Mahojiano yangu na JamboLeo

It is clear kwamba JK ametupa uwanja mpana sana wa uhuru, wakati mwingine ukijadili jambo lazima uweke mambo mengine constant au uweke scope, otherwise kila jambo liko linked na kitu kingine...

Zitto nakuelewa unavyosema JK ana political tolerance ya hali ya juu sana, na kama asingekuwa nayo mwaka wa BOT/EPA, RICHMOND etc... Taifa lingewaka motto.

Kasheshe,
kwa mifano ya hayo mawili uliyotoa, je kuwa hivyo ni jambo jema au baya kwa Taifa letu?!
 
ulitaka kugombea nafasi ya m/kiti chadema, je zilikuwa mbio za kuelekea ikulu 2010?

haya ndio mawazo ya watu ambayo nadhani wanakosea kabisa. Kwanza sio lazima mwenyekiti wa chama awe mgombea urais. Pili, sina umri wa kugombea urais mwaka 2010 wala mwaka 2015.

sizitaki mbichi hizi?
 
Zitto,
Samahani ningependa kujua mrengo wako ni upi kama mwana siasa.....ultra right,far right,right,right central,central,left central,left,far left au ultra left...nadhani uliposema kazi ya miaka minne ni kama kumi kwako hukukosea....ni mengi yametokea hiyo miaka 4...yangeweza kutoka hata mika 20!!!! keep it up
 
Nimezoea kuona walimu vyuo vikuu wakiacha kazi ya kufundisha na kutafiti na kuelekea kwenye greener pastor (siasa), hii yako ni tofauti! Naona unatoka kwenye greener pastor unaenda kwenye ualimu pasipo 'maslahi'.

Inshaallah nasubiri kuona hili likitokea, pengine litakuwa somo kwa wanazuoni wengine kubaki kwenye taaluma zao ili kutuandalia vijana wenye elimu thabiti ili tusaidiane kulikomboa taifa letu lililodidimizwa na siasa za kulindana za CCM.
 
Mkuu Zitto, mawazo mazuri sana ila nimeshangaa kwamba kiongozi kijana anayeibukia kuwa kiongozi wa zama hizi zetu Barack Hussein Obama, aliye mfano wa "Change" mabadiliko tunayoyahitaji hata haukumtaja kama mtu anayekuvutia! Are you serious about change in Tanzania au you are for the status quo! Chadema badala ya CCM lakini mambo ni yale yale? Kiongozi makini kwa Tanzania ni yule anayefahamu "Africa does not need stong men, Africa needs strong institutions!" Obama
 
Kasheshe,
kwa mifano ya hayo mawili uliyotoa, je kuwa hivyo ni jambo jema au baya kwa Taifa letu?!

SteveD,

To make decision is a must for a leader, i can't deny this! However when to make decision is that CRITICAL.

Kiongozi mzuri hawezi kufanya decision wakati ambapo mioyo ya wananchi wako ndio inafanya kazi na sio vichwa/brain zao!!!

Wakati ule kwa kiasi kikubwa tuliokuwa tukiongozwa na mioyo... sasa hivi waweza weka decision ya BOT/EPA na RICHMOND kwa haki kabisa... maana brain zinafanya kazi na sio mioyo...

Kiongozi mwenye subira ni wa muhimu sana kwani akiwa anataka kuendana exactly na mioyo ya watu... tunaweza kushitukia taifa lilishagawanyika muda mfupi, by the time ana-realize alikosea taifa halipo la kuongoza.

That is what known as maturity na Zitto analijua hili na sio tu analijua bali ni weakness yake kubwa, kuzungumzia mamba mazito wakati usio... na Mh. Sitta anatakiwa kusoma plus za JK kwa karibu sana kama anataka kuwa kiongozi mzuri mbeleni, yeye pia ana-udhaifu kwenye hili.

