Elections 2010 MAHANGA umewafanyia nini jimbo lako la Ukonga

Maoni yangu mimi ni kuwa mara nyingi tunategemea tuanowachagua watufanyie mambo ya maendeleo na kwa bahati mbaya wagombea nao kwa kufahamu hilo nao huahidi mambo ambayo mengine ni vigumu kutekelezeka kama haimo kwenye mipango ya maendeleo serikalini.
Hivi hatuoni kuwa wakati umefika badala ya kutegemea na kulaumu viongozi tukajiuliza tumefanyia nini jamii zetu [sehemu tunazoishi], jee ni kweli tunashiriki kama wadau au tunakaa tukingojea neema toka kwa wabunge?????
Uzefue unaonyesha kuwa wapiga kura [majimboni hasa vijijini]wanapokuwa wadau wa maendeleo kwa kuchangia aidha nguvu zao au uwezo wao kwa pamoja husonga mbele zaidi ya watu wa mijini ambao tunangoja hata mapipa ya taka zetu wenyewe tuwekewe na city na hata hivyo wengine kugoma hata kulipia huduma hizo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom