Mahoteli ya Paradise na Oceanic Bay zatekekea kwa moto!

Ndugu zangu,
Majanga yanapotupata ndipo tunakumbuka mengi hasa katika kujikinga ili kuzuia yasitokee.Pia kujitafakari kuona je yanapotokea tuko tayari vipi kuyakabili?

Tumeshapata mafundisho lukuki kutokana na majanga ya moto hasa katika majumba ya makazi, maofisi na hata mahoteli.Hili tukio la sasa la kuungua kwa hoteli za Paradise, Oceanic Bay na Malaika limenikumbusha si zamani sana hotel ya Sea cliff nayo iliungua.Kuna kitu kimoja in common katika sehemu zote hizi.Uezekaji wa makuti.Damu inanisisimka SASA HIVI maana nimekumbuka kuwa pale Uwanja wa ndege Julius Nyerere International Airport kuna harakati za kujenga vibanda vya makuti uwanjani na sijui kama waliotoa idhini ujenzi huo wanafanya hivyo "kudumisha mila na tamaduni za mababu zetu" kuezeka kwa nyasi ili watalii wanaposhuka pale waanze kufurahia utalii au ni kutokujali!

Hivi janga la moto likitokea uwanjani pale, tutamlaumu nani na tumeshindwa kujifunza? Sijui wadau hili mnalionaje? Kama kuna wanachama hapa kutoka kwenye mamlaka husika chondechonde simamisheni huu ujenzi wa vibanda vya makuti pale eapoti!Licha ya kuwa ni hatari endapo moto utatokea, pia ni chukizo machoni pa wale wanaopenda umaridadi!
 
Habari toka bagamoyo zinasema hoteli ya paradise iliyopo bagamoyo inateketea kwa moto.
Kwa mujibu wa kamanda wa polisi mkoa wa pwani, afande absalom mwakyoma, juhidi zinafanyika kuuzima moto huo kwa kutumia wananchi kwa sasa. Ila amesema magari ya faya toka dar yako njiani kwenda huko.
Hoteli za jirani, amesema kamanda mwakyoma, nazo ziko hatarini kuungua moto kwani upepo ni mkali na moto ni mkubwa. Hoteli nyingi za bagamoyo zimeezekwa makuti.
Habari zaidi kufuata baadaye...

Ungetumia muda kidogo kusoma JF ungeona hii habari ipo wala usingali poteza muda wako kupost....Mod tunaomba mtuvulie unganisheni hii kitu!
 
Tunahitaji elimu kutolewa zaidi juu ya majanga ya moto kwa wamiliki na wafanyakazi wa hotel ili tahadhari zichukuliwe zaidi.
 
daaa jamanii hasara kubwa sana kwa mmiliki na piaa zaidi na kubwa zaidii ajira za ndugu zetu pale....zimekatishwa bila kutegemea poleni sana wamiliki na wafanyakazi....tunawaombea....sana mrudie wote kazini .............
 
Gari la zimamoto linatoka Dar kwenda Bagamoyo je lina maji ya kuzimia huo moto ama watalazimika kurudi tena Dar kuja kuchukua maji?.

Kaka, maji ya nini ?

Kwani hatuna vichwa vya kutingisha kwa masikitiko?
Au hatuna midomo ya kupiga miluzi ya masikitiko?

Hi ndo bongo bana kuba!
 
daaa jamanii hasara kubwa sana kwa mmiliki na piaa zaidi na kubwa zaidii ajira za ndugu zetu pale....zimekatishwa bila kutegemea poleni sana wamiliki na wafanyakazi....tunawaombea....sana mrudie wote kazini .............
Hilo ndo linaniuma sana, ajira kwa ndugu zetu, ni likizo isiyo na muda maalum. Kwa wamiliki ni fursa ya kujipatia msamaha wa kodi (mahesabu yameungua) na pia malipo ya bima. Ila tujifunze kupambana na majanga kama haya, makuti katika eneo lenye upepo mkali kama pwani ni kichocheo. Hivi hawakujifunza kwa yaliyotokea sea cliff?
 
Kuna haja huwa na sera ova paa za makuti mahoteli makubwa Tz!

Ikiwezekana basi zipigwe marufuku!
 
Last edited:
Nakumbuka Makamba alishaonya wawekezaji kujenga mabanda kwa makuti. At the same time kwa utajiri wa hawa wawekezaji wa haya mahotel nilitegemea karibu kuwe na tahadhari ya magari ya Zima moto. Tatizo watu tunataka super profit na kuogopa gharama. Wangeingia contract na kampuni kama Night Support au KK then wawe na camp hapo kwao na wanawalipa, rentention fees. Wangekuwepo damage isingekuwa kubwa kiasi hicho. Kumbuka na mitungi ya gas itakuwa imelipika na kuchochea moto zaid, ukiachilia mbali umeme. Yaani waafrica wengi hatutaki kuweka tahadhari katika mali zetu, eti tunaogopa gharama. Sasa si afadhali ingeungua sehemu kidogo ikakarabatiwa kuliko kuungua yote, na mbaya zaidi kuteketeza hata mahote ya karibu??? I can imagine how difficult compensation will be??? Hii iwe ni funzo kwa wawekezaji wa ndani na nje.
 
Ukweli ni kwamba mpaka sasa hivi moto bado unaendelea kuwaka, hakuna gari lolote linalozima moto. Unajua Tanzania inaendeshwa kisiasa sana, kuna kilomita nyingi sana kutoka Dar mpaka Bagamoyo.
 
Hilo ndo linaniuma sana, ajira kwa ndugu zetu, ni likizo isiyo na muda maalum. Kwa wamiliki ni fursa ya kujipatia msamaha wa kodi (mahesabu yameungua) na pia malipo ya bima. Ila tujifunze kupambana na majanga kama haya, makuti katika eneo lenye upepo mkali kama pwani ni kichocheo. Hivi hawakujifunza kwa yaliyotokea sea cliff?
...Wameshindwa hata kufanya mpango wa kuwa na gari la zima moto mpaka wasubiri yatoke Dar?? Wanakumbuka shuka wakati jua limechomoza. Lakini hawa wasomali huenda wamezungusha kwenye masuala ya bima hapo???
 
Ukweli ni kwamba mpaka sasa hivi moto bado unaendelea kuwaka, hakuna gari lolote linalozima moto. Unajua Tanzania inaendeshwa kisiasa sana, kuna kilomita nyingi sana kutoka Dar mpaka Bagamoyo.

acha utani ndugu, ina maana since ahsubihi hamna gari la zimamoto lililofika?
napata harufu ya hujuma hapo....
well tuangalie yatakayojiri baada ya hapo
 
Niliwahi sikia kwamba sheria za mashirika ya BIMA hawalipi nyumba zilizoezekwa kwa makuti au sensitive fire supporting materials. Kama ni hivyo hawa ndugu si imekula kwao? Hebu kwa wale wataalamu wa maeneo ya BIMA mtujuvye habari hii tafadhali!
 
HOTELI ya Paradise Holiday resort na Oceanic Bay Hotel zilizoko wilayani Bagamoyo Mkoa wa Pwani zimeteketea kwa moto.

Moto huo ulioteketeza hoteli zote mbili kwa muda saa moja, ulianzia jikoni katika hoteli ya Paradise na kushika mtungi wa gesi, saa nne asubuhi ambapo ulisambaa kwa kasi kutokana na upepo mkali na hoteli hizo ziliezekwa kwa makuti.

Mji wa Bagamoyo hauna kikosi wala vifaa vya kuzimia moto. Magari ya zima moto yaliitwa kutoka DSM lakini yalipofika Bagamoyo yalikuta majivu ndiyo yaliyobakia.
 
Kulikuwa na sheria ndogo jijini dar (enzi za Makamba) kupiga marufuku uezekaji wa nyasi katika nyumba za starehe... Sijui kama ilivuka mipaka hadi Bagamoyo

Sheria hii haikuzihusu nyumba za kawaida za wanajamii...

nadhani Arusha tu ndio waliweza ku-enforce, dar ilishindikana (na ilikuwa by-law tu)
 
maalim
simu mbona hupekei?

halafu wewe sio mtu wa kutoa sweeping statements kama hizi...kama wangekuwa hawalipi BIMA HILO NI WAO NA SHIRIKA LA BIMA LAKINI SASA HIVI HATUNA DATA..

salam zao

wala sikuitoa kama firm statement mkuu, ni mawazo tu yalikuwa yanapita mukichwa nikaamua ku-think aloud
 
Back
Top Bottom