Mahojiano yangu na JamboLeo

Yale maswali yaliulizwa kwake personally,

akijibu ki-ujumla how can he be assessed?

mkuu acheni hizo, huu wivu unawasaidia nini? unapindisha maada kwa makusudi kabisa.

I, I, I..unataka amsemee nani sasa!, kamati ya bunge ilipitisha kwa initiative za nani? bunge ni watu, waacha kila mmoja abebe msalaba wake mwenyewe! unataka awafagilie wabunge wengine wa CCM! siasa bwana

too chep for you, huna ground za kusema hivyo

anazungumza kama kiongozi thats all.

LOL!

Bunge ndilo linapitishwa miswada kwa kupiga kura .... ukitumia We unaonyesha umewiva kisiasa na unaelewa umuhimu wa team work ... hiyo ni misingi ya uongozi ..mimi simwonei wivu ... namshauri ... ningemuonea wivu ningemwacha aendelee na I... I... I... Mimi ... mimi ... zake .. halafu aboe watu wanaoelewa team work ni nini... wewe umewahi kusikia spika au Rais anasema mimi nimefanya hivi... ni sisi au chama auu serikali au bunge limefanya hiki na kile..... hata nyumbani kwako usiseme gari langu hasa kama una mwenza sema .. letu sawa kiongozi? Sio mimi ni principles tu ambazo szimekubalika kwa hiyo usije kunishambulia mimi shambulia principles.. asente...:)
 
Wakuu zangu,

Ebu tukue kiumri na kifira pia.. Hizi habari za Zitto mbona zinawasumbua sana kana kwamba Zitto ni mmoja muhimu na hatari sana.

Kila naposoma ni lawama tu Zittooo Zittooo, imefikia hata watu kusema Kundi la Zitto sijui hivi mara vile.

Lakini tukitazama ukweli watu wanaozungumzwa hapa ni watu wa Zitto tu, sijawahi kusikia maelezo ya kundi lapili hata siku moja toka mdomoni mwa Zitto ama wafuasi wake.

Hata nikichukulia kwamba Zitto na kundi lake wana Uhasama na kina Dr.Slaa, Mnyika, Mdee na wengineo, mbona sijasoma hata siku moja humu JF watu hao wakitupiwa maneno japo kidogo. Kama kweli Zitto angekuwa na uchafu huu nina hakika tungekwisha sikia mengi tu kuhsiana na kundi la pili lakini kila siku ni Zitto na kundi lake huku watyu wamejificha chini ya majina bandia..Na bado Zitto kaheshimu haki zenu. Kisha basi Zitto huja hapa kujiweni na muda mwingi hutumia kujibu matapishi yenu juu yake yeye badala ya kuzungumzia Chadema kama chama.

Ifike wakati tukubali maelezo yake na tutazama vitu vikubwa vinavyotuhusu zaidi ya Zitto..

Jamani inachosha...Ikiwa mmaswali yenyewe anaulizwa kuhusu yeye mlitegemea azungumze kuhusu nani?.. Haya ya sisi (we) mahala ambapo hapahusu!
 
Wakuu zangu,

Ebu tukue kiumri na kifira pia.. Hizi habari za Zitto mbona zinawasumbua sana kana kwamba Zitto ni mmoja muhimu na hatari sana.

Kila naposoma ni lawama tu Zittooo Zittooo, imefikia hata watu kusema Kundi la Zitto sijui hivi mara vile.

Lakini tukitazama ukweli watu wanaozungumzwa hapa ni watu wa Zitto tu, sijawahi kusikia maelezo ya kundi lapili hata siku moja toka mdomoni mwa Zitto ama wafuasi wake.

Hata nikichukulia kwamba Zitto na kundi lake wana Uhasama na kina Dr.Slaa, Mnyika, Mdee na wengineo, mbona sijasoma hata siku moja humu JF watu hao wakitupiwa maneno japo kidogo. Kama kweli Zitto angekuwa na uchafu huu nina hakika tungekwisha sikia mengi tu kuhsiana na kundi la pili lakini kila siku ni Zitto na kundi lake huku watyu wamejificha chini ya majina bandia..Na bado Zitto kaheshimu haki zenu. Kisha basi Zitto huja hapa kujiweni na muda mwingi hutumia kujibu matapishi yenu juu yake yeye badala ya kuzungumzia Chadema kama chama.

