Mahakama yatoa amri ya kuzuia mgomo wa madaktari hapo kesho!

Madaktari tanzania hawana UTU, wanatazama maslahi binafsi.

serikali ndio haina utu! mbali na kuangalia maslahi ya wafanyakazi wakiwepo madaktari, wao wanaangalia matumbo yao madaktari wanakosa hata gloves na vifaaa ambavyo ni basic?? madaktari wanaambukizwa hata magonjwa kutokana na kukosa vifaa vya kujikinga halafu unasema hawana utu? huna tofauti na mwigulu!!!
 
Utamburuza punda mpaka mtoni lakin je maji atakunywa? kama kama atakunywa bas ni kwakua ameridhika na si vinginevyo. Attendance regester itajaa by saa moja na nusu lakin je wodin wataenda?na kama wataenda watahudumu?na kama watahudumu je huduma itakua stahiki?
Watanzania maisha yetu yanachezewa kamali kwajili ya upumbavu wetu. Tukachagua kundi la wahuni (wanamtandao) na kuliweka madarakan. Hapa hatuteswi na kingine bali upumbavu na uoga wa watanzania sisi wenyewe. Usipovuka mto huez jua kilichopo ng'ambo na hilo ndio tatizo letu tunaogopa unaeza enda ng'ambo ukakuta sio kuzur bt hatujiuliz je kama ni kuzur?
Shame on us Tanzanians including me and all zamakafaz wanaoshabikia upumbavu na mtandao.

Mzalendokweli!

I tend to agree with you. Ni ukweli usiopingika kwamba Mgomo wa Madaktari imekuwa Kama ile opera ya Isidingo. Hailekei kuisha.

Kila mara wanatangaza mgomo Pinda anakimbilia Mahakama kuu kitengo cha Kazi. Nao wanasikiliza upande mmoja wa Werema tena usiku na kutoa amri ya kubatilisha mgomo. Madaktari wakifyata mkia wanaongea and them wanarudi CMA.

Tatizo ni kwamba wanaotaka kugoma they don't comply to the law na huwa hawana Plan B. Kwa mujibu wa sheria ya Kazi za mwaka 2004. Madaktari wako katika kundi la wafanyakazi ambao kisheria hayaruhusiwi KUGOMA.

Sheria haizui "a walk out " that is simply wafanyakazi hawaendi kazini mpaka madai yao yatimizwe. Kitendo Kama hicho kinahitaji ujasiri wa dhati na lazima wakae kitako na kutafakari. Maana yake serikali haitawalipa mishahara kwa muda wote wa hiyo " walk out" Swali linakuja je Madaktari wanaweza kufanya hilo and still survive?

Sidhani kama Madaktari wa Afrika wameshafikia ukomavu wa kiasi hicho! This means what they have planned sio endelevu kwa kuwa hiyo ligi ni kubwa and I can only see circus .

Kwa kuwa mgomo wao ni wa kibaguzi yaani ili wafanikiwe ni lazima wafanyakazi wote sekta ya afya ya umma( public hospitals) waweke gloves down na kutokuhudhuria hospital kutoa huduma mpaka kieleweke. Hilo haiwezi kutokea kwa hiyo basi mgomo huo utakuwa just like a paper tiger and Doctors stand to end up as loosers of course at the peril of wagonjwa.

Ushauri wangu kwa serikali Dhaifu ya Rais Dhaifu( Kikwete) kwa kuwa budget imepita kwa mbinde just give the Doctors what they want hivi Madaktari kwenye hizo public hospitals ni wangapi? You can even opt to go half mile it won't be a big deal just endeleeni kuokopa because as usual CCM can't think out of the box. Hii mgomo ni aibu just learn from Kibaki he went the extra mile kawalipa medics and avoided embarrassment . Hivi hamkuumbwa na haya au ni hiyo mioyo ya biff za extremism Boko Haram and Uamsho type??

Tufike mahali tufanye maendeleo , in the budget you want to employ 71,000 new employees sasa Kama hakuna development budget hao watu mnawaajiri kufanya kazi gani au ni hiyo Mikoa mipya mliyoanzisha with pomposity?.

Kweli watu weusi is a problem of its own.
 
Hahahahaha! MAHAKAMA! MAHAKAMA! MAHAKAMA! KWANI MAHAKAMA NI NGENI? HAMNA JIPYA HAPO! We jiulize, Ule mgomo phase II si ulizuiliwa na mahakama pia?! Nini kiliendelea baada ya madaktari kula msimamo na kuendelea kugoma? Si ilifyata! Chezea madaktari eeh! Mtasoma plate number tu, haooo! Wamatokomea! Na Huwez ukawaweka Lupango wote maana huko ni zaidi hata ya kuwaacha wagome
 
Kwanini usinunuwe wewe mtungi wa gesi kwa fedha unazopata kutoka hospitali za private, kama kweli una nia ya kuokoa maisha? ambazo kuna uwezekano mkubwa kuwa hata kodi huzilipii.



Mjomba kwa Mchango huu Umejivua Nguo kabisa,nilijua siku nyingi kwamba una dosari katika Ubongo wako wa Mbele lakini sikujua kama ni dosari kubwa kiasi hiki!!
Mgomo ukiisha nenda Muhimbili kitengo cha Wagonjwa wa Akili,Unahitaji Msaada kabisa!!
 
