Mahari na nafasi yake katika ndoa... Je, utamaduni huu umepitwa na wakati?

Ha Ha Ha! Kwa mpango huu bado nitakuwepo sana tu na kama vp inabidi tu kukamua maziwa toka kwajirani. Kilo sita mbona si kitoto.
Wakuu mwakani ni ndo nilitaka kupeleka mahari sasa kama mambo yatakuwa hv basi nitanyoosha mikono.

Mwambie mweziwako kuhusu cost sharing. Siku hizi mambo si kugawana majukumu? au?
 
Mahari muhimu bana, kama umependa msichana lazima utoe mahari. Iwe kwa gharama yeyote ile, nyie toeni tu msilalamike.
kutoa mahari hizo ni mila zetu wajemeni! Na mtu anayeacha mila yake ni mtumwa.

Wewe wacha kuleta vichekesho ba..he he he. Watu wanalia ukata wewe unaleta habari za mila? Mila gani huku tumbo li wazi?
 
Mimi ninavyojua mahari ni lazima kwa ajili ya kuwashukuru wazazi,
lakini siyo pesa nyingi au vitu vya gharama kama watu wanavyofanya siku hizi.
inatakiwa labda kitenge cha mama na shangazi, koti la baba, blanketi la bibi basi vitu ambavyo kila mtu ataaford, ila watu siku hizi binti akiolewa wanataka wamalize shida zao.
 
Ebwana mada imekuja wakati wake. Kuna jamaa aliamua kuendekea kuiba binti wa watu mpaka akamzalisha watoto wawili akiwa kwao sababu mahali aliyopangiwa ilikuwa kubwa. Mahali aliilipa kwa muda wa miaka 4 na wakati anamaliza tayari binti alikuwa amejifungua mtoto wa pili na bado alikuwa nyumbani.

Ndugu zangu akina mangi kwa sasa wamefanya biashara siyo siri. Mahali inatajwa vitu kibao halafu inakuwa transformed into money. Wasukuma nao hawako nyuma sana. Ndugu zetu wazaramo afadhali mahali hata laki 3 haifiki.
 
Katika ustaarabu wa Kiislam , mahali ni hidaya yaani ile mwanamke anayoitaka toka kwa mumewe mtarajiwa. Kwa maana ya kuwa ni kitu chochote ambacho mwanamke atapenda apewe na huyo mume mtarajiwa ikiwa kama hidaya ya kumsabilia mwili wake. Mahari hii kwa kiislamu ni ile tu inayotamkwa na muolewaji bila kushinikizwa wala kulazimishwa na mtu yoyote kuanzia wazazi, ndugu, jamaa au hata marafiki.

Mzazi au ndugu yoyote haruhusiwi kutamka mahali ya mtoto wake. na Mahali siku zote anapewa yule muolewaji.

Hio ni kwa mujibu wa Dini ya kiislamu
 
sasa mbona mke akikuzailia watoto wazuri: wewe unaona poa tu??

ila pesa mahari unaona shida?

Mazee tatizo sio mahari..tatizo ni mahari ya kufa mtu!

Nijuavyo mtu akitaka kuoa kama ni mwanaume kutoa mahari ni jambo linaloonesha ushababi na wengi hatuna pingamizi na utoaji mahari.Tatizo ni pale kwamba wakwe wanaweka mahari ya kufa mtu bila kujali hali halisi ya kipato cha mkwe mtarajiwa, huu ni ufidhuli unaostahili kupingwa.
 
Ndio maana manyanyaso ndani ya ndoa hayaishi nini kutoza mahari kama unauza mwanao kabisa? Asa mtoto kama huyo akipigwa na kung'olewa pua atarudi tena kwako kulalamika au akirudi kwako wewe kama mzazi utakuwa na nguvu ya kumkaribia huyo kijana alikupa milioni sita kama mahari kweli?

na bado ukishachukua mahari na mtotot kuolewa vijishida vya hapa na pale bado unategemea kwa mkwe eh!
 
Ndugu Zanguni, mimi kwa namna moja au nyingine, napinga kwa asilimia nyingi sana japo si zote,hili swala zima la mahari, kwani hii in hali ya kama kuuziana,alafu ,wisho wa siku,mke huyo ninayeuziwa tulikutana na kuimbishana kisha kuelewana wenyewe, kwanini tunapokuja kuomba idhini ya wazazi ndio tuanze kukomoana?

mimi nataka niwasapoti kwa kiasi kikubwa ndugu zangu wa kiislam, ambao mwanamke ndiye anayeamua, mahari,kwa kuwa kwa Jinsi hii sis ambao bado tupotupo sana haitawatisha.ila kwa wenzangu na mimi wa kikristo tunamsala.

Angalia Wahindi wao Mwanamke ndiye anayetoa Mahari(Ambayo hatuwezi tukaiita mahari. bali ni sehemu ya urithi wake katika familia ambayo wazazi wake wana;pa aende nayo kule anakokwendem na kwa kuwa kiongozi wake kule atakuwa ni mumewe basi yeye ndiye hupewa ile mali akatunze kwa ajili ya yule binti) ambayo naona kwangu inaleta maana,ila hizi milioni sita sita wanazotogonga nazom ndio maana vijana wanaamua kuingia mitini na wengine wanajichukulia tu kienyeji (cohibiting)

Kwa ndugu wangu ambao bado tupo tupo kwanza tunakazi kubwa.
 
Mi ningekuwa na uwezo ningeabolish hii kitu inaitwa mahari! ndugu zetu Waislam walijua kuna watu watatia ufisadi ndo maana wakasema mahari inatamkwa na mwolewaji tu!
 
Ndugu Zanguni, mimi kwa namna moja au nyingine, napinga kwa asilimia nyingi sana japo si zote,hili swala zima la mahari, kwani hii in hali ya kama kuuziana,alafu ,wisho wa siku,mke huyo ninayeuziwa tulikutana na kuimbishana kisha kuelewana wenyewe, kwanini tunapokuja kuomba idhini ya wazazi ndio tuanze kukomoana?

mimi nataka niwasapoti kwa kiasi kikubwa ndugu zangu wa kiislam, ambao mwanamke ndiye anayeamua, mahari,kwa kuwa kwa Jinsi hii sis ambao bado tupotupo sana haitawatisha.ila kwa wenzangu na mimi wa kikristo tunamsala.

Angalia Wahindi wao Mwanamke ndiye anayetoa Mahari(Ambayo hatuwezi tukaiita mahari. bali ni sehemu ya urithi wake katika familia ambayo wazazi wake wana;pa aende nayo kule anakokwendem na kwa kuwa kiongozi wake kule atakuwa ni mumewe basi yeye ndiye hupewa ile mali akatunze kwa ajili ya yule binti) ambayo naona kwangu inaleta maana,ila hizi milioni sita sita wanazotogonga nazom ndio maana vijana wanaamua kuingia mitini na wengine wanajichukulia tu kienyeji (cohibiting)

Kwa ndugu wangu ambao bado tupo tupo kwanza tunakazi kubwa.
Mahari inatolewa kutegemea na mila za watu na dini. Kwa mila nyingi za waafrika mahari inapangwa kwenye vikao vya koo za kijana wa kiume na wa kike. Baadaye inalipwa kwa wazazi wa binti.

Kidini (upande wa wakristo) mahari inatolewa kwa wazazi kama shukrani kwa malezi ya binti. Kumbe haipaswi kuwa na sura ya udalali kana kwamba kuna kuuziana bidhaa fulani. Kijana wa kiume anapaswa kutoa chochote alichonacho kwa wazazi.

Shida kwa sasa watu wamewafanya mabinti zao mtaji. Wamewekeza. Wanataka kupata faida. Hapa ndipo penye shida. Wapanga mahari unakuta wanalumbana kiudalalidalali. Kunahitajika elimu hapa! Na mara nyingi kwenye kupanga mahari wanaangalia sana hali ya familia ya mchumba wa kiume. Kama hali yao kiuchumi ni nzuri basi na mahari inakuwa juu. Kama ni hali ya chini, vivyo hivo.

Hata hivyo ushauri wa bure:
Kama mahari (fedha/vitu) unavyo, mi naona afadhali utoe. Fedha ni nini mbele ya Upendo?! Kama binti umempenda haswa na kakuingia mifupani na damuni, na mahari kamili unayo sioni kwa nini ulalamike. Ukiwa unampenda utatoa kiasi chochote unachodaiwa, tena kwa moyo radhi na bia kunung'unika. Tena unaweza pia kuongezea. Ujue kutoa mahari kubwa pia ni alama inayoonekana kwa nje kwamba UNAMPENDA na KUMTHAMINI huyo wife to be. Na mara nyingi watoto wa kike hufarijika sana wazazi wao wanapopokea mahari kubwa kutoka kwa wachumba zao.
 
Mahari muhimu bana, kama umependa msichana lazima utoe mahari. Iwe kwa gharama yeyote ile, nyie toeni tu msilalamike.
kutoa mahari hizo ni mila zetu wajemeni! Na mtu anayeacha mila yake ni mtumwa.


Kama ni kupendana ,tufike mahali na mabinti watoe mahali kwa wavulana kama wahindi.
mwenye wasichana kumi,atakuwa tajiri hapa bongo ila tatizo nim kuwa siku hizi kuolewa kwa mabinti ikiwa isssue
 
...unapokata bima si chaguo lako iwe comprehensive, third party fire and theft, au third party pekee? hivyo hivyo kwenye mahari. Mtoto wa watu huyo, sio unamchukua kwenda kumchezea siku mbili tatu, mara unamrudisha kwao...

'Akili kumkichwe!'
 
hehehe..kazi kweli kweli. Ila sasa kwa uelewa wangu nafikiri sasa hivi inakuwa kama kukomoana ingawa naona kama taratibu za kimila sasa hivi zinaishiwa nguvu hasa kwenye hili suala maana nakumbuka kuna sehemu jamaa yangu alikwenda kuoa, mwanamke (Mke mtarajiwa) ndiye aliyetaja mahari na mambo yakaenda sawa kabisa ila sasa kama ndio unakwenda kuoa halafu maamuzi yanatoka kwenye vikaoo vya ukooo mzima hapo lazima mwana uende na hela ya kutosha maana lazima utakutana na bei za Supermarket


Hii nimeipenda mkuu!
 
Mahari muhimu bana, kama umependa msichana lazima utoe mahari. Iwe kwa gharama yeyote ile, nyie toeni tu msilalamike.
kutoa mahari hizo ni mila zetu wajemeni! Na mtu anayeacha mila yake ni mtumwa.
Wewe Pretty nakuambia hata kama nimekupenda vipi mkipanga mahari 6,000,000 kwa kweli hatutaoana. Wewe hela zote hizo mnataka kununua Fuso nini!
 
Hata hivyo ushauri wa bure: kama mahari (fedha/vitu) unavyo, mi naona afadhali utoe. Fedha ni nini mbele ya Upendo?! Kama binti umempenda haswa na kakuingia mifupani na damuni, na mahari kamili unayo sioni kwa nini ulalamike. Ukiwa unampenda utatoa kiasi chochote unachodaiwa, tena kwa moyo radhi na bia kunung'unika. Tena unaweza pia kuongezea. Ujue kutoa mahari kubwa pia ni alama inayoonekana kwa nje kwamba UNAMPENDA na KUMTHAMINI huyo wife to be. Na mara nyingi watoto wa kike hufarijika sana wazazi wao wanapopokea mahari kubwa kutoka kwa wachumba zao.

Ni wazi kuwa mwanamke (kama mwanaume) ana thamani kubwa kuliko mahari yoyote ile. Kamwe mahari haiwezi kuwa kipimo cha upendo.

Kwa maoni yangu mahari inamdhalilisha mwanamke.Inamfanya awe 'object of trade'. Hawezi mwisho wa siku kuwa mwenza katika familia mpya bali atakuwa 'kifaa kilichonunuliwa' kwa kazi maalumu(eg kuzaa - asipozaa anaweza kuachwa au kifaa kngine kutafutwa!). Mara kadhaa watu wamekuwa wakijaribu kutafuta visababu vya kuendelea 'kutoza' mahari lakini kimsingi ni 'kumuuza' binti kwa ukoo wa mwanaume kitu ambacho hakiwatendei haki wanawake (pamoja na kuwa wengi wa wanawake -hata hapa JF!- bado wanaamini katika mahari).

Mahari haipaswi kuwapo. Kama ni shukrani, pande zote mbili zimehusika katika malezi ya vijana wao hivyo sioni ni kwa nini upande mmoja tu uushukuru upande mwingine tena kwa kutoa mali.

Nafasi ya mwanamke katika ndoa, itaendelea kuwa chini kama mila kama za mahari zitaendelea kuwapo. Haiwezekani 'aliyenunua' na 'aliyenunuliwa' wawe na haki sawa katika ndoa.
 
Hizi mahari ndio unakuta baba anapanga yake, mama naye anataka vitenge na mashangazi nao utasikia tulisaidia kumlea tunataka hiki na kile.
Inakuwa kama biashara ya utumwa mamboleo bana.
 
Back
Top Bottom