Maige afichua siri nzito maliasili

KIM KARDASH

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
5,139
1,139
KUTEMWA UWAZIRI: Maige afichua siri *Mwanasheria ajipanga kuchukua hatua *Kuanika uozo wa Maliasili bungeni

Na Salim Nyomolelo

ALIYEKUWA Waziri wa Maliasili na Utalii, Bw. Ezekiel Maige, amefichua siri nzito zilizochangia kung'olewa katika wizara mojawapo ikiwa ni kugusa maslahi vigogo wenye nguvu kubwa na ushawishi wa hali ya juu.

Bw. Maige ilifichua siri hiyo jana kupitia ujumbe wake alioutoa kwenye mtandao wa kijamii.

Aliongeza kuwa maamuzi aliyokuwa akiyatoa wakati akiwa waziri wa wizara hiyo alijua fika kuwa hayawafurahishi vigogo hao.

"Kwa kifupi sana, niwafahamishe kuwa yaliyotokea ni ushahidi kwamba maliasili ni ngumu... ni ngumu kukabiliala na wabaya. Wapo waliojipanga ukiwavamia hovyo hovyo unaondoka wewe," alisema Bw. Maige na kuongeza; "Ndivyo ilivyotokea."

Alisema maamuzi yake aliyokuwa akisimamia ndiyo yamemfanya yamfike yaliyotokea. Alisema akiwa wizarani alisimamia sheria na kuwapa vitalu Watanzania maskini wenye sifa na kuwaacha wazungu kama sheria ilivyoelekeza.

"Ni Waziri gani aliyewafikisha mahakamni watorosha twiga akina Kamrani na wenzake? Watu wametumia records (kumbukumbu) za matukio ya mwaka 2009/10 kuficha matendo na maamuzi ya kishujaa ya Maige ya 2011," alisema Bw. Maige na kuongeza;"Yawezekana hawakutaka nipate sifa, lakini ipo siku nitaipata. Tena si siku nyingi.

Niliwaomba wenzangu wamwogope Mungu...bado nasisisitiza hivyo."Alihoji kuwa; "NI waziri gani aliyefunga biashara ya wanyamahai, ni waziri gani aliyeonesha mfano wa kuchukua hatua kwa watumishi pale alipoona hawatendi sawa? Lakini mimi sikusita kuchukua hatua."

Alisema anawahakikishia wazalendo kuwa wamepoteza mpambanaji aliyejitolea kupambana na wahalifu angani, majini, porini, mijini na vijijini ndani na nje ya nchi.

Bw. Maige alisema alitumia kila aina ya uwezo wake kuzawadia taifa lake utumishi uliotukuka.

Alisisitiza kuwa maamuzi hayo magumu yamegusa watu wenye nguvu na ushawishi mkubwa. "Nilitegemea vita hii, na ninaamini tutashinda," alisema Bw. Maige akinukuu maneno aliyowahi kuyatamka Bungeni na kuongeza;"Watanzania wapenda haki wanisikilize kwa makini muda haukuruhusu, ila nitarudi bungeni na nitasema."

Kuhusu sakata la nyumba alisema suala hilo amelifafanua na kutoa vielelezo. "Kila mbunge aliyetaka alikopeshwa sh. milioni 290, wengine wameanzisha biashara na wengine wamenununua magari na wengine majumba," alisema.

Alisema mwenye mashaka aende kwa Msajili wa Hati Wizara ya Ardhi, au kwa kamishna wa maadili, au CRDB tawi la Azikiwe na Dodoma alikokopa au amtafute muuzaji.

Alisema maeneo yote hayo atapata rekodi ya bei. "Wapo wahuni, kwa maslahi ya kisiasa na chuki binafsi wametangaza bei tofauti na niliyonunulia...mwanasheria wangu anashughulikia suala hilo," alisema Bw. Maige.

Kwa upande wa ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Bw. Maige alisema haikumgusa, kwani ilikuwa inaishia Juni 2010, wakati yeye alipewa dhamana ya kuongoza wizara hiyo Novemba 2010.

Kuhusu biashara ya wanyamahai, Bw. Maige alisema hakuna wanyama waliosafirishwa kinyume cha sheria wakati wa uongozi wake mwaka 2011 na kuwa matukio ya utoroshaji yalipobainika, walifungua mashitaka kwa watuhumiwa na kufunga biashara hiyo.

