahada.

4. Vijana kushindwa kudumu kwenye ndoa au kumzalisha mwanamke na kumtelekeza. Hii ilikuwepo toka enzi na enzi lakini sasa imezidi. Watu wanakutana chuo, njiani, disco, kwenye mduara, kigodoro au ngomani wanachukuana... mara mtoto.... kidogo tena mtoto. Siku mbili tatu wameachana, mama na watoto anarudi kwao kwa wazazi au nduguze na bwana anaelekea anakokujua.

Najua utajiuliza.. huyu vipi? hii ina mchango gani? au lengo hasa ni nini la kusema hili?

Sikia, huyu binti na mtoto au watoto wake wanarudi kwa ndugu au wazazi na hapo ni kushinda kucha kutwa bila kuchangia chochote kwenye cash flow ya hiyo familia. Hii inamanisha umaskini unaongezeka kwakuwa familia hiyo haikupanga kuwa na mzigo wa ziada na inashindwa kuweka akiba na kufungua biashara au miradi ambapo wangeajiri mtu au watu na kusaidia kupunguza idadi ya watu ambao hawajajiriwa mtaani au kijijini.

5. Vijana kutaka ufahari na utajiri kwa haraka mfano kuimba muziki, kuigiza na kuuza unga. Hii nayo sasa imesababisha kauli mbiu ile isifikiwe na iwe ndoto. Vijana wana mawazo kuwa watatoka kimaisha siku wakitoka kimuziki au kwenye maigizo ya kibongo na kwenye kuuza unga. Mtu anakaa akisubiri hiyo siku, kama ni kuuza madawa, anasubiri siku akipakiwa mzigo mkubwa ambapo ataibuka na kitita cha hela na kutoka kimaisha.

Hii ina mchango kwasababu, hiyo ni kama mtu nayesubiria daladala katikati ya kalahari desert. Meanwhile anaendelea kutumia kitu ambacho hajazalisha na hiyo ina maana kuna mtu anamnyonya. Anakuwa kupe na mwisho wa siku asipofanikiwa kwenye hiyo ndoto yake, muda unakuwa umeenda na anakata tamaa ya maisha, anaanza kuvuta bangi na kubwia unga.

Tuwe wakweli, soko letu la starehe kwamfano, linaweza kuhimili msanii mmoja tu mkubwa na wengine wadogo kama kumi tu. Wengine wote ni wasindikizaji. Na kwasasa soko lenyewe lipo kwenye muziki wa kizazi kipya, kuna kipindi lilikuwa kwenye taarabu then bongo movie.

Kama unaona huna kipaji, usilazimishe. Bora mapema sana, uanze kijimradi chako, kidogo kidogo baada ya miaka mitano upo mbali na wewe unaajiri.

6. Kutekeleza kilimo. Acha kilimo cha mvua, kuna maeneo mengi sana Tanzania ambako kuna maji mengi na ardhi nzuri yenye rutuba lakini vijana wameikimbia, wapo mjini wengine ni wapiga debe na kujifanya mawakala wa magari au biashara za watu na wengine ni madali uchwara.

Kwenye haya maeneo, sio lazima ulime kilimo kikubwa. Unaanza tu mbogamboga na vitu vinavyohitajika kwenye mazingira unayoishi halafu kuanzia hapo unakua taratibu.

7. Kununua vitu vya nje kwenye ma-supermarket. Huku ni kukosa uzalendo kwa hali ya juu. Mtu anaacha kununua nyanya au vitunguu na nazi au matunda mtaani kwake anapouza MAMA JUMA, anaeda kununua kwenye Ma-supermarket.

Mtu atasema huko kuna quality, lakini kumbuka vitu hivyo vimetoka nje ya nchi na ukinunua husaidii kukuza masoko ya ndani na kumuinua mkulima wa hapa nyumbani. We umezaliwa uru au ushirombo au mheza au kratu, kweli wewe ni wa kushindwa kula nyanya toka Iringa au machungwa toka Tanga????????????????Huko ni kujidharau na kumshusha mkulima wetu.

Hii inaenda mpaka kwenye vinywaji na nguo na vitu vingine vyote vinavyopatikana Nchini. Usinunue kitu kama kitu hicho unaweza kukipata hapa chini.

Sasa hizi ni baadhi ya sababu rahisi kabisa kwanini sisi kama wananchi hatujaweza kuiishi kauli mbiu ya maisha bora kwa kila mtanzania inawezekana. Sababu hizi ni zile ambazo zinamgusa kila Mwananchi na kila mwananchi anazijua na anaweza kuziepuka.

Itaendelea..................................................................................................................................................................................................................................................................................................
 
Kikwete ameshaondoka. Inabidi iendelee under magufuli.
 
UMENENA VYEMA!!

Maisha bora kwa kila Mtanzania ilikua ni Kamari tu,Hawa wanasiasa wa Nchi hii wameshayafanya Mawazo yetu Madogo kuwa Ndiyo Mtaji wao.Maisha bora kwa kila Mtanzania isingefanikiwa kwa kuwa Tumekosa Viongozi wenye Utashi wa Jinsi ya kutatua Matatizo yanayotukabili Wananchi!!
Sera ya Maisha bora kwa kila Mtanzania isingefanikiwa kwa sababu zifuatazo;

1,Wakulima tunadanganywa na Sera dhaifu za Kilimo Kwanza, kilimo kiko kijijini pembejeo ziko Mijini/Dar es salaam zinafanya nini? Kulima tunalima, Masoko hakuna na wala hakuna anayejishughulisha na hilo,Unategemea Maisha bora kwa kila Mtanzania yangewezekana??

2,Vijana tunapelekwa VETA kusomea ufundi, Viwanda hakuna huo ufundi tunaupeleka wapi zaidi ya kuanzisha vijiwe vya kubeti huku tukiongelea siasa Masaa 24?? Unategemea Maisha bora kwa kila Mtanzania yangewezekana??

3,Vyuo tunasoma na Mikopo tunapata,Baada ya Kumaliza kusoma Unaambiwa anahitajika Mtu Mwenye Uzoefu wa Miaka Miatano! Unategemea kuwa Mimi Niliyemaliza chuo Nitaajiriwa?? Unategemea Maisha bora kwa kila Mtanzania yangewezekana??

4,Serikali haitengenezi Mazingira wezeshi kwa sisi vijana kujiajiri,Unategemea hao kuku Nitawafuga vipi?? Hivi unadhani ni kweli hatuna Mawazo ya kujikomboa kutoka hapa tulipo?? Kiongozi ni Waziri/Mbunge,Mama ni Naibu katibu Mkuu,Mtoto ni Mjumbe wa kamati kuu,Je unadhani ni lini wataliona suala hili kuwa ni sugu?? Unategemea Maisha bora kwa kila Mtanzania yangewezekana??

5,Hospitali hazina Dawa, tunaenda katika Hospitali ya Wilaya hadi Panadol eti unaelekezwa kanunue Duka la dawa,Hilo Duka la mtu binafsi lilipataje Dawa hospitali ikakosa? Unategemea Maisha bora kwa kila Mtanzania yangewezekana??

6,Wewe pamoja na Hawa viongozi wetu Kila siku mnapiga kelele eti vijana tujiajiri!!! Vijana tujiajiri!!! Familia zenu Baba, Mama, Mtoto wote Ni wakurugenzi kwenye taasisi za Umma. Mnaishi Tanzania kiakili lakini kimwili Mpo Nchi za Nje,Je ni lini mtajua kama Mtaji ni tatizo? Hivi unawezaje kujiajiri bila mazingira wezeshi pamoja na Mtaji?? Unategemea Maisha bora kwa kila Mtanzania yangewezekana??

7,Wafanyakazi wengi wanakufa masikini kwa sababu Serikali inawanyonya mpaka kwenye mifupa, Mtu mshahara 300,000/= halafu take home 190,000/=, kweli hii ni sawa? Huko mijitu bila aibu inasema tumeongeza mafao ya wastaafu kwa 100% (kutoka 50,000/= hadi 100,000/=) kweli,Yaani Mzee wangu aliyelisotea Taifa lake kwa zaidi ya miaka 30 ya maisha yake leo unaona raha kumpa Mil 1 kwa mwaka?? Is it possible, aibu huwa mmezihifadhi wapi mnapotamka mambo kama haya? Mzee huyu bila shaka hata kiinua mgongo chenyewe alipata Mil 7, leo hii Wakurugenzi wa Mashirika ya Umma wanalipwa Zaidi ya Mil 35 kwa Mwezi,Mbunge Mmoja anajinyakulia Mil. 230, Unategemea Maisha bora kwa kila Mtanzania yangewezekana??

8,Mwekezaji wa madini anapokuja anapewa miaka Mitano ya kufanya kazi bila Kodi huku wazawa tukifungua tu Vibanda vya Chipsi hata kabla hajamazia kuisimamisha tunatakiwa tuonane na TRA na kodi kibao zisizo na Maana, Unategemea Maisha bora kwa kila Mtanzania yangewezekana??

Sisi siyo wavivu bwana,Mfumo wa Serikali kwa sisi Masikini unatuumiza Mno!! Labda Sijaielewa Thread yako Mkuu.
 
Back
Top Bottom