Maige tunataka uturudishie Twiga wetu na wale Faru wa JK

Lifer

Member
Jan 28, 2007
36
27
Ezekiel Maige uliyekuwa Waziri wa Mali asili na utalii:

Chini ya uongozi wako, mwaka jana (2011) Tanzania tuliibiwa Twiga wanne (nembo ya taifa "national heritage") waliotoroshwa kwa kupitia uwanja wa ndege wa Kilimanjaro kwa vibali batili vilivyotoka wizara ya maliasili na utalii. Kama waziri wa wizara husika wakati huo, unawajibika moja kwa moja na huu ujangili wa hawa twiga wetu.

Wananchi: Tunataka uturudishie hawa Twiga wetu.

Hivi majuzi, mchana kweupe, Faru na mtoto wake (walioko kweney orodha ya "endangerd species") ambao JK aliwaomba kutoka South Africa ili wazaliane upya baada ya Faru tuliokuwa nao katika mbuga ya serengeti kuteketea karibu kumalizika kwaajili ya pembe, waliuwawa na pembe zao kuchukuliwa wakiwa chini uangalizi na ulinzi wa maafisa wa wizara yako. Hili pia limetokea wakati wewe ukiwa waiziri wa wizara husika. Unawajibika moja kwa moja na haya mauaji na huu ujangili wa Pembe.

Wananchi: Tunataka utulipe fidia kwa vifo vya hawa Faru na wizi wa Pembe zao.
 
..Waziri Membe anatakiwa aidai serikali ya Qatar iturudishie wanyama wetu.

..mbona suala la rada alilibebea bango lakini hili la wanyama amekuwa kimya??
 
Yaani hawa faru wamenisikitisha sana. Inaniuma, tunafanya jitihadi kuwalinda endangered species, halafu watu wanawauwa sababu ya pesa. Please watu wa usalama na mahakama, mkifanikiwa kuwakamata wauwaji, napendekeza adhabu yao iwe kifo! Wakifa hawana shida, coz sisi hatupo kwenye hatari ya kutoweka.
 
unataka Maige auze nyumba yake au malori yake?

Since yale malori yake yanaingiza US$ 20,000 kila mwezi, anauwezo kabisa wa kutulipa fidia ya Kifaru wetu na mtoto wake. ndani ya miezi mitano.

Nime research online, Cost ya kifaru mmoja na pembe zake on the black market, ni roughly US$ 50,000.
 
Ezekiel Maige uliyekuwa Waziri wa Mali asili na utalii:

Chini ya uongozi wako, mwaka jana (2011) Tanzania tuliibiwa Twiga wanne (nembo ya taifa "national heritage") waliotoroshwa kwa kupitia uwanja wa ndege wa Kilimanjaro kwa vibali batili vilivyotoka wizara ya maliasili na utalii. Kama waziri wa wizara husika wakati huo, unawajibika moja kwa moja na huu ujangili wa hawa twiga wetu.

Wananchi: Tunataka uturudishie hawa Twiga wetu.

Hivi majuzi, mchana kweupe, Faru na mtoto wake (walioko kweney orodha ya "endangerd species") ambao JK aliwaomba kutoka South Africa ili wazaliane upya baada ya Faru tuliokuwa nao katika mbuga ya serengeti kuteketea karibu kumalizika kwaajili ya pembe, waliuwawa na pembe zao kuchukuliwa wakiwa chini uangalizi na ulinzi wa maafisa wa wizara yako. Hili pia limetokea wakati wewe ukiwa waiziri wa wizara husika. Unawajibika moja kwa moja na haya mauaji na huu ujangili wa Pembe.

Wananchi: Tunataka utulipe fidia kwa vifo vya hawa Faru na wizi wa Pembe zao.

Nini maana ya kutumia neno wananchi? mkuu ushahidi unao tusaidie tumpeleke fisadi maige kortin.Your presantation of the matter here might trigger some inquinstive minds about this whole matter,taking into consideration the ongoing verbal war between Maige and Nape
 
wanyama hawawezi kuuzwa bila kibali cha JK au waziri
kuna mawili hapa either JK alijua hili au waziri alifanya bila JK kujua
hata hivo cha msingi kuna mtu wa kunyonga hapa
leo wameuza wanyama kesho watatuuza na sisi
afu anashinda kutwa kucha kujidai msafi wakati ni jizi tena nafuu ya jambazi
JK chukua hatua we want the head of this man ktk sinia.ni kosa kubwa mno kuuza rasilimali na urithi wetu
wakijenga migorofa huku sisi hata mlo wa mchana unakuwa tabu
chadema mkichukua nchi hawa watu anzeni nao kuwashughulikia mapema
 
Back
Top Bottom