Mahakama yatoa Amri Askofu Mokiwa na Wenzake wakamatwe kwa kutotii mahakama!

Kuna tatizo hapa tena kubwa sana, maana wewe mkeo akikushtaki mahakamani mahakama inatumia sheria ya ndoa kuhoji na kusikiliza hilo shauri!? Kama ni makosa ya Jina yana kuwa chini ya sheria ya makosa ya Jina, Kama ni malalamiko ya uchaguzi na pingamizi za uchaguzi Mahakama inatumia sheria ya Uchaguzi na ile ya tume ya uchaguzi sasa hili la kupinga uchaguzi wa Askofu Mahakama ina-refer sheria hipi? Jamani wanasheria tusaidieni kama kunasherika inasimamia chaguzi za Maaskofu hapa Tanzania.
 
Si wanasema sheria za dini zisikiuke au zisiende kinyume sheria au katiba ya JMT.
 
acheni ujuha, askofu mokiwa kafafanua, mahakama ilizuia kusimikwa kwa askofu wa angilkani jimbo la arusha. kanisa la anglikani limemsimika askofu wa anglikani jimbo la Tanzania, halijasema kuwa ni wa arusha. wamesema kuwa ibada imefanyika arusha, lakini askofu aliyesimkwa ni wa Tanzania yote. kama kesi ikiisha watampangia kituo arusha. la hasha watampeleka mahali popote duniani. ni kama kanisa katoliki maaskofu wanachaguliwa na papa, sasa mahakamani gani ya hapa nchini itazuia kuteuliwa kwao? ni vema hawo mahakimu vilaza wa hapo arusha wakafahamu sheria. kila siku wanatoa amri zinagonga mwamba
 
Wiki iliyopita mahakama mkoani Arusha ilitoa amri kuzuia kusimikwa kwa askofu mmojawapo wa kanisa la anglikana mkoani humo kufuatia kesi iliyofunguliwa na waumini watatu wa kanisa hilo.

Licha ya amri hiyo
HALALI ya mahakama jana askofu huyo amesimikwa hadharani katika sherehe iliyohudhuliwa na askofu mkuu wa kanisa hilo Valentino mokiwa. Najiuliza maswali, je kanisa liko juu ya sheria kiasi cha kutotii amri ya mahakama?

Je tutarajie hakimu atoe hati ya kukamatwa askofu mokiwa na wenzake kwa kukiuka amri halali ya mahakama?

Je mahakama itamzuia askofu huyo kutimiza majukumu yake ya kichungaji???? Je si kwamba kitendo hicho kimeidhalilisha mahakama na kuishushia hadhi mbele ya jamii na kuonekana amri yake si lolote si chochote? Yote haya ni maswali yanayohitaji majibu.

Wakuu
Mimi na wasiwasi na jinsi tunavyopokea taarifa, ikisoma maelezo au taarifa zilizo andikwa kwenye gazeti la Tanzania Daima la jumatatu,13 Juni 2011. Mwandishi Grace Macha pamoja ana kuwa na kichwa cha habari ambacho kwa mtizamo wangu hakiendani na aliyoyaandika kina fafanua kauli ya askofu Dr. Mokiwa anasema" kwa sasa wamemsimika kuwa askofu wa kanisa la Anglican huku wakisubiri matokeo ya kesi iliyo mahakamani ili waweze kumkabidhi dayosisi. Waandishi wa habari mliopo hapa mkaueleze umma kuwa hapa tumemsimika kuwa askofu,tunasubiri maamuzi ya mahakama ili tuweze kumkabidhi rasmi dayosisi. Msijali wiki ijayo nitakuwa hapa kuhitimisha hili" Kwa maelezo haya ya Askofu Mokiwa moja kwa moja yanaonyesha jinsi ambavyo hawajapingana na mahakama, kesi iliyoko mahakamani ni pingamizi la askofu Hotay kuwa askofu wa Dayosisi ta Mount Kilimanjaro. Haimkatazi askofu mkuu kumpandisha daraja/kumpa uasikofu kati ya watumishi walio chini yake.

Hawa viongozi wa dini hawaajiliwi na serikali wala mahakama hivyo sidhani kama wana uwezo wa kuzuia mtumishi yeyote kupatiwa madaraka. Kwa hiyo nafasi iliyoachwa na askofu Simon Makundi wa dayosisi ya Mount Kilimanjaro kimisingi bado iko wazi na wakati huo huo Askofu Hotay amepandishwa daraja la uaskofu. Ipo tofauti kubwa sana kati ya kilichofanyika na kilichokusudiwa kufanyika kikazuiliwa na mahakama sasa hapa mahakama ina mshutumu askofu na wafuasi wake kwa lipi?.

