Mahubiri ya leo: Mzee Sitta na Kisa cha nabii mzee

Elli

Platinum Member
Mar 17, 2008
55,499
86,035
Kisa kizima kinapatikana hapa 1 Wafalme 13:1-34

Kwa ufupi sana, Mfalme Yeroboamu alimtenda MUNGU dhambi, na dhambi hii ilipozidi kuwa kubwa MUNGU akamwinua Nabii MWINGINE ambaye alikwenda hadi kwa Yeroboamu na akatoa Unabii wake kama alivyotumwa, LAKINI aliamriwa kuwa asije akanywa wala kula kitu chochote katika nchi hii maana nchi ilikua najisi kwa kumtenda MUNGU dhambi. Baada ya kutoa unabii wake katika nchi ya Betheli akawa anaondoka kwenye nchi ile ili kuerejea kwake. Nabii mmoja Mzee wa Betheli aliposikia habari zile kwa watoto wake akamfuata hadi alipokutana naye njiani huko na kumsihi yule nabii arudi nyumbani kwake pamoja naye.

Manabii wote wawili walirejea nyumbani na kula chakula pamoja na mara baada ya kula chakula kile ndipo Roho wa Bwana alimpojia na kumkumbusha neno lile aliloambiwa, USILE wala KUNYWA. Adhabu yake kwa kutokutii neno hili ilikua ni kutokuzikwa kwa heshima yaani hatalazwa mahali walipolazwa ndugu zake, na unabii huu ulitimia kwani alishambuliwa na Simba na kuuwawa lakini Punda hakuguswa na Simba huyu.

Sasa, Mzee Siita alionekana kama Nabii, alietumwa akaiokoe Tanzania kwa kusaidia upatikanaji wa Katiba Mpya, katiba ambayo ingesaidia sana kuwatoa watanzania kwenye umaskini uliokithiri, kuonea na kuibiwa mali zao. Hakika Sitta alisimama kwenye nafasi yake LAKINI hakutakiwa kamwe kujiunga tena na kundi hili la Walafi, wenye kula na kuendekeza anasa huku mamia ya watanzania wakifa njaa na magonjwa.

Maskini, Mzee Sitta alianza vyema na kwamba MUNGU alilenga kumwinua zaidi na zaidi lakini amesahau sharti lile la kujipambanua na Walafi wale, wenye Njaa na damu za watu, akarudi, akarejea na amekaaa amekula nao tena chakula cha Unajisi, hivyo amelinajisi neno lile lililowekwa ndani yake, lile alilotumwa alihubiri limemshinda. MUNGU asema hivi, ile ndoto yake ya kuwa mgombea Urais haipo tena, imeondoshwa na kwamba Jamii yake iliyomtia unajisi huu itamtenga very soon. Atakuwa na mwisho mbaya kuliko mwanzo mwema.

Lakini, analo neno la mwisho lililobaki mkononi mwake, KUMBUKA NI WAPI ULIPOANGUKA UKATUBU, NA USIPOTUBU TAZAMA NAKUJA UPESI NAMI NITAPAONDOA MAHALI PAKO PASIWEPO KAMWE.
 
Kasome theolojia kisha uanze kuhubiri kama akina mzee wa upako huku hayo hayapo! Tueleze historia za kiutawala tutakusikiliza na kukupongeza. By the way SItta ni shujaa!
 
Huu ni uvivu wa kufikiri.shujaa kwa kukusanya maoni upya?shujaa kwa kubadili kanuni? shujaa kwa lipi kutupilia kubali uwajibishwaji wa viongozi wanapokengeuka? Au shujaa kwa kukataa ukomo wa ubunge?
 
hahahha hawezi kukujibu
 
Kasome theolojia kisha uanze kuhubiri kama akina mzee wa upako huku hayo hayapo! Tueleze historia za kiutawala tutakusikiliza na kukupongeza. By the way SItta ni shujaa!

Uwe unawaza kidogo,TUME ILIFANYA KAZI GANI? JE KAZI YA BUNGE MAALUMU LA KATIBA NI NINI KWA SHERIA YA MABADILIKO YA KATIBA? JE KINACHOFANYIKA SHERIA YA MABADILIKO YA KATIBA INASEMAJE. ni maswali rahisi sana kwa kusema lakini kimantiki ni bora upitie kwenye hivyo vitini vyenye huo muongozo ndio ujibu usikurupuke.USHAURI WA BURE-sio kila kinachoandikwa ni lazima ujibu
 
Kisa kizima kinapatikana hapa 1 Wafalme 13:1-34

Kwa ufupi sana, Mfalme Yeroboamu alimtenda MUNGU dhambi, na dhambi hii ilipozidi kuwa kubwa MUNGU akamwinua Nabii MWINGINE ambaye alikwenda hadi kwa Yeroboamu na akatoa Unabii wake kama alivyotumwa, LAKINI aliamriwa kuwa asije akanywa wala kula kitu chochote katika nchi hii maana nchi ilikua najisi kwa kumtenda MUNGU dhambi. Baada ya kutoa unabii wake katika nchi ya Betheli akawa anaondoka kwenye nchi ile ili kuerejea kwake. Nabii mmoja Mzee wa Betheli aliposikia habari zile kwa watoto wake akamfuata hadi alipokutana naye njiani huko na kumsihi yule nabii arudi nyumbani kwake pamoja naye.