Wenzake JK na Chief Justice... wako fresh sana kwenye utulivu na tolerance... aidha wangekuwa na kama yeye... Du! Taifa pia lingewaka motto
 
lakini mh.zitto naomba unijibu haya yafuatayo
je, ni kweli kampeni zako za kugombea uenyekiti wa chadema zilikuwa zinafadhiliwa ni fisadi nimrod mkono?

ni nini msimamo wako kuhusu wezi wa fedha za epa? hasa mwizi rostam azizi ambaye inasemekana wewe ni best wako? mbiona sijakusikia ikikemea hili?

weka wazi, je utagombea ubunge kigoma au hata hapa dsm? isije ikawa hii mbinu ya kukimbilia kusoma ni kukimbia harakati in the holy name of mafisadi.

je? huoni kuwa huu si wakati wa kukimbia uwanja wa mapambano?
 
Ma hardcore tunaweza kusema Zitto hakuwa steadfast enough kuwakandamiza mafisadi na CCM.

Nami pia nakubaliana na wewe BLURAY; Zitto has been kind of soft on these FISADIS; may be conscious yake haimruhusu kuwasuta sana hawa jamaa!! Could it be because of his DOWANS involvement?
 
SteveD,

To make decision is a must for a leader, i can't deny this! However when to make decision is that CRITICAL.

Kiongozi mzuri hawezi kufanya decision wakati ambapo mioyo ya wananchi wako ndio inafanya kazi na sio vichwa/brain zao!!!

Wakati ule kwa kiasi kikubwa tuliokuwa tukiongozwa na mioyo... sasa hivi waweza weka decision ya BOT/EPA na RICHMOND kwa haki kabisa... maana brain zinafanya kazi na sio mioyo...

Kiongozi mwenye subira ni wa muhimu sana kwani akiwa anataka kuendana exactly na mioyo ya watu... tunaweza kushitukia taifa lilishagawanyika muda mfupi, by the time ana-realize alikosea taifa halipo la kuongoza.

That is what known as maturity na Zitto analijua hili na sio tu analijua bali ni weakness yake kubwa, kuzungumzia mamba mazito wakati usio... na Mh. Sitta anatakiwa kusoma plus za JK kwa karibu sana kama anataka kuwa kiongozi mzuri mbeleni, yeye pia ana-udhaifu kwenye hili.

Wenzake JK na Chief Justice... wako fresh sana kwenye utulivu na tolerance... aidha wangekuwa na kama yeye... Du! Taifa pia lingewaka motto

Nashukuru kwa maelezo.

Twajua kwamba "justice delayed is justice denied." Kwa maoni yako, je hili swala linahusiana na justice au kuoneshana namna ya kuongoza na styles zake?!
 
Nashukuru kwa maelezo.

Twajua kwamba "justice delayed is justice denied." Kwa maoni yako, je hili swala linahusiana na justice au kuoneshana namna ya kuongoza na styles zake?!

This is only apply, pale ambapo kuchelewa kwake kuamua kuna madhara sio ya kufikirika bali ya kweli na ya kuonekana kwa wananchi.

Mfano kesi ya Mramba isipoamuliwa mwaka huu kwa mfano SteveD utakuwa umeadhirika kwa kiasi gani? Na je kesi ya Mramba ikikimbizwa kiasi kwamba Mramba akakosa haki ya kujitetea? Nani atakuwa ameathirika Mramba au SteveD?
 
Pia niliazimia kuhakikisha kuwa uchumi wa nchi unasaidia kuongeza ubora wa maisha ya wananchi. Kazi ambayo nimeifanya kwa ufanisi sana. Nimekuwa mbunge kwa miaka 4 tu lakini kazi niliyofanya ni kana kwamba nimekuwa mbunge kwa miaka 10 au zaidi. Kazi yangu imefahamika kwa wananchi kuliko wabunge wengi ambao wamekuwa bungeni kabla yangu.

Nimeifanya ajenda ya madini iwe ya kitaifa na hata kupelekea Rais kuunda kamati ambayo imetoa taarifa nzuri sana na sasa sheria mpya ya madini imetungwa na kusubiri kupitishwa Bungeni. Niliandika mabadaliiko ya sheria ili mahesabu ya vyama vya siasa yakaguliwe na CAG na sheria tayari imepita. Hii itadhibiti matumizi mabaya ya fedha za umma katika vyama vya siasa.

Toka mwaka 2006 Bunge limepitisha bajeti ya ruzuku kwa vyama ya zaidi ya shilingi 67 bilioni lakini fedha zote hizi zilikuwa hazikaguliwi na CAG. Kuanzia mwaka huu wa fedha zitakaguliwa. Hii ni kazi ya kujivunia sana na siamini kama kna mtu atanichukia kwa kazi hii.

Kama hayo yahusuyo masuala ya Ruzuku na Madini uliyotaja hapo juu ndiyo mafanikio yako makuu tokea upewe Ubunge, basi ni wazi maendeleo ya waliokupeleka Bungeni hayana kipaumbele kabisa kwa mtazamo wako.

Tulitegemea ungetuorodhoshea mafanikio uliyowapatia Wapiga kura wako, au labda kutokana na sababu zinazofahamika hawapo kwenye kadamnasi ya Wachangiaji wa JF na Wasoma Magazeti wa JamboLeo?
 
... hao wanaoeneza kuwa mimi nitahamia CCM kwanza walikuwa CCM kabla, na pili wataenda CCM wataniacha mimi CHADEMA. CHADEMA kwangu mimi ni zaidi ya chama, ni Movement! Ni vuguvugu la harakati za kuhakikisha kuwa watanzania wanakuwa na demokrasia pana zaidi bila kuathiri uzalendo wa Taifa letu. Kijiji kwangu watu waliteswa kuijenga CHADEMA, watu walifungwa, vijana wenzangu walilala juu ya paa za nyumba ili kuijenga CHADEMA na toka hapo kijiji changu ch MWANDIGA hakijawahi kuwa na kiongozi wa CCM, toka mwaka 1994. Hao wanaosema mimi ntaenda CCM wajiulize wana historia gani na CHADEMA? Wana machungu gani na CHADEMA?

Mhe.Zitto hapo unataka kusema kuwa Dr.Slaa alikuwa CCM na hivyo atarejea nyumbani?

Mhe.Zitto, ina maana wewe peke yako ndio una historia na CHADEMA? AMA ulikuwa unatuma ujumbe gani na ni historia gani hiyo?

Ina maana wewe historia ya hao vijana wa kijijini kwako ndio ya kwako ama unamaanisha nini?mbona hukuenda na wewe kulazwa juu ya paa ? unajenga historia kwenye migongo ya watu?

Mhe.Zitto, ina maana wewe ndio una machungu na CHADEMA kuliko walioko huko ?
Ina maana wengine hawana uchungu na ndioo maana kazi yao ni kuitafuna ruzuku ya chama , wakati wewe tuu ndio huitafuni?

Mhe.Zitto, nitashukuru sana ukijibu maswali yangu kwani nimesoma hapo na kuona fumbo kubwa sana kuwa kumbe huko CHADEMA wapo wengye historia na wengine hawana historia, na nimejenga tafsiri kuwa ili uweze kuwa mwanachama na uweze kuzungumzia mambo ya chama ni lazima uwe na histori, na kama ulikuwa chama kingine basi ukija huko utakuwa kila siku unatazamwa kama mtu adui na ambaye kuna siku utarejea kwenye chama chako cha zamani, hivyo basi kwa sisi ambao tuko vyama vingine tusije?
 
Mhe.Zitto, ina maana wewe ndio una machungu na CHADEMA kuliko walioko huko ?
Ina maana wengine hawana uchungu na ndioo maana kazi yao ni kuitafuna ruzuku ya chama , wakati wewe tuu ndio huitafuni?
Majungu haya kha!!
 