Aliahidi kuwawakilisha wananchi wa Jimbo lake la Msalala kwa mujibu wa katiba na ahadi zake kwao atazitekeleza hadi 2015 watakapopata fursa ya kuamua vinginevyo. Bw. Maige kabla ya kuteuliwa kuwa waziri kamili wa wizara hiyo mwaka 2010, alikuwa naibu waziri akiwa chini ya Bi. Shamsa Mwangunga.

Ujumbe wa Maige Kutoka Facebook

Ndugu zangu na rafiki zangu. Kwanza niwape pole kwa mshituko mlioupata kwa haya yaliyojitokeza. Naomba msisikitike sana. Kila jambo alilopanga Mola hutokea kadiri ya mapenzi yake. Route ya maisha ya mwanadamu hupangwa na Mola mara tu anapompulizia pumzi ya uhai. Hili lilipangwa hata kabla sijatokea duniani miaka 42 iliyopita!

Mungu hakushindwa kumwokoa mwanawe Yesu asisulubiwe, tena kwa kuonewa! Hasha, tungeupataje ukombozi bila hilo kutokea? Wakati mwingine Mungu hutoa nafasi kwa mambomagumu kuwafika waja wake, si kwamba hawapendi,bali ili unabii utimie. Ilifika wakati hata Yesu akaona kama Mungu kamuacha! Hasa sisi kwa hili tunaweza kudhani Mungu katuacha! Hasha, ni njia ya kuufikia ukombozi wa kweli.

Pili, kwa kifupi sana, niwafahamishe kuwa, yaliyotokea ni ushahidi kwamba maliasili ni ngumu. Kukabiliala na wabaya ni kazi ngumu. Wapo waliojipanga ukiwavamia ovyoovyo unaondoka wewe. Ndivyo ilivyotokea.

Niwahakikishie, wazalendo wamepoteza mpambanaji. Nimepambana na wahalifu angani, majini, porini, mijini na vijijini ndani na nje ya nchi. Nilitumia kila aina ya uwezo wangu kulizawadia taifa langu utumishi uliotukuka. Sikubakisha chembe ya energy.

Waziri gani aliyesimamia sheria na kuwapa vitalu watanzania maskini wenye sifa na kuwaacha wazungu kama sheria ilivyoelekeza?

Waziri gani aliyewafikisha mahakamni watorosha twiga akina Kamrani na wenzake? Watu wametumia records za matukio ya 2009/10 kuficha matendo na maamuzi ya kishujaa ya maige ya 2011. Yawezekana hawakutaka nipate sifa, lakini ipo siku nitaipata. Tena si siku nyingi. Niliwaomba wenzangu wamwogope Mungu. Bado nasisisitza hivyo, si Mungu wangu kama ilivyodhaniwa, bali Mungu wetu wa haki.

Waziri gani aliyefunga biashara ya wanyamahai?

Waziri gani aliyeonyesha mfano wa kuchukua hatua kwa watumishi pale alipoona hawatendi sawa? Maige hakusita kuchukua hatua.

Maamuzi haya ni magumu na yamegusa watu wenye nguvu na ushawishi mkubwa. Nilitegemea vita hii, na ninaamini tutashinda. Nilisema Bungeni, watanzania wapenda haki wanisikilize kwa makini. Muda haukuruhusu, ila nitarudi Bungeni na nitasema.

Imesemwa issue ya nyumba. Nimefafanua na kutoa vielelezo. Kila mbunge aliyetaka amekopeshwa shs 290m, wengine wameanzisha biashara na wengine wamenununua magari na wengine majumba. Wapo walioficha, na tupo tuliojiweka wazi! Mkopo wangu huo umekuwa my contribution na balance kulipwa na benki na nyumba kuimortgage. Nimetoa nyaraka zote kwa wanahabari na vyombo vyote husika. Nimesema mwenye mashaka aende kwa Msajili wa hati wizara ya ardhi, au kwa kamishna wa maadili, au CRDB Azikiwe na Dodoma nilikokopa au amtafute muuzaji. Kote huko utapata rekodi ya bei na mode of payment. Wapo wahuni, kwa maslahi ya kisiasa na chuki binafsi wametangaza bei tofauti na niliyonunulia. Manasheria wangu anashughulikia hilo.

Niwahakikishie, vita nimepigana, imani na dhamana nimeilinda, muda wa kutuzwa na mwenye kumbukumbu sahihi, Mungu utafika. Naamini nimejiwekea akiba isyooza Mbiguni.

Yapo mengi yasiyo sahihi yaliyosemwa. Nitakuwa nafafanua kila nipatapo fursa na muda utazidi kutufunua. Kwa kifupi, kwa suala la vitalu, hakuna kampuni hata moja iliyopewa kitalu cha uwindaji bila kuomba, kukaguliwa na kamati ya ushauri na hatimaye kupewa alama. Kampuni zisizokuwa na sifa ni zile zilizopata chini ya alama 50. Na kwa kampuni zilizokuwa kwenye biashara, passmark ni alama 40 kwa mujibu wa kanuni ya 16(5) ya kanuni za uwindaji wa kitalii za mwaka 2010. Hakuna kampuni iliyopata chini ya alama 50 iliyopata kitalu. Hakuna kampuni ya kizalendo iliyopendekezwa na kamati ya ushauri ambayo haikupewa kitalu.

Kwa upande wa report ya CAG, haikunigusa binafsi kwani ilikuwa inaishia juni 2010 wakati mimi ilishika dhamana Novemba 2010.

Ka upande wa biasharaya wanyamahai, hakuna wanyama waliosafirishwa kinyume cha sheria wakati wangu (2011), na matukio ya utoroshaji tulipoyabaini, tulifungua mashitaka kwa watuhumiwa nakufnug biashara hiyo.

Naanza kazi ya kuwawakilisha wananchi wa Msalala. Nitawawakilisha kwa mujibu wa katiba na ahadi zangu kwao hadi 2015 watakapopata fursa ya kuamua vinginevyo.

Mara nyingi watenda mema hufanyiwa hiyana. Ka wakristo, naomba msome Mwanzo 4:1-15.

Wasalaam.
 
KUTEMWA UWAZIRI: Maige afichua siri *Mwanasheria ajipanga kuchukua hatua *Kuanika uozo wa Maliasili bungeni

Na Salim Nyomolelo

ALIYEKUWA Waziri wa Maliasili na Utalii, Bw. Ezekiel Maige, amefichua siri nzito zilizochangia kung'olewa katika wizara mojawapo ikiwa ni kugusa maslahi vigogo wenye nguvu kubwa na ushawishi wa hali ya juu.

Bw. Maige ilifichua siri hiyo jana kupitia ujumbe wake alioutoa kwenye mtandao wa kijamii.

Aliongeza kuwa maamuzi aliyokuwa akiyatoa wakati akiwa waziri wa wizara hiyo alijua fika kuwa hayawafurahishi vigogo hao.

"Kwa kifupi sana, niwafahamishe kuwa yaliyotokea ni ushahidi kwamba maliasili ni ngumu... ni ngumu kukabiliala na wabaya. Wapo waliojipanga ukiwavamia hovyo hovyo unaondoka wewe," alisema Bw. Maige na kuongeza; "Ndivyo ilivyotokea."

Alisema maamuzi yake aliyokuwa akisimamia ndiyo yamemfanya yamfike yaliyotokea. Alisema akiwa wizarani alisimamia sheria na kuwapa vitalu Watanzania maskini wenye sifa na kuwaacha wazungu kama sheria ilivyoelekeza.

"Ni Waziri gani aliyewafikisha mahakamni watorosha twiga akina Kamrani na wenzake? Watu wametumia records (kumbukumbu) za matukio ya mwaka 2009/10 kuficha matendo na maamuzi ya kishujaa ya Maige ya 2011," alisema Bw. Maige na kuongeza;"Yawezekana hawakutaka nipate sifa, lakini ipo siku nitaipata. Tena si siku nyingi.

Niliwaomba wenzangu wamwogope Mungu...bado nasisisitiza hivyo."Alihoji kuwa; "NI waziri gani aliyefunga biashara ya wanyamahai, ni waziri gani aliyeonesha mfano wa kuchukua hatua kwa watumishi pale alipoona hawatendi sawa? Lakini mimi sikusita kuchukua hatua."

Alisema anawahakikishia wazalendo kuwa wamepoteza mpambanaji aliyejitolea kupambana na wahalifu angani, majini, porini, mijini na vijijini ndani na nje ya nchi.

Bw. Maige alisema alitumia kila aina ya uwezo wake kuzawadia taifa lake utumishi uliotukuka.

Alisisitiza kuwa maamuzi hayo magumu yamegusa watu wenye nguvu na ushawishi mkubwa. "Nilitegemea vita hii, na ninaamini tutashinda," alisema Bw. Maige akinukuu maneno aliyowahi kuyatamka Bungeni na kuongeza;"Watanzania wapenda haki wanisikilize kwa makini muda haukuruhusu, ila nitarudi bungeni na nitasema."

Kuhusu sakata la nyumba alisema suala hilo amelifafanua na kutoa vielelezo. "Kila mbunge aliyetaka alikopeshwa sh. milioni 290, wengine wameanzisha biashara na wengine wamenununua magari na wengine majumba," alisema.

Alisema mwenye mashaka aende kwa Msajili wa Hati Wizara ya Ardhi, au kwa kamishna wa maadili, au CRDB tawi la Azikiwe na Dodoma alikokopa au amtafute muuzaji.

Alisema maeneo yote hayo atapata rekodi ya bei. "Wapo wahuni, kwa maslahi ya kisiasa na chuki binafsi wametangaza bei tofauti na niliyonunulia...mwanasheria wangu anashughulikia suala hilo," alisema Bw. Maige.

Kwa upande wa ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Bw. Maige alisema haikumgusa, kwani ilikuwa inaishia Juni 2010, wakati yeye alipewa dhamana ya kuongoza wizara hiyo Novemba 2010.

Kuhusu biashara ya wanyamahai, Bw. Maige alisema hakuna wanyama waliosafirishwa kinyume cha sheria wakati wa uongozi wake mwaka 2011 na kuwa matukio ya utoroshaji yalipobainika, walifungua mashitaka kwa watuhumiwa na kufunga biashara hiyo.

Aliahidi kuwawakilisha wananchi wa Jimbo lake la Msalala kwa mujibu wa katiba na ahadi zake kwao atazitekeleza hadi 2015 watakapopata fursa ya kuamua vinginevyo. Bw. Maige kabla ya kuteuliwa kuwa waziri kamili wa wizara hiyo mwaka 2010, alikuwa naibu waziri akiwa chini ya Bi. Shamsa Mwangunga.

Maige could be a good Finance Minister
 
Aliahidi kuwawakilisha wananchi wa Jimbo lake la Msalala kwa mujibu wa katiba na ahadi zake kwao atazitekeleza hadi 2015 watakapopata fursa ya kuamua vinginevyo. Bw. Maige kabla ya kuteuliwa kuwa waziri kamili wa wizara hiyo mwaka 2010, alikuwa naibu waziri akiwa chini ya Bi. Shamsa Mwangunga.

Hivi muda wote alikuwa hawawakilishi wananchi wake hadi kibarua cha uwaziri kilipoota nyasi. Lakini mbona Maige analalamika sana kana kwamba aligombea ubunge kwa lengo la kuwa waziri na sio kuwatumikia wananchi wa jimbo lake.

Watu kama Maige sio wa kuwapa madaraka kabisa. Kwa anayofanya sasa anaonekana ni mbinafsi sana na ana uroho wa madaraka!!!
 
Inasaidia nini kama ameamua kuongea baada ya meli kuzama kabisa? Na yeye ni muhusika wa madudu hayo hawezi kukwepa
 
Mbona asiliseme kabla?aache kujitetea amepigwa chini akae kimya,nani asiyeujua huu mfumo mbovu?
 
Yaah. Nakubaliana naye lakini isije ikawa ni kwa nia mbaya kuyaelezea yote haya bungeni. Ayafanye yote haya kwa nia ya kurekebisha palipo pabovu ili raslimali za Taifa hili ziyanufaishe makundi yote ya jamii
 
Maige nimemuelewa vizuri sana,kuna kitu kimoja wanajamvi tunakisahau hata wewe unapochaguliwa kuongoza sehemu na hauna budi kuongoza kutokana na maelekezo atakayokuwa anakupa.maana ya maige nini kwamba matatizo yote yaliyotokea si yeye yamesababishwa na wakubwa yeye kama yeye hawezi kuzuia matakwa ya wakubwa,ni ukweli ulio wazi kwamba viongozi wengi hawafanyi kazi kwa utashi wao au ujuzu wao.ndio maana tunaludi nyuma kimaendeleo kila kukicha.
sabuni kipande tsh 500/-?kibiriti tsh 100/-?
 
Its to late angekuwa mwanaume angefunguka siku mabalaa yalipo kuwa yanamwandama bungeni ametoka ndo unafunguka tehe tehe bongo bwana atukosi visingizio.Kina mkulo nao watakuja kwa style hii mtaniambia
 
mr maige binafsi sikubaliani na hoja zako .
Mosi, kabla ya kuwa waziri ulikuwa naibu kwa wizara hiyo hiyo!
Ulifanya nini kama naibu madudu yalipotendeka?
Au unatwambia kuwa naibu ni sawa na kuwa mfungwa asiye na kauli ?
Wewe ni mtuhumiwA No 1!!!!!
 
Maige wacha kutapatapa kijana wangu,hii ni Dunia na uwaziri sio maisha ile ni ajira,hvy ulipaswa kuitumikia kwa hali na mali,sasa kilicho kungusha unakijua vizuri.
Kuwapa Maskini wenzangu kitalu sikatai kabisa, ila inakuwaje anapewa mtu kitalu ambaye hata ofisi hana?hana Idea ya Indsrty hy kwasababu tu ni mfanya biashara na ana hela na amekuhonga?unaaacha kutoa ushauri kwa hao watanzania waweze hata kuingia ubia na wenye uzoefu wa kazi hy ikiwa ni njia rahisi za kuwateka na kuwandoa wazungu taratibu bila wao kujielewa,
Wizara hii ni nyeti mno,mchezo uliokuwa unaufanya ndo umekutoa hapo huna sababu ya kumlaum mtu yeyote,pale hakuna siasa ila ulipaswa pia kusikiliza wataalam wa wizara na Idara za utafiti,sasa wewe umekunja zako mfukoni then unanza kulaum wenzako wakati mkosaji wewe.
Nakumbuka kulikuwa na kamati ya ku kaguwa makampuni yooote yaliyo omba vitalu,ripoti unayo,na umeona sisi watanzania tuko wapi ukilinganisha na wenzetu,sasa kwanini usichukue maamuzi ya kuwaunganisha si ktk kampuni kwamfano kitalu kimoja ukampa mgeni aliyekaa nacho kwa muda mrefu ila kwa masharti ya kuingia ubia na mtanzania.
Maige acha kelele sifa unazozitaka hazina maana,ushapoteza mwelekeo kaa kimya,ulitaka ukae kwenye hy wizara milele maana inaonekana imekuuma sasa,umeshindwa acha kaa kumya fanya shughuli zako.
 
Usilie sana Maige,acha wanaichi wataamua,mshtuko ulikuwa kwa wewe kutajirika gafla kwa kuwa na malori,nyumba ya dolla 450....au $750,hivi ni ubunge tu ndio unalipa kiasi hicho mheshimiwa???
 
Maliasili na ardhi kuna watu wakorofi sana ambao huwatetemesha mpaka mawaziri,nadhani mnamkumbuka severe wa maliasili alivyomtingisha Antony diallo na matokeo yake diallo akaondoka pale,na wamekua wakiwatambia mawaziri kwamba utaondoka utatuacha wamekuja wangapi hapa?

lakinio maige mimi naamini anachokisema,kiukweli alijitahidi sana sema pale pagumu nilijua tu hatawaweza wale hasa baada ya kipindi fulani kupigana kufa na kupona kuhakikisha anaifuta safari ya vigogo kwenda kujifunza utalii hongkong wakiwemo na wajumbe wa bodi ya utalii kina Halima mamuya,tena huku wakiwa wameshalipana na posho,mbona zilirudi jinsi dogo maige kwa kushirikiana na mzee msekwani board chairman.
 
Jamaa alikua jembe,soma Habari kamili-source Raia mwema 17 Aug 2011

Safari ya matanuzi ya vigogo yazimwa
Mwandishi Wetu
Toleo la 199
17 Aug 2011

* Walikuwa waende Hong Kong kwa ziara ya siku 10
* Waziri Maige, Msekwa waipiga ‘stop' dakika za mwisho
* Ingeteketeza mamilioni ya pesa za walipa kodi
* Walipanga kusafiri daraja la kwanza

KATIKA kile kinachoonekana kuwa ni kupambana na matumizi mabaya ya fedha za umma, Waziri wa Maliasili na Utalii, Ezekiel Maige "amezima" jaribio la watumishi tisa na wajumbe wanne wa Bodi ya Mamlaka ya Hifadhi ya Bonde la Ngorongoro (NCAA) kusafiri kwenda Hong Kong kwa lengo la kujifunza shughuli za utalii.

Habari za uhakika ambazo Raia Mwema limezipata zinasema kwamba hatua yake hiyo imesaidia kuokoa Shilingi milioni 120 ambazo zingeteketea kama ziara hiyo ya siku 10, iliyoelekea kuwa ya kitalii zaidi kuliko ya kujifunza, ingefanyika.

Hatua hiyo imekuja ikiwa ni mwezi mmoja tu tangu Waziri huyo kupiga marufuku kusafiri nje menejimenti ya mamlaka hiyo inayoongozwa na Mhifadhi Mkuu, Bernard Murunya kwa mwaka mzima baada ya kubaini kuwa wameshindwa kutekeleza majukumu yao ya msingi ya kusimamia shughuli za uhifadhi na utalii katika bonde hilo.

Uamuzi huo wa kumwekea "karantini" ya kutokusafiri nje ya nchi Mhifadhi huyo na wenzake kwa mwaka mzima, umekuja baada ya kubainika kuwa katika kipindi cha mwaka moja pekee, watendaji wa mamlaka hiyo na baadhi ya wajumbe wa bodi, wametumia mamilioni ya shilingi kwa safari za nje; huku wananchi wanaoishi ndani ya bonde hilo wakikabiliwa na njaa kali.

Maige alifikia uamuzi huo mgumu wakati alipofanya ziara ya siku mbili ndani ya Mamlaka hiyo kukagua shughuli mbalimbali za uhifadhi pamoja na miradi kadhaa ya maendeleo ambako alipokelewa kwa mabango na wananchi waliokuwa wakiilalamikia menejimenti ya NCAA kwa kushindwa kuwahudumia kutokana na watendaji kusafiri kila mara.

Taarifa zilizolifikia Raia Mwema na kuthibitishwa na vyanzo kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya NCAA, Pius Msekwa, wiki iliyopita, zilieleza kuwa Mhifadhi huyo alikuwa asafiri na ujumbe wa watu 12 wakiwamo wajumbe wanne wa Bodi, Agost 6, 2011, kwa ndege ya shirika la Emirates kwenda Hong Kong katika kile kinachoitwa kuwa ni "ziara ya kujifunza" shughuli za utalii nchini humo.

Habari zaidi zinawataja waliokuwa wasafiri kuwa ni pamoja na Mjumbe wa Bodi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha na Utawala na kingozi wa msafara huo, Halima Mamuya. Mamuya alikuwa mbunge wa viti maalumu (CCM) kwa vipindi viwili kati ya mwaka 2000-2005 na 2005-2010 baada ya kushindwa katika kura za maoni.

Wajumbe wengine ni Mbunge wa Bukoba, Deogratius Ntukamazima, Mkurugenzi wa Bodi, Fatma Simba na Mhandisi George Kaidoh, Mhandisi Joseph Mallya na Veronica Ufunguo wa idara ya uhifadhi na utalii.

Wengine ni Mhandisi Ezra Misana, Meneja Utumishi na Raslimali Watu, Ringbert Marcos, Meneja Idara ya Fedha, Shadrack Kyambile, Naibu Meneja Huduma za Sheria, Yusuf Machumu na Meneja Uhusiano, Adam Akyoo.

Taarifa zinasema, hata hivyo, ya kuwa ndoto za ujumbe huo kusafiri nje zilizimwa baada ya Maige kutumiwa taarifa za safari hiyo na baadhi ya wafanyakazi wa ngazi za chini ambao walimtumia ujumbe wa simu (sms) waziri huyo na kumweleza siri ya safari hiyo.

Baada ya kupokea ujumbe huo, inaelezwa kuwa Maige aliwasiliana na baadhi ya watendaji wa Menejimenti ambao walijaribu kujenga hoja kuwa safari hiyo ilikuwa muhimu sana kwa maendeleo ya shughuli za utalii wa mamlaka hiyo.

Hata hivyo, inadaiwa kuwa Waziri Maige alikataa ushawishi huo, na ndipo alipompigia simu Mwenyekiti wa Bodi ya Ngorongoro, Mzee Pius Msekwa ambaye naye alimwagiza Mhifadhi Murunya na kiongozi wa msafara, Halima Mamuya kuvunja na kusitisha safari hiyo.

Akimkariri Waziri Maige, mtoa habari wetu alieleza kuwa Waziri alikuwa amekasirishwa sana na "kiburi" cha watumishi hao kupuuza maagizo yake aliyotoa mwezi uliopita kuwa hawataruhusiwa kusafiri nje ya nchi kwa mwaka mzima hadi watakapojirekebisha hasa katika kutekeleza majukumu ya kazi zao.

Aidha, imeelezwa pia ya kuwa Waziri Maige pia alipinga kuwa ziara za aina hiyo hazina tija kubwa kwa mamlaka hiyo zaidi ya kutafuna posho za mamlaka, kwani kazi ya kutangaza utalii ilitakiwa ifanywe na Bodi ya Utalii nchini (TTB) badala ya mashirika yanayoshughulikia usimamizi wa hifadhi kufanya kazi akitoa mfano wa NCAA na TANAPA.

Watoa taarifa wetu wameeleza pia kwamba kimsingi, Waziri Maige pia alikasirishwa na wingi wa wajumbe waliokuwa wanakwenda safari hiyo na ilionekana kuwa wanakwenda kutalii badala ya kwenda kujifunza kwa kuwa kuna baadhi ya ambao walikuwa wasafiri wasifu wao hauendani na shughuli za kutangaza utalii.

"Mzee Msekwa alipopata simu ya Waziri alitoa amri haraka na kuwaagiza watumishi hao kusitisha haraka safari hiyo na kuwaonya kuwa iwapo hawatatekeleza, basi, wangechukuliwa hatua za kinidhamu", alieleza mtoa taarifa wetu kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii.

Taarifa zaidi zilizokusanywa na Raia Mwema zinaeleza kuwa ujumbe huo ungeteketeza kiasi cha dola za Kimarekani 72,200 ambazo ni karibu sawa na shilingi za Kitanzania milioni 120.

Dola moja ya Kimarekani kwa sasa hununuliwa kwa Shilingi kati ya 1,650 hadi 1,660 katika maduka mengi ya kuuzia fedha na bei hiyo hutegemeana na nguvu ya soko.

Katika safari hiyo, kila mjumbe wa bodi angelipwa posho ya dola za Kimarekani 6,000 wakati wajumbe wengine wangelipwa dola 5,600 ambazo ni karibu sawa na sawa na shilingi 9,240,000, na fedha hizo ni mbali na gharama za tiketi ya ndege ya daraja la juu (business class) ya kwenda na kurudi Hong Kong ambayo ingegharimu dola zaidi ya 1,500 kwa kila mjumbe.

"Kila mjumbe alikuwa alipwe posho dola za Kimarekani 5,600, na fedha hizo ni tofauti na gharama za tiketi za ndege ya shirika la Emirates, " aliongeza mtoa habari wetu.

Takwimu zinaonyesha ya kuwa NCAA imetenga kiasi cha shilingi bilioni 2.4 kwa safari za nje ya nchi na watumishi hufanya safari 32 kwa mwaka ambazo ni sawa na wastani wa safari tatu kwa kila mwezi katika maeneo mbalimbali duniani kwa kigezo cha kutangaza utalii.

Mamlaka hiyo pia hutoa kiasi cha shilingi milioni 789 kwa Wizara ya Maliasili na Utalii na shirika la TTB kama fedha za kutangaza utalii nje ya nchi na pia hutoa milioni 327 kwa ajili ya matangazo kwenye michezo ya Ligi Kuu ya mpira wa miguu ya Uingereza.

NCAA pia hutoa shilingi milioni 35 kwa ajili ya matangazo katika gazeti la US Today la nchini Marekani na Support Tourism Office iliyoko nchini Abudhabi (Falme za Kiarabu) shilingi milioni 24.

Matumizi ya fedha hizo hata hivyo yanakwenda kinyume na utafiti wa mtaalamu wa shughuli za Utalii nchini Dk.Victor Appolo Lunyoro aliyoipa kichwa cha habari Global Tourism Marketing Campaign, The case of Ngorongoro Conservation ya mwaka 2009 ambayo inaeleza kuwa ziara ya mafunzo au maonyesho huchangia asilimia mbili tu ya watalii wanaotembelea Bonde hilo.

Katika mchanganuo wake mtaalamu huyo anabainisha kuwa asilimia 34 ya watalii wanaotembelea Bonde hilo ni wale waliosikia kwa ndugu na jamaa zao waliokwishaku tembelea, asilimia 27.5 ni watalii wanaopata taarifa kupitia kwa kampuni za uwakala wa utalii, asilimia 17.9 hupata taarifa kupitia mitandao na tovuti mbalimbali, asilimia 1 kupitia vipeperushi, asilimia 0.2 maonyesho na nyinginezo asilimia 6.7.

"Kwa mchanganuo huo utaona kuwa bajeti ya matangazo ya mamlaka ni karibu shilingi bilioni 4 kwa mwaka na asilimia 70 ya fedha hizo hutumika kwa safari za nje ya nchi na ndiyo maana Waziri ameamua kuingilia kati kwani inaonekana kuwa kuna ufujaji wa fedha makusudi unaofanywa na watumishi na ndiyo sababu ya kumtumia Mwenyekiti wa Bodi Mzee Msekwa," alieleza mtoa taarifa wetu.

Akizungumzia hatua hiyo ya kupiga "stop" safari hiyo, Mwenyekiti wa Bodi ya NCAA, Pius Msekwa alilithibitishia Raia Mwema kwa njia ya mawasiliano ya simu kuwa ni kweli wamefuta ziara hiyo ya kwenda Hong Kong kwa kufuatia maagizo ya Waziri Maige.

