maisha bila marafiki

The Boss

JF-Expert Member
Aug 18, 2009
49,110
115,884
ni kawaida watu wengi hata hapa jf kuzungumzia faida za kuwa na mpenzi

na hasara za kutokuwa nae.....

pamoja na yote mtu anaweza kuamua kuwa single kwa maana ya kutokuwa na mpenzi

lakini mara chache sana huwa tunazungumzia hasara au faida za kuwa au kutokuwa na marafiki au rafiki

hapa nazungumzia rafiki wa kawaida ambae most of times ni wa jinsia moja......

swali ambalo nimejiuliza ni hili

ni lazima mtu kuwa na rafiki/marafiki?????/

hasara za kuishi bila rafiki/marafiki?????

ni kwa nini hatungumzii saana uurafiki huuu na umuhimu wake?????

binafsi huwa nawaa admire wale ambao their best friend unakuta ni mkewe au mumewe

wewe je unaonaje????????

best wako ni mkeo/gf/bf/mumeo??????

kama sio,je huyo best wako anahusika vipi na life yako???????/

unaweza kuishi bila rafiki?????????????
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
mimi sina rafiki kabisa
naamanisha urafiki serious,nakumbuka wakati nikiwa mdogo nilikuwa na rafiki tuliyesoma wote
nafikiri ni ngumu sana kupata rafiki
lakini watu wa kawaida tunaongea vizuri tunaishi vizuri na tunakula vizuri pamoja,thats all
 
faida za kuwa na rafiki/marafiki ni nyingi, bt kubwa zaid ni kushea/ kubadilishana mawazo pale inapobidi. Kushea raha/karaha pale zinapotokea!
 
ukitaka kuona kama una marafiki wa kweli pata shida halafu jiulize ni nani ataweza kukusaidia hiyo shida yako. ndipo utakapogundua kuwa unafahamiana na watu wengi lakini una watu uwezao kuwaita marafiki wachache sana!
 
mie na wengi mpaka wengine natamani kuwafuta katika list langu...if you need i can give you some...
 
Tafiti nyingi zinzonyesha kua mtu aliye mpweke hua hana furaha na mra nyingi hupata msongo wa mawazo maana hana mtu wakumweleza matatizo yake na furaha zake.ila mtu aliwa na marafiki wengi wakumfariji wakati wa matatizo na wa kushirikiana nao wakati wa furaha mtu huyu huishi maisha marefu.nawasihi wana jf kuwa na marafiki na kuepuka upweke.
 
inategemea mkuu! kuna watu they ar good @sweating over petty issues! yaani kitu kidogo tu,kisirani kama nini sijui. wa hivyo bora awe mpweke kuliko kuhamaki kwa kila jambo. kupanga ni kuchagua, unaweza kuchagua kuwa na furaha wakati wote.
 
Wakizidi pia inakua kero tena uwachuje ni afadhali kua nao wachache lakini wenye busara kuliko wengi wakakuletea uzushi.
 
Si kweli wakati wote. Kuna wakati wingi wa marafiki ni kukaribisha drama maishani mwako maana hazitaisha. Kama hazikuhusu wewe moja kwa moja basi zitawahusu wenzako.
 
Nina rafiki mmoja tu wa kwel,2lianza urafki we2 tangu 2kiwa primary hadi leo 2ko chuon,bahati mbaya 2 ni kwamba mie niko ungwinin na yeye yuko coet,2nasaidiana kwa mambo meng sana..
 
Si dhani kama ni kweli zaidi ni kero tu ya ku accomodate kila tabia ya hao rafiki coz haiwezekani wote mkafanana tabia,labda tu kama ni walevi maana hao urafi wao ni wakudumu na hawahitaji kufahamiana ID ni beer
 
...nimefanikiwa kupunguza kwa kiwango kikubwa idadi ya "marafiki"...kwasababu rafiki wa kweli utamjua
kipindi cha shida. Kama alivyogusia mwenzangu aliyetangulia, muhimu kujuana/kufahamiana na wengi..
lakini kurundika 'spongers' hakusaidii lolote ila majuto mjukuu!...

Kwa sasa, marafiki zangu wa karibu ni Mpenzi wa roho yangu, familia yangu na wachache niliowa vet na
kuwakubali kuwa kwenye circle yangu..
 
"Rafiki Shafiki", whatever it means!

FF nimejikuta nacheka tu hapa mpenzi wangu dah!
Binafsi katika maisha yangu nimekuwa na rafiki mmoja ambaye kwa bahati mbaya amenisababishia maumivu makubwa maishani mwangu..but she cha ajabu she is still my friend!!

Faida:
kuwa na mtu mmoja unayemtrust ambaye unawezamweleza maswaibu yako ambayo hupendi family members wayajue!! Akiwa mzuri atakushauri vizuri.

Hasara: Kama si rafiki mzuri anaweza kukuletea mambo makubwa ukashangaa.
For me its better and safe to be without.......mambo ya best friend sijui kwa kweli I do not think kama yana faida kihiiivyooo
 
Aisee....(ofcoz najua nani ni rafiki yangu)

Wengi huwa tunachanganya kufahamiana na urafiki. Hapo ndo unajidanganya jumla! Wewe unamchukulia mtu kama rafiki yako kumbe mwenzio anakuona poa tu.


Bora kufahamiana tu (kimjini mjini) mi naona inatosha.
 
Mimi ninaelewana na kushirikiana vizuri na watu wanaonizunguka lakini sina rafiki kipenzi kwani niliwahi kuwa nae enzi za shule na nilikuwa namthamini kuliko ndugu yangu wa kuzaliwa,nilikuwa siwezi kula kitu peke yangu bila kumwekea,alikuwa anaumwa mara kwa mara na nilikuwa nikimuhudumia lakini siku niliugua mimi alihama hata chumba na nikateseka sana kitendo cha yeye kunitelekeza wakati wa taabu kiliniumiza sana mpaka sasa sitaki kuwa na urafiki wa kushibana na mtu.
 
Mimi kwangu kila mtu ni rafiki kwani nawakubali wote bila masharti,urafiki ni kusuku!
 
ukitaka kuona kama una marafiki wa kweli pata shida halafu jiulize ni nani ataweza kukusaidia hiyo shida yako. ndipo utakapogundua kuwa unafahamiana na watu wengi lakini una watu uwezao kuwaita marafiki wachache sana!
Wengi wamekua pamoja na kusoma pamoja, marafiki wachache sana
 
Urafiki wa siku hizi mashaka makubwa, rafiki kipenzi ndiye anayekukanyagia mkeo, Dada zako na ndugu wengine wa karibu. Ndie aliye mstali wa mbele ktk kukufitini ili usifanikiwe, unafiki ndio unamfanya aonekane mwema kwako lakini moyoni mwake anajuaye Mungu. Sio kama hakuna Marafiki wakweli lakini matatizo yao kuwa mengi na yanayofanana basi ni bora tu kufahamiana na watu vizuri kuliko urafiki.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom