Mahoka ! Manji naye aishtaki Kagoda- imebaki Rostamu kuishtaki Dowans !

Mag3

Platinum Member
May 31, 2008
13,064
22,756
Mmiliki wa Kagoda akwama kutokea kortini

Ni katika kesi iliyofunguliwa na Manji


Kesi iliyofunguliwa na mfanyabiashara wa Dar es Salaam, Yusuf Manji dhidi ya kampuni tata ya Kagoda Agriculture Ltd., jana ilitajwa rasmi katika Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam, huku mmiliki wa Kagoda akishindwa kutokea.
Katika kesi hiyo ya madai Na. 16 ya mwaka 2011, Manji kupitia kampuni yake ya Quality Finance Corporation Limited (QFC), ameishtaki Kagoda akidai kuwa mwaka 2008 aliikopesha Sh. 18.7 bilioni ambazo imeshindwa kuzirejesha.
Kupitia kampuni ya mawakili ya Law Associates ya Dar es Salaam, Manji amewasilisha madai makubwa manne, ikiwamo Kagoda kulipa kiasi hicho cha Sh. bilioni 18.7 kama yalivyokuwa katika makubaliano.
Anataka kulipwa pia riba ya asilimia 18 ya kiasi hicho cha fedha kufikia siku ambayo hukumu ya kesi hiyo itatajwa, gharama za kesi na mengine ambayo mahakama itaona yanafaa.
Jaji Ama Munis, anayesikiliza kesi hiyo, aliema kesi hiyo itatajwa tena Aprili 24, mwaka huu na kuagiza walalamikaji kutoa ushirikiano wa kuhakikisha Kagoda wanapatiwa taarifa ya kufika mahakamani.
Kampuni ya Kagoda ndiyo inayotuhumiwa kuchota zaidi ya dola 30.7 milioni kutoka Akanuti ya Madeni ya Nje (Epa), kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT).
Manji ndiye aliyeidhamini Kagoda wakati wa kufungua akaunti katika benki ya CRDB Benki, huku mkataba wa mkopo ukionyesha kuwa uliandaliwa 12 Septemba 2005, siku 17 kabla ya Kagoda kusajiliwa.
Kampuni ya Kagoda ilisajiliwa rasmi kwa Msajili wa Kampuni (Brela), Septemba 29, mwaka 2005.
Manji anadai kuwa ni yeye kupitia kampuni yake ya Quality Finance Limited (QFCL), alikopeshwa fedha hizo ambazo Kagoda inasema zilikuwa ni sehemu ya fedha ambazo serikali ilikuwa inadaiwa na makampuni ya kigeni.
CHANZO: NIPASHE

Twazidi kugeuzwa mazezeta !
 
Tatizo hakuna anayejua mmiliki wa Kagoda nani.. Manji anashtaki hewa tu utadhani zile movies za kichina..
 
Ee Mungu,cc watanzania 2mefanya kosa gani mbele zako,mpaka unashindwa kutuokoa na uovu huu unaotupata,tunatukanwa,tunanyanyasika,tunaibiwa na wageni pamoja na wTzwenzetu.MUNGU TUOKOE NA MIDOMO YAO,WANAOKULA KEKI ULIYOTUPA WOTE BURE..
 
Wahindi a.k.a mafisadi wana mbinu sana isije ni namna ya kupoteza gemu, hebu tutafakari vizuri, mwishowe itasemwa kagoda haipo na wamiliki hawajulikani kupitia mahakama. Hivyo watu watakuwa wamezibwa midomo na mahakama, kwisha!
 
Miye naona huu ni mwanzo mzuri kwa maana ya kwamba sasa tutawajua hao wamiliki wa Kagoda! Manji lazima anawajua hao wamiliki wa Kagoda, maana huwezi kumdhamini mtu usiyemjua hasa linapoingia suala la hela. Siijui sheria vizuri, lakini nadhani mahakama itahitaji mmiliki au mwakilishi wa kampuni, huyo atatusaidia kutupa majibu mazuri ya nani ni Kagoda?
 
Back
Top Bottom