Maige amwita Nape 'Gamba', Nape amjibu...

Mkuu maneno yako yamejaa busara.
Nape nimekushauri mara nyingi kuwa UNAPOONGEA USIMALIZE UBAKISHE MENGINE na USITUKANE MAMBA KABLA HUJAVUKA MTO. muda Si MREFU utafukuzwa ccm kama Jambazi sugu, Hio ndo ccm ambayo kila mtu kafunzwa kuchafua wengine ili apate madaraka, kama ulivyopata Madaraka kwa kuwachafua watu na wewe utatoka kwa kuchafuliwa 2
 
Maige kama kachanganyikiwa hivi, atulie kuukosa uwaziri siyo mwisho wa maisha. Ajifunze kuwa mkomavu katika siasa.

very true...isitoshe si ana ile biashara yake ya malori mawili ambapo kila lori moja linamuingizia USD 10,000/- kwa mwezi.

si akomae na malori mbona anaingiza pesa ya kutosha tu...USD 20,000 kwa mwezi ni karibu TSH. 30m kwa mwezi..anahitaji nini tena au kulikuwa na zaidi katika uwaziri zaidi ya pesa..aseme..afunguke...wakti ndiyo huu..2015 will be too late b'se tutamshika na M4C.
 
INANIPA FARAJA KUCHUKIWA NA KUSEMWA VIBAYA NA WAOVU( wezi na watumiaji vibaya wa rasilimali na dhamana za uongozi walizopewa). HII INANIFANYA NISONGE MBELE KUWATETEA WANYONGE NA MASIKINI WA NCHI YANGU DHIDI YA UNYANG'AU WA MAFISADI HAWA!

Huwa inauma na mafunzo kusema vibaya na wazalendo na wanyonge wenzangu, na imekuwa ni mafundisho mazuri kwangu. Lakini nikisemwa na mafisadi, wezi, watumiaji vibaya wa rasilimali za nchi, tena kwa kuumia tu kisa mirija yao imekatwa, kwangu ni faraja kubwa kwani inaonyesha vita dhidi ya matumizi ya rasilimali za nchi yetu inaenda vizuri na imekamata pazuri!

SITAKATA TAMAA, NITASONGA MBELE MPAKA TONE LA MWISHO LA DAMU YANGU. NCHI KWANZA VYAMA BAADAE!
 
Mkakati wako wa kuwavua wazee magamba umefikia wapi?

Vumilia, CCM ikikufia mkononi, Utakuwa umweka historia.

Quality
 
songa mbele mkuu, magamba mengine yakishindwa kutoka njoo CDM uvae gwanda ili tuyashikishe adabu, usikatishwe tamaa na baadhi ya magamba mkuu.
 
Willian kakojoe ulale Nape ni Gamba liko wazi tatizo udomo kaya kama Shibuda hatafakari maamuzi yake. Kuwa katibu mwenezi sio kwamba chama unakifanyia maamuzi bali unafanya maamuzi ya chama. Shirikisha wanachama na viongozi katika maamuzi. Na fikiri kabla ya kutenda
 
Kwenye uchambuzi wa magazeti ya leo asubuhi kupitia MAGIC FM nimesikia kauli ya Maige aliyenukuliwa na moja ya magazeti nchini akisema NAPE ni Gamba nambari moja na anatakiwa ajiuzulu.Hapa najiuliza je ni hasira tu za Mh Maige kuvuliwa nafasi ya uwaziri au ana hoja pale?.Naonba mchango wenu wanajamiiforums.
 
Bwana Nnauye kwa nini unamuogopa Maige kwa kuandika kwenye JF tu? Muambie yeye au umwajibishe kwenye vikao vya MAGAMBA.
 
Ukitaka mtu aseme ukweli wa rohoni mwake kwa ukweli kabisa, basi mguse vibaya patamu pake. Kila atakachokisema kitakuwa na ukweli zaidi. Ukibisha subiri watamchukulia hatua gani wale awasemao. Hukumbuki ya Augustino wa Kiraracha? Watabaki kumtisha tu lakini wataogopa kumgusa asije akatoboa siri zaidi. Mahakamani waendesha mashitaka watakuchokoza makusudi halafu unapandisha hasira, kisha majibu utakayotoa kwa hasira ndiyo sahihi zaidi. ndio maana inashauriwa uweke advocate usijiwakilishe mwenyewe kama una roho kama ya kiwavi.
 
Maige bana sasa unapanic nini si utulie tu ufanye ile biashara yako na dadako inayokulipa $20,000 a month? mbona unatweta sana Maige
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom