Mahojiano Ya Mwandishi Jackton Manyerere Na Wana- Uamsho Zanzibar

Kakke

JF-Expert Member
Dec 4, 2010
1,883
1,482
[h=1][/h]Written by maalim // 15/06/2012 // Habari // 3 Comments


Mahojiano Ya Mwandishi Jackton Manyerere Na Wana- Uamsho Zanzibar
5 June 2012
Mwandishi Manyerere aliyefanya mahojiano haya akiwa na wanauamsho
Haya ndiyo madai ya Uamsho kuuvunja Muungano
*Wasema bayana kwamba wanataka Zanzibar iwe ‘Sovereign State’, ijitawale yenyewe
*Wasema Dar es Salaam ilikuwa ya Zanzibar, maili kumi kuingia ndani, mikataba ipo
*Kiongozi ahoji: Kilomita chache zinakushughulisheni wakati mna mapori tele
Jumuiya ya Uamsho ya Visiwani Zanzibar hivi karibuni ilijikuta matatani, baada ya Jeshi la Polisi kutumia mabomu ya kutoa machozi kutawanya wafuasi wake. Mwandishi wa gazeti la JAMHURI, Manyerere Jackton, amefanya mahojiano ya ana kwa ana na Amiri Mkuu wa Jumuiya ya Maimamu Zanzibar, Sheikh Farid Hadi Ahmed, aliyeeleza lengo kuu la Jumuiya hiyo ya Kiislamu.
JAMHURI: Ni nini chanzo cha vurugu za Mei 26?
Sheikh Farid: Kilichotokea hapa kwa muda mrefu, japo inasikika Jumuiya ya Uamsho ndiyo inayofanya mihadhara, lakini ni Umoja na Jumuiya za Kiislamu ambazo zimekuwa zinaendesha mihadhara. Tumefanya mihadhara zaidi ya mia moja hadi sasa – mikutano zaidi ya mia pamoja na makongamano tofauti. Na lengo zaidi hapo awali lilikuwa ni kuwaelimisha watu kujua Sheria ya Mabadiliko ya Katiba na kuona ni jinsi gani inawabana Wanzibari na haijawapa ile haki yao ya kuujadili Muungano.
Na baada ya hapo kilichokuwa kinazungumzwa zaidi ni kuwaelimisha wananchi kujua haki yao kujua mustakabali wa nchi yao na umuhimu wa kuuhoji Muungano au kuujua Muungano. Wazanzibari wao kama washirika na Watanganyika wana haki ya kuuhoji Muungano. Sasa hii mihadhara imeendelea kwa muda mrefu na ilikuwa inakwenda misafara ya mbali mingine hadi shamba. Na ilikuwa misafara mikubwa inaweza ikabeba magari mia mbili, mia mbili na zaidi, kuna mapikipiki, watu wanakwenda wanarudi kwa usalama wala hakuna tabu na matatizo yoyote. Hayo yote ndiyo kwa jumla yamefanyika.
Sasa kilichojitokeza hivi karibuni ni kuwa lilifanyika kongamano. Katikati ya lile kongamano watu waliamua kutembea, kama ni matembezi tu lakini si maandamano hasa. Maandamano ni kitu ambacho kimeandaliwa, kina slogan yake, kina ujumbe, kinaenda maeneo maalumu kufikisha ujumbe maalumu. Haikuwa hivyo.
JAMHURI: Je, Polisi walivamia?
Sheikh Farid: Polisi hawakuvamia, hawakuwahi kuvamia. Na walipokuja kwa kweli walikuja matembezi yameanza kutoka maeneo ya Lumumba. Watu wote wameacha baiskeli zao, vifaa vyao palepale na walinzi walibaki eneo lile. Watu wametoka wametembea mpaka hapa Michenzani, katika roundabout, wameshuka chini mpaka maeneo ya Kariakoo. Kwa hiyo watu wakaenda moja kwa moja wakarudi kwenye kile kiwanja walichoanzia. Wakarudi palepale wakaaa kitako. Wakawa wanaendelea na shughuli zao. Wakazungumza, wakazungumza mpaka wakamaliza. Walipomaliza kuzungumza wakatawanyika wakaenda majumbani mwao salama salmini.