Kwa mtizamo wangu wananchi wanapotoshwa sana hasa na hizi taarifa ambazo zinatolewa,nyingine zenye harufu ya uchochezi
au baaadhi ya vyombo vya habari kueleza hadithi kwa lengo la biashara.
Na endapo hatuchukui muda wa kufanya tafiti tukalishwa kama watoto wadogo "spoon feeding" kuna hatari ya kuamini mambo ambayo yamepikwa ya fananefanane na ukweli, hali siyo kweli.

Mara yangu ya kwanza kuona taarifa hizi hata mimi zilinishitua, kwani nilimshangaa Askofu au viongozi wa dini ambao jamii inawategemea sana hasa kwenye maswala ya maadili, wanajihusisha na vitendo vya kuyavunja nilishangaa na kwa kuzingatia Dr. Mokiwa ambaye naamini udaktari wake siyo wa kupewa kama ambavyo sasa hivi madaktari wa kupewa walivyo wengi anaweza kufanya jambo hilo. Ndo katika fuatilia nikaiona hii article ya Tanzania Daima japo kuwa mwandishi wake naye kaandika kichwa chenye mwelekeo huohuo nikagundua kuwa kuna tatizo ya jinsi jamii walivyo habarishwa dhidi ya ukweli halisi.

Wakuu hasa wana jamvi hili tusaidie nchi yetu kama kweli tunao uzalendo kwa nchi yetu ili taarifa za jinsi hii ikipidi tuwe tunazifanyia kazi na pia na kuzisahihisha kisha kuelimisha jamii kwa ujumla.
 
Mahakama za Tanzania ni shirika la Binafsi, huko kumeja majitu Pungwani kabisa, gelesha na usanii ndiyo sheria yao. Tangu lini unaagizwa na watu watátu kutosimikwa Askofu aliyechaguliwa na mamia ya watu. Hao watatu ndiyo kundi la mafisadi. na Ukiwachunguza utagundua ndiyo wezi na watoa Rushwa wakubwa ngoja tuwadavadue.
 
MOD amechakachua kichwa cha habari. Niliandika kwa mtindo wa swali nikiuliza,"valentino mokiwa na wenzake kukamatwa???? Naomba MOD urejeshe hiyo heading unawachanganya wasomaji. Please MOD do it isije onekana nimeandika habari ya kupotosha. Binafsi sijasikia kama kuna amri yoyote imetolewa bali nilikuwa nahoja kama hali hiyo inaweza kutokea.
 
Arafat;tatizo co sheria,inategemea katiba ya anglican inasema vipi au miongozo yao inasemaje kama inasema asie ridhika akapinge mahakamani hawa mabwana wana haki,kama haisemi hivyo kesi itatupwa,na hili la kusimikwa mahakama ita angalia utaratibu wa kumpata askofu ukoje ni kuchaguliwa au kuteuliwa au vyote kwa pamoja kama ni kwa kuchaguliwa,basi huyu walie mteua atakua ni batili,nawasilisha
 
Hapa ndiyo mjue JK ni mtu wa visasi, amri ya kumkamata Dr.Mokiwa ni jibu la JK kwa kupewa masaa 48 kuwataja maaskofu wauza madawa ya kulevya
 
Wakuu
Mimi na wasiwasi na jinsi tunavyopokea taarifa, ikisoma maelezo au taarifa zilizo andikwa kwenye gazeti la Tanzania Daima la jumatatu,13 Juni 2011. Mwandishi Grace Macha pamoja ana kuwa na kichwa cha habari ambacho kwa mtizamo wangu hakiendani na aliyoyaandika kina fafanua kauli ya askofu Dr. Mokiwa anasema" kwa sasa wamemsimika kuwa askofu wa kanisa la Anglican huku wakisubiri matokeo ya kesi iliyo mahakamani ili waweze kumkabidhi dayosisi. Waandishi wa habari mliopo hapa mkaueleze umma kuwa hapa tumemsimika kuwa askofu,tunasubiri maamuzi ya mahakama ili tuweze kumkabidhi rasmi dayosisi. Msijali wiki ijayo nitakuwa hapa kuhitimisha hili" Kwa maelezo haya ya Askofu Mokiwa moja kwa moja yanaonyesha jinsi ambavyo hawajapingana na mahakama, kesi iliyoko mahakamani ni pingamizi la askofu Hotay kuwa askofu wa Dayosisi ta Mount Kilimanjaro. Haimkatazi askofu mkuu kumpandisha daraja/kumpa uasikofu kati ya watumishi walio chini yake.

Hawa viongozi wa dini hawaajiliwi na serikali wala mahakama hivyo sidhani kama wana uwezo wa kuzuia mtumishi yeyote kupatiwa madaraka. Kwa hiyo nafasi iliyoachwa na askofu Simon Makundi wa dayosisi ya Mount Kilimanjaro kimisingi bado iko wazi na wakati huo huo Askofu Hotay amepandishwa daraja la uaskofu. Ipo tofauti kubwa sana kati ya kilichofanyika na kilichokusudiwa kufanyika kikazuiliwa na mahakama sasa hapa mahakama ina mshutumu askofu na wafuasi wake kwa lipi?.

