Mahubiri ya leo: Mzee Sitta na Kisa cha nabii mzee

Historia inaoenyesha mara nyingi unabii huwa unapuuzwa unapotolewa, lakini unapokamilika huja na majuto makuu
 
Unacheka nini kama sio kupoteza muda watu. Tumia muda huu kujifunza Katiba Inayopendekezwa kwa maana kusoma sina hakika kama unajua kwani ni mtu wa kucheka tu!
Hakika hakuna neno lililodondoka katika unabii huu
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Unabii huu ulitimia kama ilivyoandikwa, ahlikupunguzwa wala kuongezwa neno katika unabii huu. BAK MANI zumbemkuu tpaul assadsyria3 Chakaza laki si pesa. Mod 1

Sasa kuna ule unabii wa uliotolewa kwa njia ya Ndoto......Nani anaukumbuka??
Magamba waliambiwa tangu zamani kwamba nchi hii wanaiuza kama njugu wakakaidi ndio wanakuja kukumbuka shuka leo asubuhi wakati usiku umeikwisha. Shame on all gambaz!
 
Kasome theolojia kisha uanze kuhubiri kama akina mzee wa upako huku hayo hayapo! Tueleze historia za kiutawala tutakusikiliza na kukupongeza. By the way SItta ni shujaa!
Pamoja na kwamba sikusoma theolojia lakini nasikitika kusema kuwa yalitimia
 
Nimependa ulivyoitoa habari hii, Je yule nabii hakupona kwa kutozingatia yale aliyoamriwa na Mungu lakini kwa nini wewe umetoa mwanya wa Sita kupona kwenye maandishi yako ya herufi kubwa. Je kwa nini na yeye asiraruliwe na Simba kama ilivyokuwa kwa nabii??????????
Ndivyo ilivyotokea kadiri ya mapenzi yako
 
Kisa kizima kinapatikana hapa 1 Wafalme 13:1-34

Kwa ufupi sana, Mfalme Yeroboamu alimtenda MUNGU dhambi, na dhambi hii ilipozidi kuwa kubwa MUNGU akamwinua Nabii MWINGINE ambaye alikwenda hadi kwa Yeroboamu na akatoa Unabii wake kama alivyotumwa, LAKINI aliamriwa kuwa asije akanywa wala kula kitu chochote katika nchi hii maana nchi ilikua najisi kwa kumtenda MUNGU dhambi. Baada ya kutoa unabii wake katika nchi ya Betheli akawa anaondoka kwenye nchi ile ili kuerejea kwake. Nabii mmoja Mzee wa Betheli aliposikia habari zile kwa watoto wake akamfuata hadi alipokutana naye njiani huko na kumsihi yule nabii arudi nyumbani kwake pamoja naye.

Manabii wote wawili walirejea nyumbani na kula chakula pamoja na mara baada ya kula chakula kile ndipo Roho wa Bwana alimpojia na kumkumbusha neno lile aliloambiwa, USILE wala KUNYWA. Adhabu yake kwa kutokutii neno hili ilikua ni kutokuzikwa kwa heshima yaani hatalazwa mahali walipolazwa ndugu zake, na unabii huu ulitimia kwani alishambuliwa na Simba na kuuwawa lakini Punda hakuguswa na Simba huyu.

Sasa, Mzee Siita alionekana kama Nabii, alietumwa akaiokoe Tanzania kwa kusaidia upatikanaji wa Katiba Mpya, katiba ambayo ingesaidia sana kuwatoa watanzania kwenye umaskini uliokithiri, kuonea na kuibiwa mali zao. Hakika Sitta alisimama kwenye nafasi yake LAKINI hakutakiwa kamwe kujiunga tena na kundi hili la Walafi, wenye kula na kuendekeza anasa huku mamia ya watanzania wakifa njaa na magonjwa.

Maskini, Mzee Sitta alianza vyema na kwamba MUNGU alilenga kumwinua zaidi na zaidi lakini amesahau sharti lile la kujipambanua na Walafi wale, wenye Njaa na damu za watu, akarudi, akarejea na amekaaa amekula nao tena chakula cha Unajisi, hivyo amelinajisi neno lile lililowekwa ndani yake, lile alilotumwa alihubiri limemshinda. MUNGU asema hivi, ile ndoto yake ya kuwa mgombea Urais haipo tena, imeondoshwa na kwamba Jamii yake iliyomtia unajisi huu itamtenga very soon. Atakuwa na mwisho mbaya kuliko mwanzo mwema.

Lakini, analo neno la mwisho lililobaki mkononi mwake, KUMBUKA NI WAPI ULIPOANGUKA UKATUBU, NA USIPOTUBU TAZAMA NAKUJA UPESI NAMI NITAPAONDOA MAHALI PAKO PASIWEPO KAMWE.
DAH, watabiri wa kitanzania kiboko,kweli mzee hakufika nchi ya ahadi akafia ugenini du!
 
Back
Top Bottom