Nashangaa sasa alipokuja Waziri, Jeshi la Polisi wamemdanganya. Na alipokuja IGP wamemdanganya wamemwambia uongo. Wanamwambia kuwa Jeshi la Polisi limejaribu kuzima fujo, lakini si kweli. Ni uongo huo. CD zipo zinauzwa kila pahali. Wazi kabisa. Zinaonyesha maandamano kitu mbali, na zile fujo kitu mbali kabisa. Hayo matembezi kitu mbali na hizo fujo kitu mbali kabisa.
JAMHURI: Nini chanzo kilichosababisha fujo?
Sheikh Farid: Fujo ilisababishwa na Jeshi la Polisi kukosa utaratibu, kuchukua mazoea yale yale ya uhuni na mabavu. Ndicho kilichofanyika kwa sababu kati ya mmoja wa watu waliohudhuria pale kwenye viwanja palipokuwa na mdahalo ni Maalim Musa Juma, yeye ni mmoja katika wahadhiri wala si kiongozi wa Jumuiya ya Uamsho, lakini ni mwalimu ambaye anahadhiri, anafundisha. Sasa siku ile yeye alikuwa si mzungumzaji, alikuwa mkaribishaji wa wazungumzaji. Walichokifanya wakati wa majira ya saa moja na kidogo usiku, yumo msikitini mwake anasomesha, alikwenda mtu ana shida naye. Alipomwita, kutoka nje kuwafuata wale watu wakamkamata kwenye kiuno, na wengine watano wamekuja wamemzoa wamemshindilia kwenye gari wakampeleka kituo cha Polisi. Wale vijana waliokuwa pale – wanafunzi na watu ambao wanampenda, na sasa kimekuwa kitu sensitive kwa sheikh kumdharau. Sasa hii dharau iliyofanyika, wananchi hawajakubali kwa hiyo wakaanza kupigiana simu wote kwamba Sheikh wetu kakamatwa, twendeni tukamdai kwanini kakamatwa, na tujue. Kama kumchukulia dhamana tumchukulie.
JAMHURI: Lipi jina sahihi la Jumuiya hii? Ni Uamsho au Muamsho?
Sheikh Farid: Hizi harakati zinazoendelea hapa nchini (Zanzibar) zinafanywa na Umoja wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu. Ndiyo wanaofanya hizi harakati zote. Isipokuwa katika utaratibu wa mambo ya mihadhara, Jumuiya pekee ina uzoefu mkubwa kwenye mihadhara ni Jumuiya ya Uamsho.
JAMHURI: Taasisi ya kidini kwanini ijikite kwenye siasa?
Sheikh Farid: Hakuna tatizo lolote. Hakuna tatizo kikatiba, hakuna tatizo kidini yetu, hakuna tatizo kimtazamo sahihi wa wanasiasa. Kote hakuna tatizo. Mtazamo sahihi wa wanasiasa. Tumchukue Rais wetu wa hapa Zanzibar, Mheshimiwa Jumbe ameandika kitabu na kuna sura maalumu anaita “Dini na Siasa”. Kaeleza mengi. Kaeleza jinsi watu wengine walivyo katika dini zao, lakini akaelezea ama upande wa Uislamu huwezi kutenganisha dini na siasa. Hilo moja. Basi kama watu wanajua wanasiasa, huyu mwanasiasa anatamka kwenye kinywa chake. Alikuwa Rais wa Zanzibar, Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Tanzania. Alikuwa pia Makamu wa Mwenyekiti wa CCM na kaeleza wazi kabisa kwenye Uislamu huwezi kutenganisha na siasa.
Ukija kwenye Koran, Uislamu unahesabu kuwa dini ni mfumo kamili wa maisha ya mwanadamu, ikiwamo sehemu ndogo inayoitwa “siasa”. Siasa kwenye Uislamu au kwenye lugha ya Kiarabu, neno hilo hilo siasa kama lilivyo, maana yake ni “uongozi”, kwa hiyo uongozi ni sehemu ndogo, ni mlango katika maisha ya mwanadamu au katika dini ya Kiislamu. Kwa hiyo sisi kuzungumza siasa ni sahihi kabisa.
JAMHURI: Nyuma ya Uamsho kuna msukumo wa kisiasa?
Sheikh Farid: Uamsho haina uhusiano na CUF. Hili suala limeanza ilipokuja hii rasimu ya Katiba, ilipokuja kama rasimu, Serikali nzima iliikataa, Wazanzibari waliikataa wakaona wamedharauliwa. Iliporudi ikaja na dharau nyingine, badala ya kuletwa kama rasimu ikaletwa kuwa ni sheria sasa…kinguvu. Unaposema sheria maana yake ni nguvu, utake usitake. Ikaletwa kama sheria na ilikuwa iletwe kama rasimu. Hilo tatizo la mwanzo. Tatizo la pili, ndani ya rasimu ile kama alivyosema Mheshimiwa Kikwete mwenyewe wakati anazindua Tume, hakuna mjadala wa Muungano mle ndani yake, ni kwenda mbele tu kuuboresha, lakini suala la kutazama mustakabali wa Zanzibar je, inafaidika na Muungano? Hilo hakuna. Imeshapita miaka 48 na hawajawahi kuulizwa huko nyuma. Sasa sisi hapa ndipo tulipoona kuna haja ya kuulizwa, na njia ya kufanya hivyo ni kupitia kura ya maoni.
JAMHURI: Kuna umuhimu wa kuwapo Muungano wa Tanganyika na Zanzibar?
Sheikh Farid: Sisi tunachotaka ni kura ya maoni. Wazanzibari waseme wenyewe. Hakuna mtu amepewa kibali cha kumsemea mtu. Hakuna Mtanganyika wala Mzanzibari. Kila mtu aseme mwenyewe na hiyo ndiyo demokrasia, kwa hiyo sisi kama Jumuiya ya Taasisi za Kiislamu tunasema iitwe kura ya maoni. Nisiseme mie, mie nitasema kwenye karatasi. Kila Mzanzibari atasema kwenye karatasi. Kura ya maoni ni nyepesi tu.
JAMHURI: Mbona hamjasikika mkilaani kuchomwa makanisa? Mnaunga mkono kitendo hicho?
Sheikh Farid: Tumeshatoa taarifa nyingi sana. Tatizo unajua hakuna uadilifu kwenye uandishi wa habari. Hakuna uadilifu hata kwenye hii TV yetu iliyopo hapa (ZBC), hata redio zilizoko hapa hakuna uadilifu bwana. Hii ni kwa mtu anachukia kitu anakuwa si mwadilifu. Na haya ndiyo yanayosababisha matatizo kama haya kuzuka. Mtu unamnyima haki yake anafika mahali hawezi kustahamili. Kwa hiyo sisi kiufupi tunalaani vibaya sana suala zima la kuchoma makanisa, dini haisemi hivyo. Si dini yetu wala si nyingineyo, haisemi hivyo. Lakini tunashangazwa vilevile, tumechoma makanisa, sisi ameuliwa imam ndani ya msikiti na Jeshi la Polisi…ameuliwa imam ndani ya msikiti, huko Mwembechai kwenu huko Dar es Salaam ameuliwa Muislamu ndani ya msikiti. Acha kuchoma makanisa. Sisi tunalaani uvunjifu wa amani wa aina yoyote – ikiwa wa ubaguzi wa kidini wa kuchoma makanisa, ikiwa wa kuwahujumu watu, tukubali haya si mafunzo maana hata kwenye nyumba yangu wamekuja wamehujumu ndani, wamepiga mabomu ndani ya nyumba, wamevunja mlango.
JAMHURI: Mambo gani ambayo Zanzibar haitendewi haki ndani ya Muungano?
Sheikh Farid: Ni mamlaka kamili ya kimaamuzi ya kimataifa, ya ndani na nje ya nchi. Hiki ndicho tunachokosa Zanzibar. Wanaita Sovereignty, Zanzibar inakosa sovereign yake kwa hiyo tunataka sovereign state. Kama ni Zanzibar iheshimike, kama ni Rais wa Zanzibar aheshimike, Serikali ya Zanzibar iheshimike ndani na nje ya nchi. Iwe na mamlaka kamili. Na wao wenyewe (Wazanzibari) wataona utaratibu nini watafanya. Kwa hiyo wananchi waulizwe, chepesi tu hakina tabu. Si waliulizwa kwenye Serikali ya Umoja wa Kitaifa na hakupigwa mtu?
JAMHURI: Marekani majimbo yale ni nchi – ni Muungano, mbona majimbo hayana mamlaka kamili kama nchi?
Sheikh Farid: Mbona upo muungano tofauti na huo. Kama Umoja wa Ulaya si upo? Upo vipi? Katika Umoja wa Mataifa si kila nchi ina kiti?
JAMHURI: Huo si muungano ni kama jumuiya tu.
Sheikh Farid: Huo ni muungano, si wameungana katika vitu maalumu? Wamarekani wameamua wao vile. Sisi tumeamua hivi. Wao hatuwasemei. Sie tunaamua tunachotaka sie. Na sisi hawezi kutulazimisha mtu tuamue kwa akili za Kimarekani. Wamarekani wataamua wao wenyewe Kimarekani, haki za Kizanzibari zitaamuliwa Kizanzibari-Zanzibari.
JAMHURI: Ungependa Muungano wa uwe wa namna gani?
Sheikh Farid: Mie ninachosema ule mchakato wa Katiba imekuwa sawa na kumchukua ng’ombe na gari ya ng’ombe halafu ng’ombe ukamweka nyuma gari ya ng’ombe ukaweka mbele. Au mashine ukaweka nyuma, gari ukaweka mbele. Sijui itakwenda vipi. Sasa tunashangaa, watu wataalamu wana akili lakini inaonyesha akili zao zimefika mahali wanatuona sisi wapumbavu. Sisi bwana tunasema ilivyo kitu kinachowafungamanisha Wazanzibari na Watanganyika ni Muungano. Ninyi mnataka kujadili Katiba ya Muungano, hili tatizo la Muungano kwanini msilizungumze mwanzo? Hili la kuzungumza mwanzo. Kwanza, lizungumzwe hili kwanza mpaka likae sawasawa halafu ndiyo tuzungumze Katiba.
Sasa unasema mimi na wewe tunataka kufanya biashara njoo tufunge mkataba mimi na wewe. Si tuzungumze tukubaliane kwanza halafu ndiyo tuandike mkataba kwa sababu Katiba ndiyo umefunga kila kitu. Kitu kinachotufungamanisha tukizungumze mwanzo. Wananchi wapewe fursa wazungumze mwanzo. Watu wanapewa fursa hizo wasiokuwa na nchi mwanzo…hii ni nchi. Hii ni nchi. Ilikuwa ni nchi tena kubwa mpaka Dar es Salaam yote ilikuwa yetu ile, tena mikataba ipo ya kimataifa ya kuonyesha Dar es Salaam yote ile ni yetu sisi. Na kuingia ndani huko maili 10.
JAMHURI: Je, mtaidai Dar es Salaam?
Sheikh Farid: Hatuna shida nayo hiyo. Tutakuachieni. Sisi watu makarimu sana sie. Tutawaachieni. Nashangaa nyie tu hizi kilomita za mraba ngapi zinakushughulisheni nyie wakati mna mapori tele kule juu, na mna ardhi ya kwenda na kurudi, mashamba ya kwenda na kurudi mnang’ang’ania hiki tu!
JAMHURI: Muungano ukivunjika, nini hatima ya Wazanzibari wanaoishi/waliowekeza Bara?
Sheikh Farid: Jawabu moja, wewe huwajui Watanzania wanaofanya biashara Kenya? Uganda? Hatima yao ipo vipi? Sasa ninyi inaonyesha kuna watu wana fikra mbovu katika vichwa wanaona maana yake tukiwa hivi (tukitengana) tutakuwa maadui, hata! Udugu lazima utabakia. Tumeoa kule. Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar usingizi wake (mkewe) ni wa kule (Bara) au hujui wewe? Hatuwezi kuachana bwana, watu watabakia, mapenzi yapo, undugu upo, ujirani mwema kabisa, waliokuwapo hapa Watanganyika watabakia, Wakristo hapa watabakia, itakuwa kila kitu kina utaratibu. Si maana yake kwamba mmetengana muwadhulumu wale ndugu zenu (walio Bara). Mkiwadhulumu sawa! Sisi kawaida yetu hatuko hivyo.


[h=4]Related Posts[/h][h=3]Mbunge avishutumu vyombo vya habari vurugu za Zanzibar[/h]
[h=3]Form independent team on Zanzibar chaos-MP[/h]
[h=3]Zanzibar hospital to start offering cancer treatment[/h]


[h=3]Zanzibar increases taxes, fees to cover budget gap[/h]
[h=3]Video : Sala na Duuwa ya Pamoja – Tibirinzi Zanzibar[/h]





[h=3]3 Comments on "Mahojiano Ya Mwandishi Jackton Manyerere Na Wana- Uamsho Zanzibar"[/h]


  1. Wamtambwe 15/06/2012 kwa 8:10 mu · Ingia kujibu
    Mimi rafiki zangu wa Tanganyika siwafahamuni. Kama kuna wazanzbari wanaofanya biashara Dar (Tanganyika) wanaofaidika ni nani? Nafikiria serikali ya Tangananyika ndio inayofaidika zaidi kwa kodi na nilitegemea mutafurahi kama watu kama wale wale watabakia waendelee biashara zao hata kama muungano utavunjika.
    Musitegemee Wazanzibari wataacha kudai haki kwa kishingizio ndugu zao watafukuzwa Bara.
    Kumbukeni kwamba Wazanzibari washadhulumiwa sana, na hawajafungua kesi mahakamani ya kwamba warudishiwe kile chote mulichowadhulumu kwa muda wa miaka 48. Wanajuwa hamtolipa na hamna uwezo wa kuwalipa. Kitu wanachotaka Wazanzibari wanataka waanze tena kutoka zero lakini wao wenyewe, kama ni mafanikio ni yao na kama itakuwa ni matatizo pia ni yao wenyewe na sio ya kusababishwa na mtu mwengine.
    Wazanzibari wanaofanya biashara Tanganyika wako pale kisheria na sheria za nchi zinawaruhusu kufafanya hivyo. Kwa hiyo kile chote walichichuma ni chao kisheria. Kwa hio kama mutaonelea sio vyema kubakia pale Dar la mihimu ni kuruhusiwa kutokana na sheria za nchi waondoke na kilicho chao. Kama ni nyumba watauza na watalipa mapato serikalini kutokana na sheria za nchi. Wao wenyewe ndio wataamua kurudi Zanzibar au kuekeza katika nchi nyengine za Jurani.
    Kumbukeni kitu kimoja tu, vyenginevyo vyovyote mutakavyoamua mujuwe ziko Mahkama za kimataifa , sheria hatoikwepa yoyote.
    Shime wazanzibari, wakati wa Ukombozi umewadia!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!




