Papa Mopao
JF-Expert Member
- Oct 7, 2009
- 4,107
- 2,506
1. Kuna ule urafiki wa kufuatana kila mahali mpaka unaona watu wengine ni wapumbavu katika sayari hii, huu urafiki ni mbaya siku utakapopata shida watu hawatakujali kabisa maana haiwaingii mioyoni wao, wanakuchukulia kama vile huwajali heshima zao.
2. Kuna urafiki ambao ni kama bahari, kila mahali urafiki ni wa kubalance au wa kiasi, huu ni mzuri maana hata Mungu hupendezwa na hili, ni kama unajali unachokiona mbele ya macho yako au mbele ya mzunguko wa maisha yako na ya wengine.
3. Kuna ule urafiki wa kuchagua, urafiki wa pesa tu, au urafiki wa biashara tu, au urafiki wa usharobaro tu, au urafiki wa status ya juu au matawi ya juu katika madaraka! Lkn katika urafiki wa aina hii upo mzuri na mbaya vilevile, kuna urafiki unaodumu na ule haudumu kwa mema au mabaya. Wale ambao wanapenda kujishaua sana katika maisha yao kuonesha wao ni wa matawi sana hawakosekani humu.
Binafsi nafagilia sana ya kuwa na urafiki wa kama bahari, wa kubalance kutegemea na hali mawasiliano baina ya mtu na mtu! Ni rahisi kusukuma maisha kupitia urafiki wa aina hii.