Ifike wakati tukubali maelezo yake na tutazama vitu vikubwa vinavyotuhusu zaidi ya Zitto..

Jamani inachosha...Ikiwa mmaswali yenyewe anaulizwa kuhusu yeye mlitegemea azungumze kuhusu nani?.. Haya ya sisi (we) mahala ambapo hapahusu!



Duuh mkubwa ina maana "matapishi' kama unavyoita wewe ya kina Zitto na Omary huwa huyaoni au ulikuwa busy ..:):).
 
Zitto,

..mahusiano yako na hawa viongozi wa CCM yanatisha.

..yaani huna role model hata mmoja ndani ya Chadema?

..hivi kada wa CCM akisema role model wake ni Mzee Mtei, au Dr.Slaa, na kwamba kila siku hushinda huko akifundishwa siasa, unafikiri CCM watafanya nini naye?

..halafu how could you be impressed na kiongozi kama JK? jinsi anavyovumilia wala rushwa umeona ni jambo la maana kweli?

..huu mwenendo wako unaweza kuwa sababu iliyowafanya wazee wakushauri usigombee Uenyekiti wa Chadema.
 
Nini matarajio yako ya baadaye?

Ninatamani kuwa mwalimu wa chuo kikuu, kufundisha, kutafiti na kuandika vitabu. Nitakapoacha siasa, hii ndio kazi ambayo ningependa kufanya. Kufundisha.

Zitto, OK kwa kutomtaja Obama umejitetea lakini ujue sasa you are a political and a public figure! Kila mahojiano utakayotokea tutayapima kwa matarajio ya nafasi watanzania wanayotaka kukupa kama kiongozi! Ni kweli kwamba mahojiano haya umeyajibu kwa ufanisi sana, lakini kuna flops kama jibu la swali hilo hapo juu... jibu lako ni ni somehow selfish (umimi) na shallow niwieradhi ashakum si..., au jibu la kijana aliyemaliza shule sekondari anayetarajia kujijengea career! Hapa ningetarajia kusikia vision yako kwa watanzania, au shauku yako ya kisiasa (political ambition)... jibu kama ningependa kuona Tanzania iliyoneemeka isiyo na ufisadi, iliyo na demokrasia kweli, watoto wetu kwenye shule zenye kutoa elimu inayoweza kumudu zama zetu...nk Kwa mwanasiasa hakuna excuse interview ilikua fupi, every opportunity ni lazima uitumie ipasavyo... Zitto hii ni changamoto!
 
Lukele2009,
Mkuu mambo yote anayozungumza Zitto yanamhusu yeye personal na kama kiongozi wa chama -Yamemkuta, yanamkuta na yatamkuta hazungumzi kwa kudhania. Binafsi sikubaliani naye ktk baadhi ya maamuzi yake lakini sina haki ya kumtukana na kutoaq hukumu juu yake kwa sababu mambo hayo hayakunikuta mimi wala siwezi kujiweka ktk nafasi ambayo sipo.

Kwa hiyo, nimemsoma Zitto nikaelewa vizuri hasira zake na yote aloandika kisha nikapima uzito. na ndipo nilipomkosoa Zitto kwa hatua alizochukua nikiwa nanjia nyingine ambazo angetakiwa kuzifuata kiustaarabu. Lakini wakati huo huo nasoma matusi mengi sana humu toka kwa watu tusiowafahamu, watu ambao nina hakika hawana ustaarabu wowote zaidi ya wao kutazama wa wengine. Kumkosoa Zitto ni moja lakini uwanja uwe huru na wazi kwenu pia maanake Zitto anapoandika madudu yenu mnakuja juu vibaya vibaya. Ni rahisi kwenu kuzungumzia Uhusianao wa Zitto na mama yake, Zitto na Omaryas lakini msitajwe nyie uhusiano wenu. Yaani hapa Zitto amekuwa sinema.