  2. Wamtambwe 15/06/2012 kwa 8:16 mu · Ingia kujibu
    Kumbukeni Sheria ni msumeno hukata mbele na nyuma!!!!!!!




  3. amini 15/06/2012 kwa 9:37 mu · Ingia kujibu
    Katika utafiti wangu wa Muda mrefu nilio fanya, inaonekana Zanzibar haiko katika Muungano wa Zanzibar na ilokuwa Tanganyika.
    Zanzibar ni kweli ni teka la Tanganyika liko chini ya Ukoloni wa Tanganyika ijitayo Tanzania hivi sasa.
    Hii inaonyesha ishara za Tanganyika kuitia kwenye makuucha yake na isipate kufurukuta na kila ikifurukuta inapata mbinyo mkali, na ikiweza kujinasua katika makucha hayo basi Wazanzibar waloko bara chamtema kuni watakiona.
    Ndio maana watashwa wachina,wahindi,wasouth africa na wengineo waliokuwa hawana Muungano nchi zao na Tanganyika, lakini watakao sulubiwa kichuki ni Wazanzibar kukataa kuendelea huo Ukoloni.
    Hivi sasa zamira za Juliasi Nyerere na ndugu zake zinatowa picha halisi ya kuwa Muungano ilikuwa si hiari ya dola mbili huru zilizoungana, ilikuwa ni ukoloni wa ilokuwa Tanganyika kuitawala Zanzibar kimabavu.
    Baada ya kuvunjika Muungano chuki zidi ya wazanzibar waichio Tanganyika
    Hivi sasa kauli za Watanganyika takribani 99% wote wanakubaliana mawazo yao kuitawala kimabavu Zanzibar bila ridhaa za Wazanzibar wenyewe.
    Na vishingizio vyao vya uongo na imani ya Mamba nikuwa eti Muungano ukivunjika Wazanzibar waloko bara vipi? na vipi vyakula kutoka bara itakuwa vipi? umeme vipi?
    Hivi ndio vichingizio vyao vikubwa, nazani Zanzibar ni kisiwa na kivugo cha Tanganyika na Zanzibar na kabla ya hapo nyuma 1964 Zanzibar ilikuwa nchi huru ikiitwa Dola ya Watu wa Zanzibar na Tanganyika ilikuwa huru.
    Ikiwa ilikuwa hivyo basi nikigezo tocha kuwa Zanzibar na Tanganyika zilikuwa na mambo yake mbali na kila nchi ikijiendesha kivyake na tulikuwa tukiishi na ujirani mwema.
    Sasa vipi tushindwe kuichi na ujirani mwema kama hapo mwanzo tuliweza? Tanzania si Bara lililozungumkwa na nchi jirani kibao? Zambia,Kenya,Uganda,Burundi, etc na zote hizo watu wa mipakani kwake wanaingiliana ki makabila utamaduni na mambo mengi tu, jee hizo nchi zimeungana na Tanzania?.
    Au iwe nongwa kwa kuwa Wazanzibar wameamua kuvunja Muungano tu? hii ndio tunayosema Ukoloni na sio Muungano kama Muungano basi ni uchirika na uchirika mara zate ni hiari .
    Haiwi ndowa ya mkke na Mume huvunjika itakuwa Muungano fake,

 
Jee ukivunjika Muungano huu unaoambiwa na Juliasi Nyerere kuwa ni wahiari sio wa nguvu au kulazimishana, Wachina,wahindi na wasaouth afrika mutawafukuza?.

Maana na wao hawamo katika Muungano lakini wanafanya biashara hapo na kulipa kodi, sasa ikiwa mutawafukuza Wazanzibar jee hao vipi?.

Au chuki zitakuwa zidi ya wazanzibar kuwakataa?.
 
KUMBE LISEMWALO LIPO !!!

Post #28 ; Thread: Zanzibar is gone
Ebu msikieni na huyu anavyosema.....

" Na kwambia Mwl. Nyerere alikosea step kusema kuwa Eti Wazanzibar wakijitenga, dhambi yao hiyo haitaisha hapo wataanaza kujitenga pia kwa kuliuzana we mzanzibari au wewe ni mzanzibari, wataendelea kusema wewe ni Mpemba au ni Muunguja....narudia Mwalimu alikosea ....wazanzibari wala hawawazi hivyo... Wazanzibari wakisha kujitenga watakuwa wamoja kuliko walivyowamoja sasa baada ya muafaka wa CCM na CUF... Na umoja huo utadhihiri hivi punde tu baada ya kujitenga na Tanganyika watakapounganisha nguvu kudai kurudishiwa maeneo yote ya pwani ya Tanzania Bara, Kenya na Msumbiji pamoja na kisiwa cha Mafia. Wazanzibari wanayosababu ya "msingi" ya kudai Zanzibar huru....Watanganyika hili hawajaliona Mwl. akuliona lakini Mkapa aliliona ndiyo maana akiulizwa juu ya Muungano wakati wa Utawala wake alikuwa na majibu yaliyokuwa yana onyesha wasiwasi wake kwenye nia ya kuzitenga nchi mbili hizi..... Nakuelezeeni Mwalimu alikosea step......

Sikuendelea kumsikiliza maana nilijua kwa vyovyote vile maelezo mengine yatakuwa yanazunguka hapo hapo.

SWALI:

Wazanzibari mnania hiyo ya kuteka pwani ya Tanzania bara baada ya kututenga na kuimarisha nchi yenu?
 
KUMBE LISEMWALO LIPO !!!

Post #28 ; Thread: Zanzibar is gone
MpigaKelele

Hujajibu swala bado unajiganganya kwa mambo yasio kuhusu, na kukumbatia Muungano ambao kwa Wananchi wa Zanzibar ni uharo wa Bata kunya .

Jee kabla ya Muungano wa 1964 Wazanzibar walikuwa ni Watanganyika au Wazanzibar na hivi sasa ni nani ?

Nyiyi mulitakiwa Baada ya Wazanzibar kupinga Muungano ni nema kwenu kudai Tanganyika yenu Juliasi alio ipoteza, Muungekuwa na Tanganyika yenu na katiba yenu basi kidogo joto lingepungua la Muungano maana mchirika wa Zanzibar angekuwepo lakini kilimacho hichi kwa wazanzibar hakikubaliki ,kama nyiyi mumeridhia kifo cha Tanganyika basi kivyenu.

Mh MpigaKelele vita vya ndugu kwa ndugu havina haja ya kuvingilia wewe, after roul Munguja na Mpemba wote ni wana wa Zanzibar kindaki ndaki wewe huna haja ya kujuwa hilo, Uguja na Zanzibar hazina mikataba ya Muungano.

Wewe la umuhimu ni kuchika kamba ile ile ya kuwa Muungano ukivunjika Mutawafukuza Wazanzibar na kuto kuwauzia viazi vibovu na nyanya?, na kupata maduka na majumba kurisi hii ndio laumuhimu kwako wewe kulijuwa nyiyi ni majambazi tu na hizo ndio tabia zenu.

Wazanzibar waloko Bara ni walipa kodi kama Wahindi,wasouth afrika,wachina na jamii nyingine, sasa chakujiuliza Watanganyika wauza garanga ,ukahaba na ujambazi huko Zanzibar tuwarudishe kwao bada ya Kuvunja Muungano au vipi? maana ujambazi na ukahaba hauingizi pato Zanzibar zaidi ya mafaa kwa jamii ya Kizanzibar.
 
Last edited by a moderator:
MpigaKelele ............

Mh MpigaKelele vita vya ndugu kwa ndugu havina haja ya kuvingilia wewe, after roul Munguja na Mpemba wote ni wana wa Zanzibar kindaki ndaki wewe huna haja ya kujuwa hilo, Uguja na Zanzibar hazina mikataba ya Muungano.

Wewe la umuhimu ni kuchika kamba ile ile ya kuwa Muungano ukivunjika Mutawafukuza Wazanzibar na kuto kuwauzia viazi vibovu na nyanya?, na kupata maduka na majumba kurisi hii ndio laumuhimu kwako wewe kulijuwa nyiyi ni majambazi tu na hizo ndio tabia zenu.

.........

Kweli mmepania kujitenga ama kwa shari ama heri....

Mkuu abdulahsaf , Je. Unakubalina na maazimio ya wanaUAMUSHO juu ya kuchukua pwani ya Tanzania bara/Tanganyika?

Haya ndiyo madai ya Uamsho kuuvunja Muungano
*Wasema bayana kwamba wanataka Zanzibar iwe ‘Sovereign State', ijitawale yenyewe
*Wasema Dar es Salaam ilikuwa ya Zanzibar, maili kumi kuingia ndani, mikataba ipo
*Kiongozi ahoji: Kilomita chache zinakushughulisheni wakati mna mapori tele
 
Last edited by a moderator:
Huyo Shekh ni muongo Sultani wa Zanzibar aliuza ile ten mail strip yote kwa dola ya Ujerumani kwa thamani ya paundi za uingereza 200,000/- miaka ile ya 18.. akasome upya historia
 
Hivi ninyi watanganyika mnapata nini kwenye huu muungano mpaka muutetee hivyo? Let them go, we've got nothing to loose
 
Back
Top Bottom