Mahakama yatupa hoja za serikali; Bunge laachiwa

Mimi naona siyo Mtikila aliyeshindwa bali ni watanzania wapenda demokrasia ya kweli wameshindwa. Kwa lugha nyingine ni kuwa demokrasia imeshindwa Tanzania. Kwa hiyo wabunge wa CCM wataendelea kuwa misukule ya watawala kwani wataendelea kufinywa kwa koleo liitwalo kulinda masilahi ya chama. Masikini wasomi wetu watakao kuwa wabunge kupitia CCM wataishia kufungwa midomo na akili zao na watu wasio na elimu kama akina Y M .
 
Tupate hukumu yenyewe kikamilifu; mimi sidhani kama majaji 7 wanaweza kutoa hukumu ya kijinga hivyo. Kuna conflict katika katiba maana upande mmoja inampa ,wananchi haki ya kuchaguliwa na upande mwingine inamnyang'anya haki hiyo kwa kumlazimisha kitu ambacho labda ni kinyume na matakwa yake (kujiunga na vyama vya siasa). Je conflict hiyo wameizungumziaje?
Je wamesema mahakama kuu haikuwa na uwezo wa kusikiliza kesi inayohusu masuala ya katiba? na kama ni hivyo masuala hayo yapelekwe mahakama gani maana hatuna mahakama ya katiba! Huwezi kusema hayo yapelekwe bungeni maana uamuzi wa wabunge ndiyo ulileta conflict hiyo na hivyo mwananchi yeyote aliyekuwa -aggrived na maamuzi ya bunge hawezi tena kwenda bungeni- bali mahakamani.
Kuna ,mambo mengi yanayohitaji ufafanuzi katika hukumu hiyo.

Kama kweli mahakama imesema suala ni la kisiasa - je kesi ya kisiasa ipelekwe mahakama gani?

Ni hatari sana - watu wamepoteza imani na polisi, wamepoteza imani na mahakama hasa za chini na sasa wakipoteza imani na mahakama ya juu kabisa! itakuwa hatari zaidi ya kile mahakama ya rufaa ilichokiogopa - eti hakuna nchi inaongozwa na mtu huru/binafsi maana ni vizuri mtu binafsi akaingia kwa kupigiwa kura kuliko ukimzibia njia ya kura akaamua kuingia kwa njia ya mtutu! Tusijidanganye eti TZ hiyo haiwezekani, hata enzi za Obote hakuna aliyewazia hilo, enzi za Kenyatta na Moi hakuna akliwazia hilo - lakini yakatokea.!
 
its not, and it can never be a big deal than to overhaul the whole constitution!

These are petty things in a rotten country
 
hakuna mahakama nyingine juu yake.. ndio uamuzi wa mwisho.. ila ningependa kupata details na reasoning yao. Inawezekana ameshinda kwenye hoja ya uwezo wa mahakama kutengua kipengele cha Katiba na siyo hoja ya wagombea binafsi au itarudishwa kesi mahakama Kuu.. kupitia tena.

Mwanakikijiji, the brief summary is, Issue ni kuwa mahakama haiwezi kutengua mabadiliko ya katiba hata kama yangekuwa mabaya kiasi gani. Mahakama inaweza kufanya hivyo pale tu endapo masharti ya ibara 98(1) (a) na (b) yanayohusu utaratibu wa marekebisho yatakuwa yamekiukwa na sio content ya marekebisho.Vipengele vya katiba vinakinzana in the sense kuwa haki ya mgombea binafsi ipo lakini wakati huo huo sheria na katiba vinakataza na kwa maoni yao basi hakuna wanachoweza kufanya zaidi ya kumwambia mwanasheria kuwa aangalie hilo na kulifanyia kazi.Mwanasheria mkuu wa serikali ameambiwa na kuelekezwa mara nyingi kuhusu issue mbalimbali lakini anakuwa mzito kutekelezawakatoa mfano wa Kesi ya Seif Sharriff Hamadi miaka 17 iliyopita amabapo mpaka leo hakuna kilichofanyika pamoja na mahakama ya rufaa kukumbusha tena hapo katikati.Hivyo basi suala la mgombea binafsi liende bungeni kwa kuzingatia matamko ya haki za binadamu ( universal declaration on Human rights) amabzo tumesaini hususani kifungu 26 ambacho kinafanana na kifungu 21 cha katiba yetu.
 
Wagombea huru hata huko ilikoanzia hii democrasia tunayoiiga ni wachache sana tena kwenye ngazi ya UBUNGE tu. Sisi tunataka kuuparamia utaratibu huu kichwakichwa bila maandalizi yoyote, uelewa wa watu wetu bado mdogo. Mnataka kurudisha masultani, watemi na wafalme kwa mlango huu? Acheni hizo.
Tujipange vizuri kwanza kwenye mambo ya kuchagua na kuchaguliwa. Wagombea huru wabaki kwenye mambo ya uchumba tu kwanza. Hata kugombea uongozi YANGA ni lazima uwe MWANACHAMA!
 
MAHAKAMA KUU YA TANZANIA, leo imetoa hukumu yake katika kesi ya kikatiba iliyofunguliwa na Mchungaji Mtikila akitaka wagombea Urais binafsi waruhusiwe. Wakitoa hukumu yao leo, jopo la majaji saba likiongozwa na Jaji Mkuu wa Tanzania, Augustina Ramadhani, wamesema kuwa shauri hilo ni la kisiasa zaidi na lilipaswa kujadiliwa Bungeni na kwamba Mahakama haina mamlaka ya kuamua suala hili.Mtikila hakuridhika na uamuzi huo na badala yake amedai atakata rufaa na ataiomba Mahakama izuie Uchaguzi Mkuu ujao hadi hapo shauri lake litakapopatiwa ufumbuzi. Ameahadi kwenda hata Mahakama ya Afrika Mashariki kama ikibidi kufanya hivyo. Shauri hili lilivuta hisia za wanasiasa wengi na hukumu yake ilikuwa ikisubiriwa kwa hamu kwani ni ya kihistoria.
 
Wadau kama kuna aliesoma hukumu ya kuhusu uingizwaji wa mahakama ya Kadhi kwenye "Zero" au "Boma Draft" huko Kenya hivi karibuni. Nchi ambayo kwa kiasi kikubwa tunashare mfumo mahakama zetu kwa maana ya urithi toka wa waingereza ambapo moja ya hoja zilizoibuka ilikuwa ni juu ya uwezo wa mahakama kuu ya kenya kama ina mammlaka ya kutengua kipengele chochote cha katiba, naamini hata kwa kesi hii imetupwa kwa kigezo kilekile cha High Court despite of its inherent powers haina mamlaka ya kutengua kipengele chochote cha katiba. With due respect guys katika kesi ya huko Kenya haya ndiyo yaliyosemwa na mahakama;

"...........Mr. Ombwayo, learned Principal Litigation Counsel argued, and we agree with his argument, that the court does not have jurisdiction to strike out Section 66 of the Constitution even if (as he seemed to agree) it contradicts Section 82 of the Constitution. Counsel also argued that no provision of the Constitution is superior to the other. With respect we do not agree with that submission. For instance the Bill of Rights, which are also referred to as universal, inherent and natural rights, cannot be taken away by the State. In addition we also hold that the courts have the jurisdiction to declare conflict or inconsistency in the constitutional provisions, or to declare whether or not the provisions are in conflict with any values, principles or purposes of a democratic constitution such as ours.
  • This court would not have a role or does not play any role in the alteration of Section 66 of the Constitution or any other section of the Constitution. The process of altering Section 66 of the Constitution or indeed any other provision of the Constitution lies in the National Assembly (Parliament which enacts thelaw and the President who assents to the law) before it becomes operational or comes into effect. Whereas an amendment may be challenged in court once enacted into law, only Parliament has the necessary legislative mandate to alter the provision by way of amendment provided the provisions of section 47 on amendments are satisfied. … The Applicants prayer to declare Section 66 of the Constitution void is therefore not tenable and is declined.
  • the Judicature too is a creation or creature of the Constitution, and whereas it has power to interpret any provision of the Constitution (under sections 67, 84 and123(8) of the Constitution, that power is limited to interpretation and constitutional judicial review but not alteration of the Constitution. Under its constitutional judicial review jurisdiction the court may grant a declaration in the event of conflict of provisions.
  • Parliament does not have the power to take away the basic structures of the constitutional "sanctum"‐ the Bill of Rights, the security of tenure of Judges, which is the cornerstone of the rule of law, and the democratic provisions of Section IA of the Constitution. The second exception is that it is only the people who have the power to enact a new constitution."
 
reasoning yao very poor,am afraid siasa imeingia mahakamani....credibility ya court kama mhimili wa dola haipo..
 
Wagombea huru hata huko ilikoanzia hii democrasia tunayoiiga ni wachache sana tena kwenye ngazi ya UBUNGE tu. Sisi tunataka kuuparamia utaratibu huu kichwakichwa bila maandalizi yoyote, uelewa wa watu wetu bado mdogo. Mnataka kurudisha masultani, watemi na wafalme kwa mlango huu? Acheni hizo.
Tujipange vizuri kwanza kwenye mambo ya kuchagua na kuchaguliwa. Wagombea huru wabaki kwenye mambo ya uchumba tu kwanza. Hata kugombea uongozi YANGA ni lazima uwe MWANACHAMA!

Swadakta....huu ndio uhuru wa kutoa maoni..........
 
MAHAKAMA KUU YA TANZANIA, leo imetoa hukumu yake katika kesi ya kikatiba iliyofunguliwa na Mchungaji Mtikila akitaka wagombea Urais binafsi waruhusiwe. Wakitoa hukumu yao leo, jopo la majaji saba likiongozwa na Jaji Mkuu wa Tanzania, Augustina Ramadhani, wamesema kuwa shauri hilo ni la kisiasa zaidi na lilipaswa kujadiliwa Bungeni na kwamba Mahakama haina mamlaka ya kuamua suala hili.Mtikila hakuridhika na uamuzi huo na badala yake amedai atakata rufaa na ataiomba Mahakama izuie Uchaguzi Mkuu ujao hadi hapo shauri lake litakapopatiwa ufumbuzi. Ameahadi kwenda hata Mahakama ya Afrika Mashariki kama ikibidi kufanya hivyo. Shauri hili lilivuta hisia za wanasiasa wengi na hukumu yake ilikuwa ikisubiriwa kwa hamu kwani ni ya kihistoria.

Sielewi kabisa hapo kwenye highlight nyekundu, ni vipi suala la haki ya mtu kuchagua au kuchaguliwa likawa la kisiasa wakti liko ndani ya katiba? Mimi nafikiri hili ni suala la kikatiba zaidi na wala sio la kisiasa, ila Mahakama ndio imetoa uamuzi wa KISIASA! shame on our judiciary system!
 
Duuh hiki kigingi cha haki ya mtu kugombea bila kutumia mwavuli wa chama kitaondolewa lini jamani ?
 
Hatimaye rufaa yatupwa uamuzi kufanywa na Bunge!.

Na Bunge halifanyi mabadiliko mpaka yaletwe na serikali (maana wabunge wetu ni wavivu wa kuandaa miswada binafsi-in fact tangu bunge la vyama vingi lianze sijawahi kusikia mbunge akiwasilisha muswada binafsi). Kwa maana hiyo, hoja ya mgombea binafsi ni mpaka serikali itakapoamua... laiti kama tungemwelewa Marmo
 
kata rufaa mwana kesikesi huko mbele labda utashinda, eti kesi hii ni ya kisiasa zaidi, mwanzo ilikuwa ni ya kikatiba mmmh, wamenikata nyongo nilidhamiria kurudi tena ulingoni mara hii nikijisimamia mwenyewe loooooooooooh. mtikila endelea USICHOKE.
 
Sielewi kabisa hapo kwenye highlight nyekundu, ni vipi suala la haki ya mtu kuchagua au kuchaguliwa likawa la kisiasa wakti liko ndani ya katiba? Mimi nafikiri hili ni suala la kikatiba zaidi na wala sio la kisiasa, ila Mahakama ndio imetoa uamuzi wa KISIASA! shame on our judiciary system!

This country is really screwed up. Kama mahakama inakubaliana na uamuzi ambao unavunja katiba basi tumekwisha. Augustino Ramadhani unaipeleka wapi mahakama kama unaweza kuburuzwa na wanasiasa kiasi hicho? Tukimbilie wapi sisi wananchi pindi tunapoona tunaonewa? Unawafundisha nini mahakimu wanaotoa hukumu kali kwa kesi za kubambikiza au kwamba hata wewe unaweza kufanya uamuzi kwa influence ya chama tawala? Damn!!!!!!!
 
MAHAKAMA KUU YA TANZANIA, leo imetoa hukumu yake katika kesi ya kikatiba iliyofunguliwa na Mchungaji Mtikila akitaka wagombea Urais binafsi waruhusiwe. Wakitoa hukumu yao leo, jopo la majaji saba likiongozwa na Jaji Mkuu wa Tanzania, Augustina Ramadhani, wamesema kuwa shauri hilo ni la kisiasa zaidi na lilipaswa kujadiliwa Bungeni na kwamba Mahakama haina mamlaka ya kuamua suala hili.Mtikila hakuridhika na uamuzi huo na badala yake amedai atakata rufaa na ataiomba Mahakama izuie Uchaguzi Mkuu ujao hadi hapo shauri lake litakapopatiwa ufumbuzi. Ameahadi kwenda hata Mahakama ya Afrika Mashariki kama ikibidi kufanya hivyo. Shauri hili lilivuta hisia za wanasiasa wengi na hukumu yake ilikuwa ikisubiriwa kwa hamu kwani ni ya kihistoria.

Siipatipati vizuri hii habari:

Mahakama Kuu, Majaji saba, ikiongozwa na Jaji Mkuu -Agustina Ramadhani!!!...Mtikila atakata rufaa.

Awali niliwahi kusoma hii hapa nikadhani suala lilikuwa Mahakama ya Rufaa...kumbe ni Mahakama Kuu..duh!!

Rufaa ya mgombea binafsi wiki ijayo

RUFAA ya kesi ya kikatiba dhidi ya hukumu iliyobatilisha sheria inayozuia mgombea binafsi, imepangwa kuanza kusikilizwa Februari 8 na Mahakama ya Rufaa.

Katika kesi iliyofunguliwa na mwenyekiti wa Chama Demokrasia (DP), Mchungaji Christopher Mtikila, mahakama ilikubaliana na hoja zake za kupinga suala la mgombea binafsi kuzuiwa na katiba ya nchi, lakini serikali ikakata rufaa kupinga hukumu hiyo.

Rufaa hiyo namba 45/2009 itasikilizwa na Mahakama ya Rufaa.
Kwa mujibu wa orodha ya kesi zitakazosikilizwa katika vikao vya mahakama hiyo, rufaa hiyo itaanza kusikilizwa saa 3:00 asubuhi mbele ya jopo la majaji saba wakiongozwa na Jaji Mkuu Agustino Ramadhani.
Majaji wengine katika jopo hilo ni Jaji Eusebio Munuo, Jaji Msofe, Jaji Kimaro, Jaji Mbarouk Mbarouk, Jaji Bwana na Jaji Luanda.

Katika uamuzi wao kwenye kesi ya msingi, jopo la majaji watatu Mahakama Kuu (Jaji Amir Manento, Salum Massati, ambaye kwa sasa ni wa Mahakama ya Rufaa, na Thomas Mihayo (mstaafu), walikubaliana na ombi la Mtikila na kuruhusu mgombea binafsi kuwania urais na ubunge.

Lakini serikali ilikata rufaa kwa madai kuwa Mahakama Kuu ilikosea kujipa mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo; ilikosea kutengua vifungu vya katiba ya nchi, na kukosea kisheria kwa kupunguza matakwa ya lazima ya ibara 30(5) na 13 (2) ya katiba ya nchi.

Sababu nyingine ni kujipachika mamlaka ya kibunge ya kutunga sheria, kukosea kisheria kwa kuiweka katiba ya nchi katika vyombo vya kimataifa na pia ilikosea kuitolea maamuzi kesi hiyo bila kuweka suala hilo bayana.
Rufaa hii ni ya pili kwa serikali kupinga uamuzi wa kuwepo kwa mgombea binafsi. Kwa mara ya kwanza serikali ilikata rufaa kupinga uamuzi huo mwaka 2007, ikidai kuwa Mahakama Kuu ilikosea kisheria kutafsiri vipengele vya katiba ya Jamhuri ya Muungano.

Hata hivyo, rufaa hiyo ilitupwa na Mahakama ya Rufaa baada ya kukubaliana na ombi la wakili wa Mtikila, Richard Rweyongeza kwamba rufaa hiyo haina msingi na imejaa dosari za kisheria.

http://www.mzalendo.net/habari/kitaifa/rufaa-ya-mgombea-binafsi-wiki-ijayo
 
Today is a very sad day for our nation. With the judgment history has been undone; bigotry has triumphed over justice, light of hope for a prosperous nation has once again been blown-out ... we have to change the tactic
 
Back
Top Bottom