"Ni kweli safari imefutwa na hiyo ni utekelezaji wa agizo la Waziri, na watumishi lazima watekeleze jambo hilo; vinginevyo watakuwa wanakwenda kinyume cha maagizo halali ya Serikali", alisema Mzee Msekwa.

Msekwa, ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), alieleza kuwa hafahamu gharama halisi za safari hiyo lakini akaongeza kuwa fedha nyingi zingetumika kugharimia safari ya ujumbe huo.

"Sina takwimu sahihi za gharama hapa mbele yangu, lakini najua safari kama hizo zinatumia fedha nyingi ila kwa sasa hakuna safari na Waziri ameagiza, na maagizo yake yametekelezwa", alisisitiza Msekwa.

Kwa upande wake, kiongozi wa msafara huo, Halima Mamuya, alikataa kuzungumzia nia na madhumuni ya safari hiyo; hasa wakati ambapo Waziri alikwishakutoa maelekezo kuwa safari za nje zifutwe ili kubana fedha za Mamlaka hiyo.

"Kwanza nani kakuambia taarifa hizo? Mimi sijui chochote. Waulize watu wa NCAA. Mimi ni mjumbe tu wa Bodi. Siwezi kuzungumzia masuala ya Menejimenti ya Ngorongoro", alijibu Mamuya; huku akilaumu waandishi wa habari kwa kumfuatafuata.

Naye Msemaji wa NCAA, Adam Akyoo, alisema kua ni kweli safari hiyo imefutwa, lakini walikuwa wamefuata taratibu zote za kiserikali za mtumishi kusafiri nje ya nchi ikiwa ni pamoja na kujaza fomu ya safari kupitia kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya hiyo na Idara ya Utumishi.

Akyoo alisema safari hiyo ilikuwa ya kawaida na nia na madhumuni yake ilikuwa kwenda kujifunza pamoja na kutangaza utalii katika maonyesho ya utalii na utamaduni huko Hong Kong barani Asia.

"Safari unayoizungumzia haikuandaliwa kwa kificho. Kila kitu kilikuwa wazi na taratibu zote za kiserikali zilifuatwa ikiwa ni pamoja na ujazaji wa fomu za safari ili kupata ruhusa", alisema Akyoo.

Aliongeza kuwa, hata hivyo, Menejimenti inaheshimu hatua zilizochukuliwa na Waziri, na hawana kinyongo na hatua yake ambayo ina maslahi kwa ustawi wa Mamlaka yao na akasisitiza kuwa safari hiyo ilikuwa na uwazi wa kutosha na hakukuwa na upindaji wa sheria za utumishi.

Waziri Maige hakupatikana kupitia simu yake ya mkononi kuelezea sababu za kusitisha safari ya wajumbe hao; kwani ilielezwa kuwa yuko mjini Dodoma akijiaandaa kuwasilisha bajeti ya Wizara yake ndani ya wiki hii.

Wachunguzi wa mambo wanaeleza kuwa fedha hizo – Shilingi milioni zaidi ya 120 ambazo zingetumika ndani ya siku 10 tu, zinaweza kutosha kununua tani 343 za mahindi ambazo zingewasaidia wananchi wanaokabiliwa na njaa kali ndani ya hifadhi ya Ngorongoro zingeweza kusaidia familia zenye njaa kwa zaidi miezi minne
 
Hamna jembe hapo huyu Maige ni Wembe siyo jembe.
Kuzuia safari ya 120m na kuzuia Twiga asisafirishwe imeichukuliaje hapo? Pima ratio.
Hiyo ni kuzuga tu aonekane anafanya kazi, hakuna kitu hapo
 
Hivi muda wote alikuwa hawawakilishi wananchi wake hadi kibarua cha uwaziri kilipoota nyasi. Lakini mbona Maige analalamika sana kana kwamba aligombea ubunge kwa lengo la kuwa waziri na sio kuwatumikia wananchi wa jimbo lake.

Watu kama Maige sio wa kuwapa madaraka kabisa. Kwa anayofanya sasa anaonekana ni mbinafsi sana na ana uroho wa madaraka!!!
You are missing the point somewhere, anachosema Maige ni kupewa adhabu asiyostahili, usikimbilie kumhukumu kuhusu uwaziri tu, try to think twice
 
Alikuwa wapi wakati huo? si hapo hapo wizarani? tena ni naibu waziri! This is too low if it is from him.
 
Sasa kwa nini alipokuwa waziri hakuyasema hayo amesubiri amepigwa chini ndio anaongea sisi wananchi tutaona hiyo ni chuki binafsi kapewa madaraka kashindwa kuyatumi ni bora akae kimya tuu.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom