Mahari na nafasi yake katika ndoa... Je, utamaduni huu umepitwa na wakati?

Kunabinti niliskia yuko Hanimuni, hv ni binti ya mzee nani vilee... Kama sikosei anaitwa Cant......
 
Huyu jamaa ana ka-Vitz ka-rangi ya PINK, kwani kanaweza kuwa na thamani gani?
Nikipata thamani yake naweza kufanya MAGAZIJUTO, nipate thamani ya MRABAHA wangu

kama anakavitz sio mbaya akitoa 500,000.00 itamtosha sana na kuku mweusi wa kienyeji..
 
Bwana Yesu Asifiwe wapendwa.
Juzi kati mimi na jamaa yangu (bwana harusi mtarajiwa) tulienda mkoa fulani kwa wazazi wa mke wake mtarajiwa kwa ajili ya kujitambulisha pamoja na kupangiwa mahari, Baada ya utambulisho ilibaki kazi ya mshenga na wakwe kupangiana mahari.

Mshenga alipewa barua iliyokuwa imeandikwa hivi:

MAKUBALIANO YA MAHARI LEO TAREHE (...........)

1. Barua.........................15,000/=
2. Mzee sina miwani .........10,000/=
3. Ngoma ya Bibi...............10,000/=
4. Kifuata Barua................15,000/=
5. Mkaja.........................400,000/=
6. Mama sina nguo.............40,000/=
7. Shuka mbili....................40,000/=
8. Blanketi.........................40,000/=
9. Wajomba.......................50,000/=
10. Mahari........................900,000/=

JUMLA.........1,520,000/= Bila ya kuomba heri

Hivyo basi mpaka leo hii bado tunaitafakari hii mahari.
Ndugu wanaJF hivi siku hizi kuoa nako ni biashara??????
Pia tunomba kujua ni kabila gani hapa TZ ambalo halina gharama kama hizi, maana jamaa hapa kashindwa na yuko tayari kubadili maamuzi, Hali ni ngumu wapendwa.

Taja kabila na bajeti yake.
 
Mjomba poleni, lakini tukumbuke kuwa mila na desturi za kiafrika unapotaka kuoa lazima upangiwe mahari. Kulipa mahari ni kiashiria kwamba umejali mchango mkubwa wa wazazi kumlea binti ukamkuta katika umri, afya na tabia ulizoridhika nazo. Hata hivyo sio wote tunaoweza kukabili kiwango cha mahari kinachopangwa na mahari huwa hatuombi punguzo ila tunatoa kiasi tulicho nacho na unaruhusiwa kuendelea na masuala ya ndoa iwe ya kimila au ya kidini.

Hivyo ndugu yangu muambie muoaji ajiandae kwa kiwango alicho nacho, pelekeni na muahidi kumalizia mpatapo, maana hakuna anayemzuia binti yake kwa sababu eti mahari haijakamilika na hakuna anayepelekwa mahakamani eti kwa sababu hamalizii mahari.

Kila la heri
 
Mahari iko negotiable KAMA sijakosea...maana hii ilimtokea mshkaji ila aliishia kutoa posa na kusepa tu....
..mkaja ni nini kwanza
 
Mjomba poleni, lakini tukumbuke kuwa mila na desturi za kiafrika unapotaka kuoa lazima upangiwe mahari. Kulipa mahari ni kiashiria kwamba umejali mchango mkubwa wa wazazi kumlea binti ukamkuta katika umri, afya na tabia ulizoridhika nazo. Hata hivyo sio wote tunaoweza kukabili kiwango cha mahari kinachopangwa na mahari huwa hatuombi punguzo ila tunatoa kiasi tulicho nacho na unaruhusiwa kuendelea na masuala ya ndoa iwe ya kimila au ya kidini.

Hivyo ndugu yangu muambie muoaji ajiandae kwa kiwango alicho nacho, pelekeni na muahidi kumalizia mpatapo, maana hakuna anayemzuia binti yake kwa sababu eti mahari haijakamilika na hakuna anayepelekwa mahakamani eti kwa sababu hamalizii mahari.

Kila la heri
Mpendwa! nakushukuru kwa ushauri wako mzuri ila yote hayo tuliyafanya bila mafanikio.

Yaani tumechoka basi tu.
 
siku hizi ulipaji wa mahari nahisi unategemea demand and supply na mfumko wa bei pia manaake kuna mahari nyingine mmh! utatamani ughaili na huko kuoa..inakuwa kama ni kukomoana
 
kuna jamaa yangu mmoja alinidokeza kuwa akikumbuka mahari aliyotoa kwa mkewe, humrukia kwa hasira kama simba aliyejeruhiwa kum-do kwa sababbu mahari yake inamuuma sana!!!!!!

nafikiri kwa isingizio hiki, wanawake wengi wenye visirani wamebakwa sana na wame zao!!!!!!!!!!!
Inahitajika mjadala wa hizi mahari kwa undani zaidi, maana zinaumiza pande zote mbili.
 
naona sasa mnataka kusema wadada watoe mahar kwa wakaka/mwanaune!haipo hiyooo hii tamadun haita kuja potea hata!
 
Jamii nyingi za kiafrika wanaume tunalipa mahari, japo huwa najiuliza je ni shukrani kwa wazazi wa binti kumnunua binti au ni mwendelezo tu wa vizazi vilivyopita.

Ajabu zaidi baadhi ya familia hutegemea mahari ndiyo iwe kama mtaji au mali ya kuikomboa familia nini haswaa maana na umuhimu wake kwanini tusioane bure tu kwa maridhiano.
 
Mahari kwa miaka ya hivi karibuni yamekuwa juu sana. Sijui kama ntaoa kwa mahari.
 
Back
Top Bottom