Manabii wote wawili walirejea nyumbani na kula chakula pamoja na mara baada ya kula chakula kile ndipo Roho wa Bwana alimpojia na kumkumbusha neno lile aliloambiwa, USILE wala KUNYWA. Adhabu yake kwa kutokutii neno hili ilikua ni kutokuzikwa kwa heshima yaani hatalazwa mahali walipolazwa ndugu zake, na unabii huu ulitimia kwani alishambuliwa na Simba na kuuwawa lakini Punda hakuguswa na Simba huyu.

Sasa, Mzee Siita alionekana kama Nabii, alietumwa akaiokoe Tanzania kwa kusaidia upatikanaji wa Katiba Mpya, katiba ambayo ingesaidia sana kuwatoa watanzania kwenye umaskini uliokithiri, kuonea na kuibiwa mali zao. Hakika Sitta alisimama kwenye nafasi yake LAKINI hakutakiwa kamwe kujiunga tena na kundi hili la Walafi, wenye kula na kuendekeza anasa huku mamia ya watanzania wakifa njaa na magonjwa.

Maskini, Mzee Sitta alianza vyema na kwamba MUNGU alilenga kumwinua zaidi na zaidi lakini amesahau sharti lile la kujipambanua na Walafi wale, wenye Njaa na damu za watu, akarudi, akarejea na amekaaa amekula nao tena chakula cha Unajisi, hivyo amelinajisi neno lile lililowekwa ndani yake, lile alilotumwa alihubiri limemshinda. MUNGU asema hivi, ile ndoto yake ya kuwa mgombea Urais haipo tena, imeondoshwa na kwamba Jamii yake iliyomtia unajisi huu itamtenga very soon. Atakuwa na mwisho mbaya kuliko mwanzo mwema.

Lakini, analo neno la mwisho lililobaki mkononi mwake, KUMBUKA NI WAPI ULIPOANGUKA UKATUBU, NA USIPOTUBU TAZAMA NAKUJA UPESI NAMI NITAPAONDOA MAHALI PAKO PASIWEPO KAMWE.
Excellent story. Ndo uzuri wa biblia kilichoandikwa lazima kipo au kitokee kwa mwanadamu
 
vitu vingi vinavyotekea vilishatabiriwa kwenye bible sema interpretation ndio hutushinda otherwise tungekuwa tunachukua tahadhali mapema
 
Kasome theolojia kisha uanze kuhubiri kama akina mzee wa upako huku hayo hayapo! Tueleze historia za kiutawala tutakusikiliza na kukupongeza. By the way SItta ni shujaa!

ushujaa gani kama wewe siyo moja wa wajinga ai una masilahi ktk hayo yanayolazimishwa tumis akili yako.
 
Hua hata mimi napata shida sana kuwaelewa baadhi ya watu humu ndani.......
 
Amen Amen, Mzee Sitta tafadhali sana

Nimependa ulivyoitoa habari hii, Je yule nabii hakupona kwa kutozingatia yale aliyoamriwa na Mungu lakini kwa nini wewe umetoa mwanya wa Sita kupona kwenye maandishi yako ya herufi kubwa. Je kwa nini na yeye asiraruliwe na Simba kama ilivyokuwa kwa nabii??????????
 
Amen, ndio hali halisi kuwa kwa maisha ya sasa tunakombolewa kwa NEEMA tu na kwamba MUNGU hutupatia escape zone ili tuweze kujirekebisha. Mimi nimeona kuwa Mzee Six anayo nafasi bado, hajachelewa maana ameambiwa!
 
Nakubalina na wewe kuwa ni wakati wa NEEMA ila pia kuna maandiko yanayosema, yule aliyekionja kipawa kizuri cha mbingu na mara baada ya hapo akaanguka haiwezekani kufanywa upi hata akitubu kwani amemrudisha mwana wa Mungu msalabani mara ya pili.
 
aMEN aMEN
Nakubalina na wewe kuwa ni wakati wa NEEMA ila pia kuna maandiko yanayosema, yule aliyekionja kipawa kizuri cha mbingu na mara baada ya hapo akaanguka haiwezekani kufanywa upi hata akitubu kwani amemrudisha mwana wa Mungu msalabani mara ya pili.
 
Nimependa ulivyoitoa habari hii, Je yule nabii hakupona kwa kutozingatia yale aliyoamriwa na Mungu lakini kwa nini wewe umetoa mwanya wa Sita kupona kwenye maandishi yako ya herufi kubwa. Je kwa nini na yeye asiraruliwe na Simba kama ilivyokuwa kwa nabii??????????
Unabii, huonya na kutoa nafasi ya kutubu. Akiwa na kiburi, moyo wake utafanywa kuwa mgumu.
 
Back
Top Bottom