Maharage ya kopo yamuumbua sista do

charger

JF-Expert Member
Nov 21, 2010
2,320
1,369
Sista do mmoja alikuwa anapenda sana maharage ya kopo(baked beans)shida ilikuwa kila akiyala baada ya muda anaharibu atmosphere vibaya mno.Sasa ikafika point kapata mchumba aliyempenda sana na jamaa akaahidi kumwoa. Sista do kwakuwa alimpenda jamaa na hakutaka kumsumbua kwa katizo la hewa  pindiwanapokuwa pamoja akaamua kuacha kabisa kula  baked beans.

Wameshaoana sasa,siku moja sista do anarudi toka kazini gari lake likaharibika wakati akirudi home.Ni mbali kidogo na home.Akaamua kumpigia simu mumewe kwamba amepata tatizo hivyo atachelewa kidogo kurudi kwani anatembea kwa mguu.

Akiwa njiani kapita restaurant flani harufu nzuri ya baked beans ikamvutia,akasema potelea pote  I'm  craving ngoja nikale kidogo by the time nafika home mambo yatakua yameshakaa sawa.Pale restaurant kastukia kapiga kopo 3 za baked beans.Kaendelea na safari yake kurudi home huku anapiga vi shot range misile kidogo kidogo.

Ile anaingia tu home mmewake kamkaribisha kwa bashasha na kumziba kitambaa usoni akamwambia amemwandalia zawadi nzuuuri ya dinner.Akamshika mkono kumpeleka dinning.Akamfikisha kwenye kiti.Kabla hawajaendelea simu ya mme ikaita chumbani,mme akamwomba radhi sista do"Darling nakuja sasa hivi usifungue macho please" Sista do tumbo linavuruga akaona amepata ka mwanya afanye mambo yake kabla mme wake hajarudi.Kanyanyua ta...** moja kashusha fataki la kimyakimya,chumba chote ikawa kama  samaki mbichi kasahaulika kwenye frizer halafu umeme ukatike kwa siku 3.Sista do katoa leso kapungapunga kurekebisha mazingira huku anasikiliza maongezi ya simu ambayo yalionekana ni marefu.

Sista do mara tena likaja fataki jingine akaachia  then akapunga na kaleso,likaja la 3 hivohivo.Mara jamaa kamaliza kuongea akarudi."Darling I hope hujajifunua"sista do"yes hny" Ikafika saa ya kufunguliwa kitambaa,guess what happened? Meza imejaa wageni 12 wamekuja kumpongeza kwa birthday yake.
 
Hahahaha, hii imenianzia vyema siku yangu! ONYO KALI KWA WAPIGA MIZINGA: ANGALIA MAZINGIRA KABLA HUJAFYATUA.
Hii hadithi inanikumbusha movi moja ya bongo, jina nimesahau, kuna yule jamaa anacheza kiduku saa zote. Tafauti ni kuwa kwenye muvi mpiga mizinga alikuwa mume na aliyekuwemo chumbani alikuwa mwamamkwe
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom