Mahari milioni 5

zayat

JF-Expert Member
Dec 29, 2010
337
42
Jamaa aliposa msichana hajawahi kuguswa na mwanamume Akaambiwa mahari milioni 5.
AKASEMA KWA MSHAHANGO>Hee milioni 5?Wakati hapo jirani nimeambiwa laki 2 tu tena MWANAMKE MWENYEWE ANA MIMBA (BUY 1 GET 1 FREE)
 
Ahahah! Nadhani mdau alifananisha na mfugo mfano bei ya mbuzi au ng'ombe mwenye mimba ni kubwa kuliko asiye na mimba
 
Hahahahaa hii kali kuliko.


Afu hajatulia huyo moaji manake antaka kuchumbia huku na huku
 
Kweli hiyo kali,

Ila mi sishangai sana hapa kwetu tz. wazazi wamekuwa na tabia ya kupiga hesabu ya gharama walizotumia kwa mabinti zao na kufanya zilipwe wakati wa mahali. Nadhani ndo maana hata ukandamizaji kwa wanawake hauishi na mfumo dume ndo unazidi kukua ingawa wanawake wanakimbilia mikutanoni Beijing.

Wazazi wabadilike ili kuimarisha usawa wa kibinadam.
leo mahari hadi M10! utafikiri unamnunua mtu. Ndo maana wanawake wananyanyaswa maana wanaume wanaumia wakiwazia mahari na zawadi wanazotoa kwa wenziwao.hasa ndugu wa mwananmke wanapoendelea kumiminika kwa jamaa ili wasaidiwe wakati jamaa alichajiwa mahali kibao.
 
rafiki that is true.huko india madhehebu ya kihindu mwanamke anatoa mahari,unachukuliwa mzani mkubwa mwanaume anakaa upande 1 upande wa 2 familia ya kike wana jaza mali
 
Hii imekuwa kinyume na jamaa aliyekwenda kuchumbua mwanamke aliyeachika , akatajiwa mahari kubwaa zaidi ya 5mil, alipouliza sababu akajibiwa, Huyu anauzoefu mkubwa sana wa ndoa kwa hiyo kutokana na uzoefu wake inabidi mahari iwe kubwa teh teh.... teh
 
Back
Top Bottom