Mahusiano: Usafi hustawisha mapenzi!

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,956
22,144
Usafi ni tabia si uwezo kifedha!Hata kama mwonekano wako wa nje si kila kitu bado ni kitu muhimu sana katika mahusiano na mwenzi wako.

Binadamu hunagalia kwa nje na Mungu huangalia moyo (1Samweli 16:7) hii ina maana kwamba mume au mke wako anaangalia nje na si moyo.

Wanawake wengi hujisahau baada ya kuolewa na kuwa na wedding certificate mkononi na wengine akishazaa inakuwa rough hadi inashangaza.

Hivyo si vizuri kutumia wedding certificta au kwamba nimeshaolewa kuwa excuse ili u-relax na kupunguza standard za mwonekano wako.

Unashangaa kwa mume wako kutovutiwa na wewe, au unashangaa mume wako anapokula jiwe kukutambulisha kwa rafiki zake, au unataka anapokutambulisha kwa rafiki zako aanze kibarua cha kujilezea kuwaomba msamaha kwa jinsi ulivyo rough.

Wewe ni mwanaume kabla ya kuoa na muda kidogo baada ya kuoa ulikuwa unanyoa ndevu vizuri kabisa sasa imekuwa ngumu kunyoa as is umeanzisha timu ya bush stars.

Mke umekuwa nyumbani muda wote siku nzima, mume anakuja kutoka kazini jioni anakutana na mwanamke rough na amejiisahau then unalalamika hupati busu na mume amekuwa siyo romantic and gentle?

Fikiria kwa makini na jiulize hivi ulivyo leo baada ya kuolewa ni sawa na ilivyokuwa wakati wa uchumba au umepunguza standard zako na umeanza kujisahau.

Mwanaume huvutiwa kwa kuona hivyo mwanamke anayejua mume wake anahitaji kitu gani hawezi kuzembea kwenye hilo eneo.

Maintain your attractiveness to your partner!
 
Buji jamani kwann untufanyia hivi?beauty lies in the eye of the .............................,unajuaje kama jamaa yake ndo kapenda hivyo alivyo?labda huwa wanacheza kidali po wenzio?wivu huo Buji lol
 
Chochote unachokiandika na kukiweka apa kina reflect your mindset
sijakuelewa hapo...una maana hii thread ibaki hapa ilipo? I thnk Mods waipeleke kwenye jukwaa lake, Jukwaa la wakubwa na siyo hapa, otherwise maadili yatakuwa yanavunjwa...
 
vitu vingine haviihitaji jando wala unyago.
ufahamu kidogo tu utakusaidia, ndio maana wahenga walisema heri ukose mali upate akili.
 
Amini usiamini umaridadi huwafurahisha sana wadada na kufanya mapenzi yasitawi.

Ni vema kua na nguo nyingi za ndani yaani,pants na singlets pamoja na socks safi.

Ni vema sana ukawa pia unapendelea kuvaa whites kwani ni wazi hudhirisha jinsi gani ulivyo maridadi.

Lakini si mavazi pekee yake bali na uondoaji wa nywele za siri mara kwa mara.

Wadada wengi huvutiwa na wanaume wa tabia hiyo.Nawakilisha mawazo.
 
mnh ngoja wenyewe waje,utawasikia uwanaume ni kunukia kibeberu beberu lol
 
na mdada ukiona wako ana msitu wa kongo msaidie kumfyeka, siku nyingine harudii.

Kweli tupu usafi unahu!
 
kazi ipo huwa hatukosi la kusema akiwa sop sop sana nayo utasikia huyo nae kama mwanamke
 
haswaaaaaaaaaaaaa...
Umenena,
umesema,umezungumza,
umeandika
yaaaani ukweli mtupu hapo nakupa 100/100
sio unapishana na mwanaume kwapa inatema hadi kichefuchefu,
wengine akivua viatu soksi chafu zinatoa harufu hadi mtu unapata mafua
Chupi /boksa inanuka uvundo hadi akiingia ofisini unausikia,
kwenye daladala baadhi wakisimama tooooba kwapa zina nywele ndefu kama anataka kusokota rasta halafu za njanooooooooooooooooooooooo....

Usafi unahamasisha mapenzi, wengine watakuja na hoja ooooh mke hanisafishi, kama mwenyewe hujitunzi mkeo atakutunzaje loh
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom