Mahoteli ya Paradise na Oceanic Bay zatekekea kwa moto!

Tusker Bariiiidi

JF-Expert Member
Jul 3, 2007
5,520
2,091
Habari Wana JF taarifa nilizozipata sasa hivi ni kwamba Hotel ya Oceanic Bay Bagamoyo inaungua moto muda huu...
Hotel hii inamilikiwa na Familia moja yenye asili ya Somalia...
Nitaendelea kuwajuza...
Ahsanteni
 
Last edited by a moderator:
sijui kama bagamoyo kuna gari la zima moto, naikumbuka sana hii hotel niliwahi kuwa na workshop hapo 2007
 
sijui kama bagamoyo kuna gari la zima moto, naikumbuka sana hii hotel niliwahi kuwa na workshop hapo 2007

Bagamoyo HAKUNA Gari la Zima Moto - Linasubiriwa toka Dar es Salaam!
 
Last edited:
Habari nilizozipata sasa hivi ni kuwa ni Hotel zote 2 yaani Paradise na Oceanic zimekamata moto... Mji wa Bagamoyo umegubikwa na giza kubwa lilitokana na moshi mzito uliotokana na ajali... Wananchi wa Bagamoyo wanasaidia kuzima kwa zana duni kama Ndoo za maji na Mchanga gari la zimamoto linatokea Dar kuelekea huko...

Tuombe Mungu kusiwe na maafa yoyote... Na hivi wanachi ndo wamelekea kuzima moto na kuna Ma-Tank ya Gas pale...
 
Habari nilizozipata sasa hivi ni kuwa ni Hotel zote 2 yaani Paradise na Oceanic zimekamata moto... Mji wa Bagamoyo umegubikwa na giza kubwa lilitokana na moshi mzito uliotokana na ajali... Wananchi wa Bagamoyo wanasaidia kuzima kwa zana duni kama Ndoo za maji na Mchanga gari la zimamoto linatokea Dar kuelekea huko...

Hotel ya paradise imekwisha teketea kwa moto, Oceanic imeanza, na Malaika ndo imeanza, hizo zote zimefatana, na moto wenyewe umeanzia Paradise Hotel. Hata hivyo chanzo bado hakijajulikana
 
Hili ni janga, lakini isije ikawa ni hujuma ya hawa wasomali kutaka kukwepa kulipa mapato na kudai bima
 
Gari la zimamoto linatoka Dar kwenda Bagamoyo je lina maji ya kuzimia huo moto ama watalazimika kurudi tena Dar kuja kuchukua maji?.
 
michuzi blog wamesema paradise hotel,so lipi ni sahii paradise or oceani hotel kwani zote zimepana i mean zina share fence moja
 
Ndugu zimeungua Paradise, Oceanic, Malaika na sasa Livingstone iko hatarini kwani moto umeanza kuelekea huko. Haiwezekani kuwa hujuma ingeungua moja nimeunga mkono nwa mpitanjia
 
Imeanza Paradise, halafu oceanic ikafuata sasa ndio malaika. Zote tatu zinapakana. Nakumbuka Paradise Mombasa iliwahi kuungua ikaunguza hoteli nyingine 4 za jirani.
 
Livingstone haiwezi kuungua kirahisi hivyo iko mbali usawa wa mita 800 hivi kutoka hizo zilizoungua labda uniambie kuwa lile banda pale Msalabani likishika moto baaas ndo livingstone haitakuwa na ujanja wa kupona.
Poleni sana wabagamoyo kwa ajali hii mbaya, na nitasikitika zaidi endapo nitagundua kuwa FAYA walituma gari moja tu la zimamoto.

Naipenda serikali ya Tz kwa kufanya kazi kutokana na shinikizo naamini kuwa ndo itastuka na kuweka gari la zimamoto pale town.

Nina watani zangu wanaishi kigamboni ambapo two weeks ago niliambia kuna moto uliunguza nyumba eneo jirani na Kivukoni koleji, and gari la faya lilipaswa kusubiri foleni kuingia ktk pantoni (likiwa limechelewa) ili kuwahi kuzima moto... Najiuliza ni lini kule kutakuwa na standby gari la zimamoto? wacha zimamoto tu hata hospitali ya maana hakuna kule.... Sijui yule mbunge wa kigambonino anajukumu gani?? au ndo kudowezea teni pasenti za uuzaji wa ardhi???
kaaaz kweli kweli
 
Ingekuwa Romania,watu wa Bagamoyo wangejikalia pembeni,ndio hao wawekezaji wangejua maana ya raslimali watu.Waswahili wa Bagamoyo kwa hawa wenye ma Hoteli huwa ni kama sijui.......sasa angalau watajua kuwa hata kama wana pesa kiasi gani majirani wa kweli na wa waokoaji wa karibu kwao ni majirani zao-waswahili wa Bagamoyo,na sio hao jamaa wanaokuja kula na kuondoka.Sasa watawathamini vilivyo.
 
confirmed moto umesambaa kwenye hoteli za jirani

na hii credit crunch naona itakuwa ngumu sana kurecorver from this hata kama insurance ikilipa lakini big set back
 
Kulikuwa na sheria ndogo jijini dar (enzi za Makamba) kupiga marufuku uezekaji wa nyasi katika nyumba za starehe... Sijui kama ilivuka mipaka hadi Bagamoyo

Sheria hii haikuzihusu nyumba za kawaida za wanajamii...
 
Hili ni janga, lakini isije ikawa ni hujuma ya hawa wasomali kutaka kukwepa kulipa mapato na kudai bima
maalim
simu mbona hupekei?

halafu wewe sio mtu wa kutoa sweeping statements kama hizi...kama wangekuwa hawalipi BIMA HILO NI WAO NA SHIRIKA LA BIMA LAKINI SASA HIVI HATUNA DATA..

salam zao
 
Back
Top Bottom