Mahakama yatoa amri ya kuzuia mgomo wa madaktari hapo kesho!

Nicas Mtei

JF-Expert Member
Dec 21, 2010
11,556
7,085
Mahakama kuu divishen ya Kazi imepiga marufuku mgomo wa madaktari ambao ulipangwa kufanyika kuanzia kesho.

Source- Habari ITV
Mahakama Kuu ya Tanzania imetoa amri ya kusitisha mgomo wa Madaktari

Kufuatia Tangazo la Chama cha Madaktari nchini (MAT) la kuanza mgomo siku ya Jumamosi tarehe 23 Juni, 2012, Mahakama Kuu ya Tanzania, Kitengo cha kazi, Dar es Salaam imetoa amri ya kusitisha mgomo huo mpaka hapo pande zote mbili yaani Serikali na Chama cha Madaktari Tanzania (MAT) yatakaposikilizwa na kutolewa uamuzi.
- Amri hiyo ya Mahakama imetolewa kufuatia maombi namba 73 ya 2012 yaliyowasilishwa chini ya hati ya dharura na Mwanasheria Mkuu wa Serikali dhidi ya Chama cha Madaktari Tanzania (MAT).Sababu za msingi amabazo zimepelekea Mahakama kuu kutoa amri hiyo upande mmoja ni pamoja na;
- Iwapo mgomo huo utatokea utakuwa na kuwa amri hii isipotolewa madhara yake ni makubwa isiyoweza kufidiwa kwa namna yoyote ile kama vile kupoteza maisha n.k

- Wajibu maombi, ambao ni MAT, inaundwa na Madaktari ambao wapo katika Sekta ambayo inatoa huduma mahsusi (essential service sector), Aidha Chama cha Madaktari Tanzania kimetangaza mgomo bila kufuatia taratibu zilizoanishwa katika Kifungu cha 76(1 na 2) cha Sheria ya Kazi (Employment and Labour Relations Act No 6 ya 2004.

Masharti hayo ni
- Kuzuia wafanyakazi walio katika Sekta Muhimu kugoma na kama wakigoma,
- Kuwepo na makubalianao ya pamoja ya kutoa huduma za msingi wakati mgomo ukiendelea.

Kwa misingi hii, Mahakama Kuu ya Tanzania, inatoa rai kwa Chama cha Madktari Nchini na wanachama wake kusitisha na kutoshiriki katika mgomo huo.
 
Hivi unaweza kumlazimisha daktari au mwalimu kufanya kazi? :A S confused:
 
Mahakama kuu kitengo cha kazi chazui mgomo wa madaktari uliopangwa kuanza rasmi kesho.
Kwa maana hiyo watanzania tujiandae na mgomo mbaya kabisa ambao kwa mtazamo wangu utakuwa ni mgomo baridi ambao ni hatari zaidi na itakuwa kama cancer inayoua taratibu endapo hakuna juhudi zitakazochukuliwa kutatua mapema mgogoro huu.
source:taarifa ya habari ya saa 2 usiku ITV.
 
Wataalamu wa sheria naomba nisaidieni, serikali imezuia mgomo wa madaktari mahakamani. Nini kitatokea kama madaktari wataendelea na mgomo kisheria?
 
Wataalamu wa sheria naomba nisaidieni, serikali imezuia mgomo wa madaktari mahakamani. Nini kitatokea kama madaktari wataendelea na mgomo kisheria?
Watashtakiwa kwa kudharau Mahakama, na wakipatikana na hatia, ni moja kwa moja lupango.
 
Mi mwenyewe nagoma, kesho siendi kibaruani na nipo on call na hata kama nikienda sikugusi mgonjwa
 
walimu nao si waliamuliwa na mahakama wasigome hapo nyuma, eti warudi kwenye meza ya maelewano na serikali, lakin hamna kilichoendelea hadi wanataka kugoma tena....hii movie ya serikali mbona siielew elewi.!
 
Back
Top Bottom