.... Hao wanaoeneza kuwa mimi nitahamia ccm kwanza walikuwa ccm kabla, na pili wataenda ccm wataniacha mimi chadema. Chadema kwangu mimi ni zaidi ya chama, ni movement! Ni vuguvugu la harakati za kuhakikisha kuwa watanzania wanakuwa na demokrasia pana zaidi bila kuathiri uzalendo wa taifa letu. Kijiji kwangu watu waliteswa kuijenga chadema, watu walifungwa, vijana wenzangu walilala juu ya paa za nyumba ili kuijenga chadema na toka hapo kijiji changu ch mwandiga hakijawahi kuwa na kiongozi wa ccm, toka mwaka 1994. Hao wanaosema mimi ntaenda ccm wajiulize wana historia gani na chadema? wana machungu gani na chadema?

majungu haya kha!!

kasema yeye sio mimi sasa majungu yanatoka wapi tena?
 
Kiongozi makini kwa Tanzania ni yule anayefahamu "Africa does not need strong men, Africa needs strong institutions!" Obama

I concur, ndo maana kila siku mnapopongezana na kusifiana kuhusu ama Zitto au Kikwete au salim naamini tunatwanga maji kwenye kinu.

Alikuwepo Nyerere lakini kwa sababu hakututengenezea (hakutuachia) taasisi imara tumebaki tunayumba mpaka leo. Zitto types watakuwa wanakuja na kupita, lakini taasisi imara zingetujengea misingi ambayo kila mtanzania tokea utoto angekuzwa nayo!!!

Ngoja tuendelee kusubiri miujiza!!
 
Kuna maswali mengi katika mahojiano haya ya JamboLeo. Nilikuwa najibu nilichoulizwa na mwandishi jamani. Wengine wametaka niseme zaidi. Inshaallah kwenye interview nyingine kama itatokea. It was a short interview and i thought ni vizuri kushare nanyi. Hata hivyo maoni yote nimeyachukua.....
 
Mkuu Zitto, mawazo mazuri sana ila nimeshangaa kwamba kiongozi kijana anayeibukia kuwa kiongozi wa zama hizi zetu Barack Hussein Obama, aliye mfano wa "Change" mabadiliko tunayoyahitaji hata haukumtaja kama mtu anayekuvutia! Are you serious about change in Tanzania au you are for the status quo! Chadema badala ya CCM lakini mambo ni yale yale? Kiongozi makini kwa Tanzania ni yule anayefahamu "Africa does not need stong men, Africa needs strong institutions!" Obama

Kila mtu anamtaja Obama. He is simply a phenomenal. Hata Nyerere sikumtaja. Hata Castro sikumtaja. Hata Mandela sikumtaja....... the list is long
 
Nami pia nakubaliana na wewe BLURAY; Zitto has been kind of soft on these FISADIS; may be conscious yake haimruhusu kuwasuta sana hawa jamaa!! Could it be because of his DOWANS involvement?

Nilikuwa najibu maswali ya mwandishi Bulesi. Hakuuliza kuhusu hayo. Angeeuliza ningesema ambayo wala sio mapya maana niimeshasema sana. Nimesema sana on EPA, nimesema on Richmond/Dowans and sina involvement yeyote kama unavyotaka kusuggest hapa.

I have never been soft on corruption. I have even drafted a legislation on Conflict of interest code.................!
 
Kila mtu anamtaja Obama. He is simply a phenomenal. Hata Nyerere sikumtaja. Hata Castro sikumtaja. Hata Mandela sikumtaja....... the list is big

Zitto,

Mimi nakuaminia sana, lakini katika kukujenga... nakuomba ujirekebishe kwenye haya.

1. Punguza umimi, unao sana mkuu, mfano hii interview haikuwa lazima uilete wewe.

2. Punguza kuona wengine wajinga, hii mara nyingi umetukana wazee wenye heshima zao Bungeni, tumia lugha laini lakini ujumbe ufike... Nyerere alikuwa akimtusi Mwinyi lakini kwa lugha ya kiutu uzima.

3. Munkari, sio kila jambo linahitaji majibu, jifunze kutoka kwa Mzee John Samuel Malecela. Usiwe kama Mh. Sitta.

Mwisho nakukubali sana mzee endeleza libene.
 
Back
Top Bottom