Mahita na nyumba ndogo: Mtoto adai babake; ye amweka ndani

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,956
22,144
Mahita amshtaki msichana anayedai ni bintiye

Na Ummy Muya

ALIYEKUWA mkuu wa Jeshi la Polisi, Inspekta Jenerali Omary Mahita amekumbwa na msukosuko mwingine baada ya binti wa miaka 15 kuibuka na kudai kuwa ni mtoto wake, jambo lililomfanya mstaafu huyo kumfikisha mahakamani kwa kosa la kuingia nyumbani kwake kijinai.

Tayari Mahita ameshashindwa katika kesi nyingine iliyofunguliwa na Rehema Shaaban, ambaye alidai kupewa mimba na mkuu huyo wa polisi na baadaye kumzaa mtoto anayejulikana kwa jina la Juma Omari Mahita. Alidai kuwa alipata ujauzito huo wakati akiwa mfanyakazi wa ndani wa Mahita.


Kesi mpya ya kamanda huyo wa zamani wa polisi mkoani Kilimanjaro ilitajwa kwa mara ya kwanza jana mbele ya Hakimu Mary Matoi kwenye Mahakama ya Mwanzo Kinondoni.


Ilidaiwa mahakamani hapo kuwa binti huyo ambaye ni mkazi wa Sanya Juu wilayani Siha mkoani Kilimanjaro alifika nyumbani kwa Mahita Oysterbay jijini Dar es Salaam na kumweleza kuwa yeye ni mwanaye aliyezaa na polisi mwenzie, Ester Lyatuu.


Karani wa mahakama hiyo, Fatuma Hatibu alimwambia Hakimu Matoi kuwa mtuhumiwa huyo aliyejitambulisha kwa jina la Sophia Mahita, alifika nyumbani kwa mkuu huyo mstaafu wa Jeshi la Polisi Machi 22 mwaka huu, majira ya saa 5:00 usiku.


Mtuhumiwa huyo alikiri kufika nyumbani kwa Mahita na kusisitiza kuwa alifanya hivyo kwa kuwa ni baba yake mzazi.


Baada ya maelezo hayo ya awali Hakimu Matoi aliahirisha kesi hiyo hadi Aprili 12 mwaka huu itakapotajwa tena huku mtuhumiwa huyo akienda rumande kwa kukosa dhamana.



TAMWA NA WENGINEO MPO JAMANI
 
Jamani sheria za nchi zinasemaje

hivi huyu baba enzi hizo za ukatili wake akukuwa na condom??ama
alipokuwa akifanya mapenzi anatarajia kutoa ""mikaaa""""?????
Mbona kila mtoto anamkataa shame na aibu yake yule wa house girl bichwa sura babake mtupu.....

Enyi mijibaba mnayofanza nje nawaambien wazi watoto hawa mungu anawapiaga mapigo sura kila kitu anazaliwa chako ukamkane mbele ya mkeo!!!!alilazimishwa kuzaa nje ama ni ile mizigo waliokuwa wakiletewa na wale maafande wa chini....jamani serikali embu sikilizeni vizuri kesi za huyu mtu...yule mama majuzi amelalamika ameshinda kesi na pesa atoi za mtoto kama alivyoamriwa ....jamani????si laaan hii alafu jitu hili hili linataka kuongoza ubunge wa morogoro...we mahita kanisa linaanzia nyumbani kwako uwezi ongoza kanisa wakati nyumbani kuchafu rekebisha kwanza ufikirie na sie tukufikirie ...
 
Nafikiri hapa tunaona tofauti za kifikra na kimaadili kati ya watu. Kuna watu kutoka sehemu fulani au makabila fulani (Mgano uchagani) huwa wanaamini kuwa kumkataa mtoto ni kosa kubwa sana. Huwa wakiachana na mwanamke kitu cha kwanza wanachong'ang'ania ni watoto. Mara nyingine hufikia hata kuwaiba watoto hao na kuwaficha kabisa. Uchagani huwa ni desturi kumpeleka mtoto huyo nyumbani na kumfanyia mila ili atambulike na familia. Tena endapo hata baba atafariki kabla hajawatambulisha, wanaowafahamu watoto hao huwaleta kwa taratibu za kimila siku ya kuvunja tanga na hufanyiwa kwanza mila kisha hunyolewa nywele pamoja na watoto wengine, na huhesabika kuwa ni watoto wa familia. Huyu mwenzetu haoni kabisa aibu kumkana (situmii kumkataa kwa makusudi) mtoto hadharani. Ni aibu sana. Labda hata watu wanaomzunguka inelekea wanashindwa kumshauri au nao wana mtizamo finyu. Kwa mtizamo wangu, hao wato wangemshauri alishukue swala hili kiusuluhishi badala ya kutumia mabavu. Au labda ndiyo mila na desturi za kwao?

Inaelekea kuwa labda anaogopa mambo fulani lakini sioni woga ambao unaweza kukufanya umkane mtoto uliyemzaa!! Ni aibu sana.
 
Here is Mahita again !!!! mbaya ni kwamba mtoto wa nje huwa anafyatuka copyright kama karunguyeye ,, hapo hukwepi kitu wallah !!!
 
hapo dna test imuumbue, kisha yeye keshakubali mtoto wake alale rumande kwa wiki nzima!
Ona aibu baba, pale ulipokuwa ukilala na wanawake ovyo ulitarajia nini?
mtoto hana makosa, kama una beef ni na mama yake mtoto sio yeye mwenyewe
 
Mtoto kaambiwa na mama yake huyo ndio babaako..sasa si amuweke mama mtu ndani?...au hakumlipa ujira wake ndio maana anamkwepa?
 
Mkware tu huyo.hana lolote.
anaona bado yupo kwenye cheo cha IGP bado???
chukua mtoto acha ulofa wewe, aaaaaghh!
 
Aagh nimeshachoka kusikia visa vya watoto wa nje wa Mahita, inaonekana mzee alikuwa bingwa wa kazi za nje.,kama kweli ni wanae awatendee haki kwa kuwakubali haina haja ya kuwaacha watoto wateseke wakati ni raha za baba yao ndio zilizowaleta duniani.
 
Kiukweli mimi namfahmu huyo dada...aliezaa na mahita na nadhani hata watu wote wa mkoa wa kilimanjaro wanamjua alikua ni trafic mjini moshi kabla ya kuhamishiwa wilayani hai...nadhani mahita na familia yake wanamfahamu huyu mtoto vizuri kabisa na kiukweli si kitu cha kujificha kwa maasakari wa moshi kwani wengi wanamjua huyo askari na mtoto wake hapa mahita ndo anaonekana kichaa kabisa
 
Back
Top Bottom