Mahusiano ya Kimapenzi sasa hivi ni 'full Comedy'

Ndo maana siku hizi sina mapenzi ya dhati...achana naye tafuta mwingine
 
Mapenzi sinema, kama unaweza mfate ukajionee kwa macho!!
Usidanganyike kumfuata, utaenda kufa bure! unacheza na wanawake wewe? Ilishatokea mabibo hostel mtu kapigiwa kelele za mwizi kisa kamfumania mchumba wake na mwanaume mwinginen chumbani. Huyu bwana alipofika chumbani alimkuta mdada yupo na mwanaume mwingine, yule dada kwa kuona aibu akajifanya hamfahamu yule mwanaume wa mtaani. Yule jamaa akajaribu kulazimisha na kwa kutaja jina la yule dada. Ili kuficha aibu ya kugonganisha magari yule dada akaamua kupiga kelele za mwizi dhidi ya yule mwanaume wa mtaani. Sina uhakika kama yule mwanaume alipona maana kipigo alichokula hakikuwa cha kawaida. Mwanamke roho ya ubinadamu huwa anaiazima tu, wenye nayo wakiichukua, anaweza kukukula nyama huku unaona.
 
Si kasha kwambia yupo bize na maandalizi ya mitihani??

MWACHE MWENZIO ASOME
Kuna watu wengine wanapenda sana ku argue about the silliest of things whereas others argue about things that are important to them...Yani huyo jamaa anashangaza sana ameisha ambiwa na mchumba wake yuko kwenye mitihan...Amesahau kama mtu anapokuwa kwenye mtihani ana focus kwenye masomo tu.

Yani we unataka tu muwe mnaongelea mapenzi tu masaa 24, wakati mwenzako anataka kusoma.
 
Siku hizi mapenzi yamekuwa maigizo ukijifanya unampenda demu atakuumiza tu sex ndio imepewa kipaumbele. Mabinti wa chuo sio kabisa wengi wao ni vicheche wanawezana wao kwa wao. Huyo raia achana nae atakupotezea time mzazi

Dah! Haya maneno yanatoka kwa great thinker? Hao mabinti wa chuo ni watu wanaoishi miongoni mwetu, wengine ni wanafamilia zetu, na sie pia tumepita huko. Kusema mabinti wa chuo ni vicheche ni kuikosea jamii heshima. Watu kuachana ni kawaida, labda kweli yuko busy, au kweli kampata anayemfaa kwa future, yote yawezekana.

Kinachofaa hapo, mtokelezee gheto kwake, si mpenzio bwana? Ukajue mbivu na mbichi huko. Ndipo utajua ni uamuzi gani uufanye.

Watu wasikurushe roho eti mabinti wa chuo vicheche, hakuna koz ya aina hiyo vyuoni.
 
solution kuwa na mademu watatu kama wanavyotufanyia sisi.mmoja unaitwa atm wa pili vocha watatu wakutoka naye out.mi mwenzio ninao watatu kwa hiyo akimwaga mboga mi namwaga ugali kwisha
 
Nimesoma vyuo zaidi ya kimoja, nimeona wanawake wanavyobehave na nimesikia kwa rafiki zangu wa vyuo mbalimbali, kusema ukweli, anza kubadilisha mawazo, utakuja kuletewa kadi ya kuchangia harusi yake af utashindwa kujua cha kufanya. Wanawake wanaopenda huhitaji kuhangaika nae, akiona upo kimywa one hr, anakutafuta, ss huo anakuta mic kol na bado hahangaiki!
 
Sinaham na vibinti dawa ni kuwa navyo vingi kisipo pokea sim kimoja unakipigia kingine,. Mi kunakimoja kishanitesa sana asante mungu nimekisahau,.. Hela yako ndo mapenzi yako
 
Mi ndo maana nimeamua kutafta zangu hela tu, habari za mademu nimeweka pending kwanza. Na nikizipata ntawamega kwa hasira maana ndo wanachotaka siku hz
 
Sinaham na vibinti dawa ni kuwa navyo vingi kisipo pokea sim kimoja unakipigia kingine,. Mi kunakimoja kishanitesa sana asante mungu nimekisahau,.. Hela yako ndo mapenzi yako

Kitendo cha kukumbuka kuwa kalikutesa tayari ushakakumbuka,,,mabinti wanaangalia maslahi ndugu.
 
huwezi kununua furaha ya milele kwa pesa.chuo kinabana muulize ni muda gani yupo free ili uwe unampigia.sa ingine boys mnakeraga nyie aah.
 
Hii kitu imenitokea live, demu wng anayesoma UDSM mwaka wa mwisho, na tukiwa tumepanga mikakati mingi ya maisha ghafla akawa hapokei simu. Mwanzo nilidhani simu yake kaiacha mbali hasa ukizingatia mazingira ya kupanga nje ya hostels za vyuo husika, nikahisi kuwa huenda kaiacha simu room. Hivyo nikasitisha kwanza zoezi la kupiga simu, kwa lengo la kumpigia usiku, nikiamini kuwa muda huo pilika pilika zitakuwa zimeisha. Na kama atakuwa aliitelekeza simu yake, muda huo lazima atakuwa nayo, pamoja na imani yangu kuwa kuziona tu missed calls angepiga tu. Ajabu ni kwamba hakupiga, na nilipompigia bado hakupokea. Nikamtumia ujumbe bado haukujibiwa. Siku ya tatu alinitumia meseji, baada ya mimi kupiga sana na kumtumia ujumbe kuwa 'yupo bize' na maandalizi ya mitihani! Toka hapo mawasiliano yamekatika, hakuna simu wala meseji. Hivi naona ni viroja. Hivi waungwana ninyi mmesoma vyuoni wengi wenu! Katika hali ya kawaida mchumba wako au mpenzi wako akikupigia simu unaweza kubehave namna hiyo hata kama upo bize? Je, ni komedy gani hiyo ninayochezewa wanajukwaa?
hooooooooo solemba
ni bora ungeniambia ukweli solemba,kuliko kunidanganya hooo
 
Kila jambo ni mabadiliko ulimwengu wa sasa! Hakuna uhakika wa leo sikwambii kesho. Halafu kama ulipitia kitaasisi cha elimu lazima ushakuwa mwerevu na hao wanapokuwa vyuoni. Heshima yao hukaa sawa pale wanaporudi mitaani na kukuta kuwa elimu si kila kitu.

Achana nae huyo huku ukijiahidi kuwa hana nafasi kwako pale atakapopata funzo!
 
Back
Top Bottom