Profesa Costa Mahalu aibwaga serikali kortini

Tatizo Mahakama za Tanzania hazipo huru, wakubwa wanapopenda wanachakachua hukumu na mahakama zinabaki kukubali matokeo. Hii ndio Tanzania.
 
Mimi nampongeza Mahalu mnyongeni lakini mpe haki Yake. Hongera Mahalu achana na chuki binafsi za kikwete. Mbona Rostam anatembea mitaani baada ya kuhujumu uchumi na Kagoda yake, ebo!
 
Serikali kushindwa kesi mahakamani ina uhusiano gani na serikali ya awamu ya nne, tatu, pili au kwanza!?

kwani wanaokwenda mahakamani ku-defend case kwa niaba ya serikali ni Wanasiasa au Watalaam ambao ni waajiriwa kwa mujibu wa sheria na si kwamba kila awamu ikiingia madarakani inafukuza watumishi wote wa Umma na kuajiri wapya!? Hiyo inaweza kuwa indicator ya tatizo serikani lakini haliwezi kuainishwa moja kwa moja kuwa ni tatizo la awamu ya fulani, labda kama kuna hoja yuma ya advocacy kuwa hiyo awamu ilitoa ajira kwa un-competent personnel ambao ndio pia upewa kazi ya kusimamia kesi za seriakili husani kwa ushahidi kwa kesi husika zilizoshindwa.

Nakiri tatizo lipo lakini siyo la awamu ya utawala.
 
Halafu kuna watu(hapa Njb Kaskazini) wanataka eti wachague mtu aliyeishia darasa la nne(ingawa anatudanganya kafika la saba) awe mbunge wasijue kabisa kuwa hatakuwa na mchango wowote zaidi ya kupigia kura miswada kwa minajili ya kuvutia upande wao.
Kukiwa na wabunge mambumbumbu watawezaje kujadili miswada nyeti kama hii wakati wengine hawajui kusoma wala kuandika,na wengine wanaingizwa bungeni ili kulinda maslahi ya chama,na hawathubutu kujikita kwenye kujadili mambo yenye manufaa kitaifa.

Mkuu
Hata hao walio na vidato, degree nyingi kuliko thermometer walilolifanya ni lipi?
Tunao wabunge ambao wamekuwa mzigo kwa walipa kodi kwani hawajui wanapaswa wafanye nini huko bungeni.
Wengine wanadhani wametumwa ili kulinda masilahi ya vyama vilivyo wateua na kisha wananchi tukapiga mhuri.

Na pia tusisahau kuwa sahani za ubwabwa na pombe kidogo tunayopewa siku moja inagharimu miaka 5 ya kuhangaika.
hivyo basi nadhani matatizo yapo pande zote,wale wasomi hawana wanalolifanya ni sawa tu na huyo darasa la saba.
Japo kuwa darasa la saba hasa la sasa nadhani darasa la kwanza la miaka ya nyuma anamzidi uelewa.
 
Ndiyo kawaida ya serikali ya awamu ya nne inabwagwa kila sehemu. Tatizo ni kuwa kila jambo inafanya pupa tu kwa lengo la ku-win mass kwamba inapelekwa hata vigogo mahakamani kama jk anavyozungumza majukwaani.

Hata suala la mgombea binafsi lilifanywa kwa jazba tu. JK afahamu kuwa uongozi wake una dalili zote za kupwaya angeachia ngazi mapema huenda tungempatia heshima kubwa kuliko hivi sasa. Dr. Slaa akishinda urais, tumtarushia JK vilago vyake aende Chalinze.

Duh, kumbe bado una ndoto tu za Slaa kuchukua nchi hii mkuu ? hii nchi haichukuliwi kwa ww kwenda kutumbukiza tu kikaratsi
 
Duh, kumbe bado una ndoto tu za Slaa kuchukua nchi hii mkuu ? hii nchi haichukuliwi kwa ww kwenda kutumbukiza tu kikaratsi

nimekusoma dada/kaka! Ndio maana jamaa akachukua nchi japo tulitumbukiza karatasi zilizokuwa vema kwa mwenzake!
 
Kesi hii ilifunguliwa kwa shinikizo la kikwete kutaka kumkomoa mzee huyu aliyekuwa mwadilifu katika utumishi wake akiwa balozi italy.Walitaka kumuingiza katika ufisadi wa kutafuta pesa za kampeni 2005 akawatolea nje. Wakaamua kumkomoa lakini mwisho wa siku serikali hoi.Ndugu zake wasukuma wanahasira sana na ****** watammalizia kwenye sanduku la kura mwaka huu.

Prof. Mahalu alikuwa mwadilifu kazini? Haya mkuu, I hope unaelewa maana ya uadilifu.

Prof. Mahalu alikuwa mtu mzuri akiwa dean UDSM. Baada ya kuingia wizara ya elimu kuwa mkurugenzi wa elimu ya juu, madudu yalianza mengi mno. Scholarships za ngono, fedha nk.

Alipokuwa msaidizi wa balozi kule Ujerumani ikawa ni balaa tupu. Na alipoenda Italy, akafanya forgery ya kijinga kama hana elimu. Hata huyo anayeshitakiwa naye, alikuwa anatembea naye wakati anajua maadili yanakataza.

Lakini kwa Tanzania ya wajinga atashinda case yake na kuendelea kutanua mitaani.
 
<b><font color="purple">Duh, kumbe bado una ndoto tu za Slaa kuchukua nchi hii mkuu ? hii nchi haichukuliwi kwa ww kwenda kutumbukiza tu kikaratsi</font></b>
<br />
<br />


Duh! Huu ujumbe ni mkali sana; kama karatasi imegoma basi tutegemee makubwa
 
Duh, kumbe bado una ndoto tu za Slaa kuchukua nchi hii mkuu ? hii nchi haichukuliwi kwa ww kwenda kutumbukiza tu kikaratsi

2015 itakuwa kazi tutapigana kufa kupona hatukubali kupokonywa kura Kama mwaka Jana.
 
2015 chadema itakuwa vipande vipande, hata Vito 10 vya bunge haitapata achilia mbali upangaji wa magogoni.
 
watanzania hawa viongozi tulionao ni viatu tuvivue kama kweli tunahitaji mabadiliko kwenye nchii hii, ni mahalu mwenye pesa aliyeweka mawakili makini kufuatilia kesi yake ingekuwa kabwela kama mimi nimeshaozea jela
 
Back
Top Bottom