Kiongozi wa serikali yetu ni dhaifu, matokeo yake serikali yetu anayoiongoza kiongozi dhaifu imekuwa dhaifu ingawa wengi hawataki kukiri wazi juu ya hili. Ushahidi mkubwa upo katika namna serikali inavyoshindwa kutatua matatizo muhimu ya nchi kama hili la madaktari. Sikuweza kuamini nilipomsikia Waziri Mkuu anasema serikali imelipeleka swala la madaktari mahakamani.
 
Kiongozi wa serikali yetu ni dhaifu matokeo yake serikali anayoiongoza imekuwa dhaifu. Ushahidi wa udhaifu huu ni pamoja na namna inavyotatua matatizo makubwa ya nchi kama hili la madaktari. Sikuamini nilipomsikia waziri mkuu anasema serikali imelipeleka swala la madaktari mahakamani.
 
Mahakama kuu divishen ya Kazi imepiga marufuku mgomo wa madaktari ambao ulipangwa kufanyika kuanzia kesho.

Source- Habari ITV

Hivi hii mahakama ya kazi, kwanini isiibane serikali kutekeza makubaliano. Hizi mahaka zina harufu ya mgongano wa kimaslahi
 
Wala hakuna Keko au babake na Keko, wakati wanahangaika Muhimbili na kwingineko mahakama zilikuwa wapi? Tatizo la TZ hatuna kigezo cha mshahara, watu darasa la 7 (eti wabunge wakiingia tu wanaanza na 90,000,000/=) kama gratuity ya kununua magari, halafu msomi aliyekaa shuleni kwa miaka zaidi ya 23 anaambiwa atapewa laki tatu wapi na wapi na nani atakubali? Nchi hii inahitaji akina Hiter ili tuongeze bidii ya kazi na tuogope wizi wa waziwazi

Kuna falas fulani wanona hawa wagonga mabenchi ndio wanastahili sana pesa. Hii ni saerikali dhaofu sana. Ngoja chinja tupa waanze.
 
Kwanini usinunuwe wewe mtungi wa gesi kwa fedha unazopata kutoka hospitali za private, kama kweli una nia ya kuokoa maisha? ambazo kuna uwezekano mkubwa kuwa hata kodi huzilipii.

mimi ni mwalim lakin kama chaki zimeisha siwez nunua,,,,hiyo bajet inayopitishwa na kupigiwa makof inaenda wapi,,,,huo mshahara hautosh uende ukanunue mtungi wa gas,halafu mganga mkuu anatembelea VX huu si wehu????
 
Hivi hii mahakama ya kazi, kwanini isiibane serikali kutekeza makubaliano. Hizi mahaka zina harufu ya mgongano wa kimaslahi

Kwa hakika inajionyesha kwamba mahakama ya sasa sio mhimili unaojitegemea bali chombo cha serikali. Inasikitisha.
 
mimi ni mwalim lakin kama chaki zimeisha siwez nunua,,,,hiyo bajet inayopitishwa na kupigiwa makof inaenda wapi,,,,huo mshahara hautosh uende ukanunue mtungi wa gas,halafu mganga mkuu anatembelea VX huu si wehu????

Kwani chaki zinaokoa maisha au zinatia ugonjwa tu wa kifua? Tena chunga sana na ikiwezekana sita kutumia chaki, ni hatari sana kwa afya yako ya baadae. Kuna njia mbadala nyingi tu.
 
Mtazamo wangu uko tofauti -- sisapoti mgomo!
Namfikiria zaidi mtanzania ambaye hawezi kufika hospitali binafsi za kulipia, ni muhimu sana kupata suluhu mezani. Madai ya ndugu zetu doctors yana maana hasa ktk allowances. Ingawa kwa mtazamo wangu demand yao ni kubwa kidogo, ni kweli wanafanya kazi katika mazingira magumu sana. Lakini pia ni muhimu sana kwao kuangalia on the side of the coin.
 
Kama wakigoma watu watakosa huduma na kufa. Je wasipotii amri ya mahakama wakagoma na kushtakiwa kwa kudharau amri ya mahakama, wakapelekwa mahabusu, je huko hosptalini si kutakuwa hakuna waganga? Je watakapokuwa lupango hapo wagonjwa hawatakufa? Au tutaenda kupasuliwa matumbo na kutibiwa ukichaa wetu hukohuko magereza?
 
Utu!serikali inawafanyia wao utu?Kama suala ni Utu mbona serikali isilazimishe hizi private hospitals kupokea wagonjwa
hata ambao hawana pesa?Madaktari ni moja ya sekta muhim sana kwenye nchi yoyote dunian.Nakuhakikishia wakigoma
bila kukoma Jk ataikimbia ikulu.Take my word.
 
utatia Lupango madaktari na na wauguzi wote??
Kwa jinsi serikali yetu ilivyochoka, inaweza kufanya hivyo. Unajua ukichoka sana hata uwezo wa kufikiri huwa unapungua. Hii serikali ni bure kabisa.
 
siku mahakama zikigomea serikali,hii serikali itakimbilia wapi? pccb?, kwa wananchi? au ina na mahakama wa kuto salitiana?
 
Back
Top Bottom