MAHAKIMU nao njiani KUGOMA...

mahakimu hawaruhusiwi kugoma kisheria.
labda hawa wapya hawajui ethics zao
hela watapelekewa fungu lao limeshatengwa.
waliendaje kwenye vituo vya kazi bila fedha za kujikimu na usafiri? inatia shaka.
Mgomo ndio mwisho wa mambo yote..
 
Ni kawaida Serikali ni Wazembe sana.Wafanyakazi wapya/ajira mpya serikalini huwa wanapata Tabu sana.Ni wacahache sana wanabahatika kupata mshahara baada ya miezi mitatu ya Kuajiriwa.Tena naona mahakimu wasiokuwa waadilifu wanaitumia nafasi hiyo kuchukua mlungula.
 
Aseee baba yangu sasa nani ataskiza kesi yangu niliibiwa mbuzi zangu na kesi iko mahakamani sasa wakigoma itakuwaje

ngoja nile mbege niwai mahakama kuu kisutu nikapinge mgomo
 
nani kakuabia kisutu mahakama kuu wajamini?
ni mahakama ya hakimu mkazi kama ilivo katika mikoa mingine
hakuna jaji pale. ni mahaka ya mkoa kama ilivo kinondoni pale kuna mahakama ya wilaya na mkoa pia
unaniabisha mkuu rombo ila mahakama pale mkuu wilayani karibia na bank ya NMB ina mahakimu wakazi pia sawa na kisutu tofauti ni mahakama ya wilaya lakini kimamlaka inasikiliza kesi sawa na mahakama ya kisutu.
Aseee baba yangu sasa nani ataskiza kesi yangu niliibiwa mbuzi zangu na kesi iko mahakamani sasa wakigoma itakuwaje

ngoja nile mbege niwai mahakama kuu kisutu nikapinge mgomo
 
Hakuna idara isiyostahili kugoma kwasababu hakuna idara ambayo haina rushwa.Hili ni endapo kama kuna ukweli kwamba mishahara midogo ni mojawapo ya vichocheo vya rushwa.
 
Hiyo inafanywa makusudi ili wajifunze kuomba rushwa. Mahakimu wote hupitia hatua hiyo. It is deliberately done by the government.
 
Wale Mahakimu Wakaazi 300 walioajiriwa na Serikali mnamo mwezi wa sita na kusambazwa mikoani wako njiani kugoma.Taarifa nilizozipata zinaonesha kuwa Mahakimu hao,tangu kuajiriwa kwao hawajalipwa mshahara wowote au hata fedha za kujikimu. Taarifa zinaonesha kuwa hali zao sasa ni mbaya na wanateseka vya kutosha.

Kwakuwa wote wanajuana vyema,Mahakimu hao Wakaazi ambao wamepelekwa kwa mara ya kwanza katika Mahakama za Mwanzo wamepanga kugoma ili kudai maslahi yao kwa Serikali 'sikivu'. Ifahamike kuwa Mahakimu wakaazi ni wale wenye elimu ya ngazi ya Shahada na kuendelea na hawakuwahi kuwepo katika Mahakama za Mwanzo.Kupelekwa kwao,kutaruhusu Mawakili Wasomi kujitokeza Mahakama za Mwanzo.

Wanasema 'liwalo na liwe'....

Tuondolee ***** hapa weka source? Na haya yakufikirika muyazuayo ndiyo kila siku yanazidi kuwaondoa watu makini kushabikia CHADOMO muda sio mrefu mtabaki vichwa nazi kama wewe
 
[COLOR=#RED]KJ anaingia madarakani alikiri kuwepo na kiasi cha kutosha Hazina kwa kuleta maendeleo je zile pesa zimekwenda wapi na jufanya nini[/COLOR]
 
KJ anaingia madarakani alikiri kuwepo na kiasi cha kutosha Hazina kwa kuleta maendeleo je zile pesa zimekwenda wapi ? na kufanyia nini
 
Hawa polisi nao wana subiri nini? ina maana wameridhika kukaa kweye vimagofu na tumishahara twao twa kijinga hutu!
 
"Tutaleta Mahakimu kutoka China, tumejipanga kwa hilo"
Ndo jibu tutakalopewa na Magamba hili
 
Jamani kama ni kweli ebu walipwe stahili zao! Hii migomo si mizuri haina afya kwa Serikali yetu wala maendeleo kwa jamii.
 
Aseee baba yangu sasa nani ataskiza kesi yangu niliibiwa mbuzi zangu na kesi iko mahakamani sasa wakigoma itakuwaje

ngoja nile mbege niwai mahakama kuu kisutu nikapinge mgomo
Nawe MBEGE ZITAKUZEESHA, KILA SIKU?
 
Back
Top Bottom