Inachosha sana kuona watu wanauliza maswali nje ya mada hii, soma bandiko lake na kama hukubaliani nalo orodhesha vipengele ambavyo hata sisi tunaweza kuvifuata lakini kuingiza mambo ambayo hayahusiani kabisa na mada hii sidhani kama ni uungwana. Zitto sio perfect human being, na hakuna kiumbe wa namna hiyo, na hawezi kuwa hata kama atafuata ushauri wenu nyote.. Mtang'ong'a vile vile . Kisha zaidi ya yote who is Zitto anyway! mwacheni afanye kazi zake na kama wananchi wa Kigoma hawaridhiki naye watampiga chini, ikiwa Chadema inamwona hana mpnago watamwengua Uongozi kesho..Maadam bado ni kiongozi wa chama na anaendelea kukiuza chama ipaswavyo haya majungu ya uswahili uswahili ndio yanaleta vurugu zaidi.

Waswahili wanasema - Unapo mnyooshea mtu kidole, kumbuka kuna vidole vitatu vinakutazama wewe!
 
Zitto,

..mahusiano yako na hawa viongozi wa CCM yanatisha.

..yaani huna role model hata mmoja ndani ya Chadema?

..hivi kada wa CCM akisema role model wake ni Mzee Mtei, au Dr.Slaa, na kwamba kila siku hushinda huko akifundishwa siasa, unafikiri CCM watafanya nini naye?

..halafu how could you be impressed na kiongozi kama JK? jinsi anavyovumilia wala rushwa umeona ni jambo la maana kweli?

..huu mwenendo wako unaweza kuwa sababu iliyowafanya wazee wakushauri usigombee Uenyekiti wa Chadema.

Mimi nilishaanza countdown ya Zitto kuhamia CCM. The guy hana mapenzi tena na chadema. Haya yote anayoweka hapa ni kujaribu kudanganya waandishi uchwara wa bongo ili waandike kwenye magazeti yao (si unajua tena waandishi wanachukua habari hapa moja kwa moja na kuziweka kwenye magazeti yao!).
 
Kwanza nianze kwa kukupongeza Mheshimiwa sana Zitto kwa mahojiano mazuri . Mimi nilikuwa na swali moja tuu, umesema ya kuwa role model wako ni Mheshimiwa Salim A. Salim ; jee unaweza kushare na wananchi kwamba ni vitu gani haswa ambavyo mwanadiplomasia huyu amekuvutia navyo ? Vile vile, ningependa kujua huyu bwana ameaccomplish nini haswa wakati akiwa OAU? Natanguliza shukrani.
 
Zitto,
Tafadhali fanya kila lililo ndani ya UWEZO wako kama Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Mashirika ya Umma kuyaokoa mashirika haya machache yaliyobaki yasiendelee kutafunwa na ninyi wanasiasa.
Pili, angalia uwezekano wa zile pesa zinazokusanywa pale TCRA, EWURA, SUMATRA na taasisi nyingine za uratibu kama zinaweza kumegwa na kupelekwa kwenye kugharamia huduma za jamii hasa ELIMU na MATIBABU kuliko kuachiwa watu wachache tu kuzitafuna na WANASIASA wetu. Haya ni nje ya hii mada lakini naamini juu ya uwezo wako wa KUTHUBUTU.
 
Mh Zitto, ni doubts nyingi sana kuhusu wewe. Lakini lazima niwe mkweli kuwa nimefurahishwa sana na uamuzi wako wa kuwasomesha vijana wa jimbo lako. Umewawezesha kuliko namna yoyote ambayo mtu mwingine baki angeweza kuwawezesha, kwa hili naweza kusema linafanana sana na kufanya kazi ya miaka 10 kwa miaka minne. No wonder kuwa elimu hii haitawafaa kwa miaka minne tu, mitano tu ya kipindi cha ubunge. Hapa lazima nikupongeze.
 
Zitto kaza buti mkuu, ila watanzania nashindwa kuwashangaa.Hata mwandishi anauliza swali la kipuuzi kabisa na inaelekea waandishi wengi wa habari hawaielewi hata katiba ya Tanzania inasemaje. Zitto kugombea urais 2010?

Limeniacha hoi,but nimecheka sana Zitto alipojibu swali la mpango wake kuhamia CCM,duh! Usivunjike moyo mkuu,tarajia mambo mengi ya kuudhi kuliko haya

Keep it up bro!
 
Zitto cha msingi ni kuangalia misingi ya chadema ni nini na utume wa chama kwa kizazi hiki.Migogoro ndani ya chama makini ni upotevu.nimesoma post zako nyingi na ukieleza mengi hadi kipato chako kinachohalalisha wewe kumiliki magari mazuri zaidi ya matano sasa sio sifa kulipwa laki tatu na hamsini kwa siku wakati mwalimu kwa mwezi hafiki huko na unaona sawa ni upotevu.Zitto nilikuamini sana lakini sasa mhh. kuna nja mnazo ndani ya chadema za kutatua matatizo ni bora mzifuate kuliko kuanikana kwenye JF.

Bado unaweza ukafanya vizuri katika siasa zetu hizi za bongo but you have to be real and usiendekeze makundi.
 
Chadema lazima muwe imara.

The only thing to archieve that is to fight as a team,kuondoa majungu na makundi. Sera za chama ni madhubuti kuanzia sera ya elimu na nyingine. Umaarufu umeupata na safari ni ndefu kisiasa na majukumu mbele yako ni thabiti. Unahitaji kuwa mvumilivu na kutokukurupuka. Sio kwamba usingeweza uenyekiti bt its too early you need to build up career wise first. Na hata kama ni uenyekiti sio vema kuutafuta kwa lugha za kukosanisha za kupandikiza uadui.

Mathalani uliposema unataka uenyekiti coz mbowe ni bepari wakati wewe ni mjamaa sikukuelewa coz je sere ya chadema ni ujamaa?na kama sivyo ina maana hauamini itikadi ya chama? Zitto katika thread yako moja ulipata kuponda sana vijana wa makao makuu akiwemo john mrema na mnyika je ni sawa kuanika tofauti zenu?

Ni vizuri kuchagua neno la kuandika au kusema !
 
Mimi nilishaanza countdown ya Zitto kuhamia CCM. The guy hana mapenzi tena na chadema. Haya yote anayoweka hapa ni kujaribu kudanganya waandishi uchwara wa bongo ili waandike kwenye magazeti yao (si unajua tena waandishi wanachukua habari hapa moja kwa moja na kuziweka kwenye magazeti yao!).

duh nashindwa kusema neno
 
Zitto asante kwa kutuwekea mahojiano yako na Jamboleo. Hili halina ubaya wowote.

Yangu ni haya:

1. Narudia tena kuwa unatakiwa kuwa makini katika kauli zako. Yaani ongea kitu ukiwa na uhakika nacho na jaribu kuepuka tungo za kuwaunganisha makundi (generalized statements) bila uthibitisho. Mfano kuhusu suala la tuhuma au uvumi wa wewe kutaka kuhamia CCM ulitakiwa tu kulijibu straight kuwa si kweli au hapana na kwamba wasemayo hayo ni wazushi. Maana ukianza kuwanyambulisha kuwa wote wasemao ndio wale walikuwa sijui CCM na wamekukuta na sijui watakuacha hapo unachemka maana inaonyesha kuwa unawafahamu wote wanaokuzushia hilo, kitu ambacho si kweli. Yaani nikweleze kuwa mfano hata mimi hapa hunijui na ninaweza kuwa nimepata fikra kama hizo kwa kuona miendendo na kauli zako za hivi karibuni na mimi wala si wa mwana CHADEMA!

Katika hili pia kuna mfano mbaya wa kauli yako humu ukijibu kuwa WABUNGE WOTE WA CCM walipokea fedha za kifisadi wakati wa uchaguzi uliopita. Zito nakuomba kwa kweli uondoe hii kauli yako. Maana wanaweza kuwa 'baadhi' au 'wengi' lakini ukisema WOTE nadhani ni serious na unatakiwa utuletee hapa sasa uthibitisho huo kwamba walipokea WABUNGE WOTE TANZANIA NZIMA BARA NA VISIWANI kwa njia ipi kama posho au kama nauli (nje ya fungu au fedha halali za Chama zilizokuwepo) au kama msaada wa kuwainua katika kampeni zao mmoja mmoja na ni nani alizigawa Tanzania nzima.

Zaidi ya hayo kama kweli fedha za Umma (Serikali) zilihamishwa kinyamela na kutumiwa kwa shughuli za Chama; ni fair kusema kuwa Viongozi wahusika fulani wa CCM au Serikali (unaowafahamu) walikula njama na kufanya kosa hilo. Mimi na Baba yangu ni wana CCM na kamwe hatukubali kusema kuwa wizi huo ulifanywa na CCM kama Taasisi maana hakujawahi kuwa na makubaliano kama hayo katika vikao vya chama kuanzia Shina hadi Taifa wala si sera ya CCM kuhamisha fedha za Serikali kwa shughuli za Chama bila utaratibu!

Wewe na viongozi wenzako wa CHADEMA mkiamua kutukana watu kamwe hatuwezi kusema kuwa CHADEMA kama taasisi walitukana watu maana Wanachadema hawajahi kshirikishwa katika mkakati huo wa matusi.

2. Kwa sababu una nia ya kujiunga na jamii ya Wanadhuoni na Wataalamu wa Tafiti na Chambuzi, unaribishwa sana. Hata hivyo utatakiwa uanze kuwa makini kabisa katika chambuzi na majibu yako ya sasa ili uanze kuzoea utamaduni wa jamii ya Wasomi.

Mfano:
Hujalitendea haki kabisa swali la hali ya kisiasa nchini. Yaani umekuwa too shallow to be considered as a strong analytical political animal. Siasa ya Tz ni zaidi sana ya idadi ya uwakilishi wa vyama Bungeni na migogoro ya ndani ya vyama. Ingependeza uzungumze kwa ujasili na kutoa misimamo yako juu ya mambo muhimu yanayogusa hali ya kisiasa ambayo yanaweza kuleta mabadiliko ya kimaendeleo mfano sula la Katiba ya Tz, Tume ya Uchaguzi na wajibu wake, Muungano wa bara na Visiwani, Jumuiya ya Afrika mashariki, suala la mgombea binafsi, utengano na wajibu wa mihimili ya dora (Bunge, Mahakama na Serikali), agenda ya kuwa kiongozi na kuwa mfanya biashara au kwa ujumla usemee maadili ya viongozi wa umma n.k Vinginevyo kama suala la siasa ya nchi wewe unajibu tu juu ya uwakilishi na migogoro ndani ya vyama basi unaweza kuwekwa katika makundi ya wachambuzi wa akina Global Publishers n.k ambao wanajadili vitu ndani ya uwanja mfinyu sana wa maisha.

3. Ninavyokuona siku hizi na kupitia majibu yako katika masahili haya wewe ni mwanasiasa wa mlengo wa kati-kati na hutaki mtu au watu wakulaumu. Ni mtu wa kuuma na kupuliza na kutafuta misawazisho. Ungefaa zaidi kuwa Mwanadiplomasia na Mpantanishi kuliko wengine wanavyoweza kufikiri kuwa ni Mwanasiasa Jasiri.

Mfano wa hili ni pale unapojibu isivyo maswali mawili yenye uzito sawia yaani kuhusu Kiongozi (mtu) umpendaye na yule (mtu) unayemchukia tokana na matendo au uongozi wake. Kwenye kupenda au kuvutiwa umewataja watu kwa majina na sababu, iweje sasa kwenye kuchukia utumwagie tu nadharia? Yaani hukujibu swali uliloulizwa wewe umetunga swali lako kuwa ni mambo gani au uongozi wa aina gani unaouchukia? kisha ukaanza kujijibu. Angalia sana utakapoamua kujiunga na jamii ya Wasomi utatakiwa kujibu maswali yanayoulizwa kwa ufasaha. Najua kuwa jibu la swali hilo unalo lakini nadhani wewe na mimi, tunaweza kuwa Wanadiplomasia na siyo Wanasiasa Jasiri tunaothubutu kama Sokoine (RIP).


Zitto endelea kukubali unapokosea, hiyo ndio safari ya kujifunza na kukua.
 
Kweli Jamii forums watu wanamwaga shule, Kibunago I have to tip my hat to you . Shule uliyomwaga ni nzito , umevinyambulisha vitu katika three dimension .
 
Kibunago said:
Katika hili pia kuna mfano mbaya wa kauli yako humu ukijibu kuwa WABUNGE WOTE WA CCM walipokea fedha za kifisadi wakati wa uchaguzi uliopita. Zito nakuomba kwa kweli uondoe hii kauli yako. Maana wanaweza kuwa 'baadhi' au 'wengi' lakini ukisema WOTE nadhani ni serious na unatakiwa utuletee hapa sasa uthibitisho huo kwamba walipokea WABUNGE WOTE TANZANIA NZIMA BARA NA VISIWANI kwa njia ipi kama posho au kama nauli (nje ya fungu au fedha halali za Chama zilizokuwepo) au kama msaada wa kuwainua katika kampeni zao mmoja mmoja na ni nani alizigawa Tanzania nzima.

Kibunago,

..kama CCM walichota fedha za Kagoda na kuzitumbukiza kwenye kasma ya fedha za uchaguzi basi wabunge WOTE wa CCM wamechafuka.

..binafsi naomba uache kumtisha Zitto kwa kutoa matamshi kwamba wabunge wote wa CCM wamechukua pesa za Kagoda.

..kama CCM wanaona wamechafuliwa na Zitto, basi wakamshitaki kwa kauli yake hiyo, au walishitaki gazeti lililochapisha mahojiano hayo.
 
Ndugu zangu, ninawaomba radhi niweke mahojiano yangu haya na gazeti la Jambo Leo katika uwanja wetu. Humo kuna kauli yangu rasmi kuhusu mijadala inayoendelea.

Nawaomba radhi tena kwa kuweka hii interview. Nadhani ni muhimu wakati huu. Naelewa kuna Zitto sana, mniwie radhi kwa hili langu mwenyewe!
Asante sana Zitto kwa hili, angalau sasa gazeti la Jambo leo nitaliingiza kwenye subscription yangu.

Sina neno sana na majibu yako, bali sikufurahishwa sana na aliyekuwa anakuuliza maswali, yaani mwandishi, alikufagilia sana kwa too manye leading questions hivyo kukupa mteremko.

Yako baadhi ya maswali ni facts too ulitakiwa kuzifafanua kama hili la ukabila.
Kuna maeneo ulitakiwa kutoa the motives behind nyuma ya maamuzi yako ikiwemo sababu za kugombea na kisha kujitoa, yes uliwasikiliza wazee, yes, what were the arguments ukagive in easly.

Kuna issues kibao za Chadema kama zilivyoulizwa na Mzee Mwanakijiji ndizo ulizotakiwa kukutana nazo na sio hizi interview fagilia.

Hata hivyo nakushukuru for being, reachable, open, down to earth and besides man of the people.

Pia nampongeza mwandishi, lazima atakuwa ni mchanga kama gazeti lenyewe lakini huu ni mwanzo mzuri, hili gazeti siku za usoni litakuja kuwa kisu kama Tanzania daima, japo kisu chake sasa kinakwenda butu.

Nijukue na fursa hii kumpongeza Pinto na timu mzima ya Jambo leo bila kumsahau 'Mfadhili'
 
Back
Top Bottom