Mahari na nafasi yake katika ndoa... Je, utamaduni huu umepitwa na wakati?

mmaroroi

JF-Expert Member
May 8, 2008
2,960
544
Kumekuwa na kawaida ya kulipa mahari wakati wa kuoa. Mahari hiyo hulipwa na mwanaume kwa mujibu wa tamaduni za kiafrika.

Ulipaji huu wa mahari hufanya ionekane kuwa mwanamke ananunuliwa.

Sasa si imefika muda ambapo utaratibu huu unafaa uachwe?

Nawasilisha.
 
.......hapa tunahitaji wazee watoe background kidogo chimbuko la hiki kitu. Anyway, binafsi sina tabu na dhana nzima ya utoaji maali. Lakini naichukulia kama unyonyaji kwa upande wa mtoto wa kiume na udhalilishaji kwa mtoto wa kike.

Binafsi naona wazazi wa pande mbili walipaswa kuwachangiwa vijana wao waanze maisha/wajijenge. Hakuna sababu kwa mzazi ambaye alikuwa na muda wakujiimarisha kimaisha kutaka pesa au rasilimali maka maali toka kwa kijana wa kiume ili kumuoa bintie.

Sijui wengine wanasemaje binafsi naone wanandoa wanapaswa kuchangiwa na wazazi wote na sio mwanaume kutoa pesa kwa mzazi wa binti
 
Ni sehemu ya utamaduni wetu!

Kila watu wana tamaduni zao- Wachina, Wahindi, Wazungu n.k

Na sisi Watz pia tuna tamaduni zetu!
 
Mmaroroi!

Kutoa mahari ni heshima fulani kwa wazazi wa mwanamke anayeposwa yaani shukrani kutokana na matunzo mazuri ya mtoto. Siku hizi mahari inatafsiriwa vingine ambavyo si kweli ila kutokana na mienendo ya ndoa kadhaa inakuwa hivyo.

Na kwasababu ni utamaduni wetu,kuacha ni haitawezekana. Suala la mahari ni zuri na liendelee tu kwenye jamii. Na kwa muoaji/muolewaji wanafurahia zaidi kuona mila imedumishwa na wazee wanabariki kwa kutoa/kukubali mahari!..
 
ukisema matunzo mazuri ya mtoto wa kike ilikuwa zamani wakati wewe mwanaume unachaguliwa mke. ila sasa hivi watu mnakutana wenye mnatongozana wenyewe na wazazi wanakuwa hawapo. sasa sijui ni matunzo gani wakati anakuwa anatongozwa huko nje akitafuta mchumba.
 
Ingekuwa mambo haya wanafanya wazungu wewe binasfi ungesema kuwa ndio mabo ya kileo lakini kwakuwa yanafanyika hapa afrika na sehemu nyingine za kiarabu katika macho yako hayafai; ni vyema endelea hivyo hivyo lakini kumbuka hata siku moja hutoona mzungu kuiga lolote lile ambao muafrika analifanya.

Hapa ndio tunarudi kule kule tulikotoka hivi umelifikiria suala la kutahiriwa kwani wazungu wengi hawatahiriwii na kuna baadhi ya wafrika vile vile lakini hapa Tanzania karibu watu wengi hutahiriwa namainisha wanaume sasa hilo unalionaje wewe?
 
Kiislamu mahari ni moja ya masharti manne ya ndoa mbayo mojawapo lisipotimia ndoa inakuwa batili.

Kiislamu mahari inatajwa na mke mtarajiwa na yeye ndiye alipwaye na ndiye mmilki siyo mzazi. Mzazi ni mpokeaji tu.

Kiislamu mahari si lazima iwe pesa nyingi na wala si lazima iwe pesa kabisa. Hii ni hidaya kutoka kwa mume mtarajiwa kwenda kwa mke mtarajiwa.

Kimila sijui.
 
Mmaroroi!
Kutoa mahari ni heshima fulani kwa wazazi wa mwanamke anayeposwa yaani shukrani kutokana na matunzo mazuri ya mtoto. Siku hizi mahari inatafsiriwa vingine ambavyo si kweli ila kutokana na mienendo ya ndoa kadhaa inakuwa hivyo.
Na kwasababu ni utamaduni wetu,kuacha ni haitawezekana. Suala la mahari ni zuri na liendelee tu kwenye jamii. Na kwa muoaji/muolewaji wanafurahia zaidi kuona mila imedumishwa na wazee wanabariki kwa kutoa/kukubali mahari!..

Je, Wazazi wa mwanaume nao hawastahili kupata 'shukrani' kwa matunzo mazuri ya mtoto wao kwa kuwa wamempa malezi mazuri, ana elimu nzuri, hakuwa muuza/mtumiaji unga n.k.? Je, kuna haya ya kuwa na kiwango maalum cha mahari maana utasikia wengine wanatakiwa watoe mpaka laki 5 au zaidi na ilhali kiwango hicho ni kikubwa mno kwa muoaji na wazazi wake?
 
Mahari kwa kweli ni lazima kwa utamaduni wetu, na inaleta heshima kwa msichana.
Sema kuna baadhi ya wazazi sasa wanakomoa kweli, utakuta wanataja kiasi cha juu cha pesa kama wanauza ambapo haipendezi. Swala hili lipo la mtoto wa kike kutolewa mahari toka enzi za Ibrahim bible inasema. Hivyo lina umuhimu wake.
 
Kumekuwa na kawaida ya kulipa mahari wakati wa kuoa,mahari hiyo hulipwa na mwanaume kwa mujibu wa tamaduni za kiafrika.Ulipaji huu wa mahari hufanya ionekane kuwa mwanamke ananunuliwa,sasa si imefika muda ambapo utaratibu huu unafaa uachwe?

Nawasilisha.

utaratibu wa mahali hautiliwi mkazo katika sheria ya ndoa ya mwaka 1971 hivy umuhimu wake bado haupo na ndoa itaendelea kuwepo hata kama hata bila mahali ili mradi tu makubaliano kati ya wanaooana yawepo.
 
Kwa tamnaduni nyingi za kiafrika, hususani zile zenye mfumo dume, mwanamke hana/hakuwa na tofauti sana na bidhaa au resource nyingine. Ukoo wa mwanaume 'unanunua' mwanamke kutoka ukoo wa mwanamke kwa ajili ya kufanya kazi na kuzaa watoto ili kuongeza ukoo wa mwanaume.

Baada ya ukoo wa mwanaume kutoa mahari na ukoo wa mwanamke kuikubali na kuipokea, mwanamke anakuwa mali halali ya ukoo wa mwanaume. Ndio maana hata mwanaume akifa mwanamke alikuwa anarithiwa (kama mali nyingine!) ili kama bado kijana aendelee kuongeza ukoo pamoja na kufanya kazi. Hawezi kuolewa na mwanaume kutoka ukoo mwingine (kama ilivyo mali nyingine haziwezi kurithiwa na watu baki!).

Mambo haya kwa sehemu kubwa yamepitwa na wakati. Dhana ya mahari imebadilika sana (ingawa bado haijesha!) na kwa koo nyingi imebaki kuwa ni symbolic/gesture tu. Koo nyingi hazisisitizi tena mahari (inaweza kutajwa tu lakini ikalipwa robo tu au chini ya hapo!) kama prerequisite ya watoto wao kukaa pamoja. kuna mwanaume mmoja yeye aliambiwa apeleke senti tano (the physical brown coin!) kama mahari!

Dhana ya 'kuoa' pia inapungua na tunaelekea zaidi kwenye 'kuoana'! Lakini bado kwa sehemu kubwa mwanamke anahamia (anaolewa) ukoo wa mwanaume (wengine bado wabadilisha hata surname!). Bado mke akifa anazikwa kiumeni na si kwao.

Koo nyingi zimeacha kurithi wajane na watoto. Kwa upande mmoja hili ni zuri lakini kwa upande mwingine kwa kiasi limechangia ongezeko la watoto wa mitaani. Dhana ya collective responsibility katika ukoo inaondoka.

Kwa maoni yangu, utaratibu wa mahari utaondoka wenyewe (kwa wasio waislam!) kwa sababu itafika kipindi wahusika hawataona umuhimu tena. Uamuzi na taratibu za kuoa/kuolewa halitakuwa suala la ukoo tena bali familia na baadae mtu binafsi!
 
ukisema matunzo mazuri ya mtoto wa kike ilikuwa zamani wakati wewe mwanaume unachaguliwa mke. ila sasa hivi watu mnakutana wenye mnatongozana wenyewe na wazazi wanakuwa hawapo. sasa sijui ni matunzo gani wakati anakuwa anatongozwa huko nje akitafuta mchumba.

Ni kweli mambo yamebadilika siku hizi ila bado tunadumisha na kuendeleza mila zile zile!..
 
Je, Wazazi wa mwanaume nao hawastahili kupata 'shukrani' kwa matunzo mazuri ya mtoto wao kwa kuwa wamempa malezi mazuri, ana elimu nzuri, hakuwa muuza/mtumiaji unga n.k.? Je, kuna haya ya kuwa na kiwango maalum cha mahari maana utasikia wengine wanatakiwa watoe mpaka laki 5 au zaidi na ilhali kiwango hicho ni kikubwa mno kwa muoaji na wazazi wake?

Kwa Tanzania wengine tumezaliwa na mpaka sasa tunaona utaratibu wa kimila wa kutolewa mahari kwa mwanamke, sijui kwa nini wanaume hawatolewi mahari!
Halafu hiyo ya kutoa hela tena kubwa hivyo sijui makubaliano yanakuwaje kati ya upande wa muoaji na muolewaji. Labda mahari inaweza kuwa ng'ombe kwa sababu wote wako mjini kimaisha wanaona wa-convert kwenye hela mambo yaishe haraka na shughuli ifanyike.
Zamani ukitaka kuoa unaenda mpaka kijijini kwa mwanamke kujitambulisha na kujua mwenzio asili yake, siku hizi mnachukuana tu hata msipoenda sawa kwa wengine! Mambo yamebadilika...
 
...
Zamani ukitaka kuoa unaenda mpaka kijijini kwa mwanamke kujitambulisha na kujua mwenzio asili yake, siku hizi mnachukuana tu hata msipoenda sawa kwa wengine! Mambo yamebadilika...

...Vice versa, siku hizi wenywe wenyewe mnachukuana, mnaishi kinyumba, mnazaa mtoto wa kwanza, wa pili,...then mnakwenda kuonyeshana asili ya mlipotoka na kuwatambulisha wajukuu kwa mababu na bibi zao, kisha mnaoana.
 
utaratibu wa mahali hautiliwi mkazo katika sheria ya ndoa ya mwaka 1971 hivy umuhimu wake bado haupo na ndoa itaendelea kuwepo hata kama hata bila mahali ili mradi tu makubaliano kati ya wanaooana yawepo.

Balingilaki ni sheria gani hiyo ambayo umeiquote?
 
mahari ni shukrani kwa wazazi tu basi na siyo hela inaweza kuwa kitu chochote ambacho wazazi watabaki nacho kama kumbukumbu.
Sema siku hizi watu wamefany mtaji eti mtu anaambiwa mahari milioni moja, ngombe wanne wanaotembea , vitenge doti ishirini hapo kuan ndoa kweli au biashara
 
Je, Wazazi wa mwanaume nao hawastahili kupata 'shukrani' kwa matunzo mazuri ya mtoto wao kwa kuwa wamempa malezi mazuri, ana elimu nzuri, hakuwa muuza/mtumiaji unga n.k.? Je, kuna haya ya kuwa na kiwango maalum cha mahari maana utasikia wengine wanatakiwa watoe mpaka laki 5 au zaidi na ilhali kiwango hicho ni kikubwa mno kwa muoaji na wazazi wake?
Ni kweli Mtoto wa Kiume anatunzwa kama alivyo wa kike.Mahari inawafanya baadhi ya Wazazi wasitake Watoto wao waolewe na watu wa kipato cha chini.Kwanini Wazazi wasiwachangie watoto wao kiazia maisha badala ya upande mmoja kudai mahari.
 
Back
Top Bottom