Maharusi wapuuza mbwembwe, wasafiri kwa ‘bodaboda’

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,299
33,082
MAHARUSI WAPUUZA MBWEMBWE, WASAFIRI KWA ‘BODABODA'


Maharusi hao wakiwa kwenye bodaboda baada ya kufunga ndoa.
KATIKA kile kilichoonekana kupuuza mbwembwe za harusi, maharusi wawili walioamua kufunga ndoa maeneo ya Uwanja wa Ndege katika Manispaa ya Morogoro hivi karibuni, waliamua kutumia usafiri wa pikipiki ambazo ni maarufu kama ‘Bodaboda’ na kuyapa kisogo magari ya kifahari licha ya kuwa walikuwa na uwezo wa kuyatumia.

Maharusi hao ambao majina yao hayakupatikana, walifunga ndoa yao ya Kiislam na baadaye kuanza kuelekea nyumbani maeneo ya Mawezi ambapo walitumia usafiri huo wa pikipiki ambayo ilikuwa imepambwa maalum kwa ajili yao ambapo waliwaacha watu wengi waliohudhuria wakishangaa.

Pamoja na ‘vimatatizo’ kadhaa vilivyoambatana na usafiri huo, bado shughuli yote ilifana na kuwaacha watu wengi wakipongeza hatua hiyo ya aina yake katika shughuli za kufunga ndoa.
ZIFUATAZO NI PICHA ZA TUKIO HILO:
PICHA NA DUNSTAN SHEKIDELE, /GPL, MOROGORO


1.jpg

2.jpg

IMG_2900.jpg


IMG_2901.jpg


IMG_2902.jpg

IMG_2906.jpg


IMG_2913.jpg

IMG_2918.jpg



 
Back
Top Bottom