Kwa mtizamo wangu wananchi wanapotoshwa sana hasa na hizi taarifa ambazo zinatolewa,nyingine zenye harufu ya uchochezi
au baaadhi ya vyombo vya habari kueleza hadithi kwa lengo la biashara.
Na endapo hatuchukui muda wa kufanya tafiti tukalishwa kama watoto wadogo "spoon feeding" kuna hatari ya kuamini mambo ambayo yamepikwa ya fananefanane na ukweli, hali siyo kweli.

Mara yangu ya kwanza kuona taarifa hizi hata mimi zilinishitua, kwani nilimshangaa Askofu au viongozi wa dini ambao jamii inawategemea sana hasa kwenye maswala ya maadili, wanajihusisha na vitendo vya kuyavunja nilishangaa na kwa kuzingatia Dr. Mokiwa ambaye naamini udaktari wake siyo wa kupewa kama ambavyo sasa hivi madaktari wa kupewa walivyo wengi anaweza kufanya jambo hilo. Ndo katika fuatilia nikaiona hii article ya Tanzania Daima japo kuwa mwandishi wake naye kaandika kichwa chenye mwelekeo huohuo nikagundua kuwa kuna tatizo ya jinsi jamii walivyo habarishwa dhidi ya ukweli halisi.

Wakuu hasa wana jamvi hili tusaidie nchi yetu kama kweli tunao uzalendo kwa nchi yetu ili taarifa za jinsi hii ikipidi tuwe tunazifanyia kazi na pia na kuzisahihisha kisha kuelimisha jamii kwa ujumla.

Mkuu hayo unayosema ni kweli na yanajulikana, lakini tatizo ni hawa mahakimu wetu wanaoteuliwa kimjini mjini hata uwezo wa kuhoji ubongo wao ni mdogo na NI KWELI JAMAA (JAJI) KATOA AMRI YA KUKAMATWA ASKOFU MOKIWA hebu soma nukuu ya moja ya sehemu ya hukumu yake kuhusu kukamatwa kwa Askofu Mokiwa
"Nchi hii inaongozwa kwa misingi ya sheria na Rais Jakaya Kikwete amekuwa akieleza kuwa kila mtu anapaswa kuheshimu utawala wa sheria. Inasikitisha kama viongozi wa dini wanakiuka sheria, tukiendelea hivi itakuwa tabu sana," alisema Jaji Sambo.

Angalia alivyokuwa kilaza, reference anaitoa kwa Kikwete...
 
Hivi marehemu Jaji Lugakingira alipotoa hukumu ya mgombea binafsi kwa Rev Mtikila na Serikali kuipinga kuna mtu alipelekwa mahakamani?
 
Mimi nadhani yote ni mazuri tu haya na viongozi wa Kanisa waonje mgongano wao na wanasiasa; wamekuwa wakikumbatiana sana hadi wengine wamejisahau. Lakini ni nzuri pia kwa sababu inazidi kuwaonesha wananchi maana ya double standard hasa litakapotokea kwa viongozi wa CCM na serikali hasa wale wa ngazi za juu.

Kaka hiyo ni "blanket allegation". Dr. Mokiwa ni mtu mwenye msimamo sana. Si mtu wa kutumiwa na hawa wanasiasa uchwara.
 
najaribu kupata picha ingekuwa kuna tamko la mahakama la kumkamata sheikh mkuu,reaction ingekuwaje??
 
hivi askofu akibaka mtoto serikali ikae kimya isimfunge kwa kuwa anabaka kwa jina la yesu?au akiamua kuwa shoga,na kuwageuza waamini wake msosi tusimseme.na anaye uza dawa za kulevya kwenye madhabahu?.acheni kuingiza siasa za kijuha (magwanda politics)kwenye ishu za msingi..............most of your discussions here are based on hate ,hazina faida yoyote kwa mtanzania.mnafikiri mtaingia ikulu kupitia vi-comment vyenu vya kihuni mnavyotoa hapa,YOU ARE VERY WRONG!
 
najaribu kupata picha ingekuwa kuna tamko la mahakama la kumkamata sheikh mkuu,reaction ingekuwaje??

Mijanjaweed ingekuwa imesharuka barabarani bila kutafakari. Kati ya mambo yanayoshangaza duniani ni kitu kinaitwa dini make hakuna dini isiyokuwa na wafuasi na kila kimoja kina vituko vyake. Hata Shetani siku akiamriwa kukamatwa utashangaa watu watakavomwagika barabarani kumtetea kwani wanaokula kwa jina lake ni wengi. Utashangaa hata viongozi wa hizo dini nao watamwagika barabaran kumtetea kuwa shetani ni mwema sana make bila yeye hawana ajira wala ulaji.
 
Mimi nadhani yote ni mazuri tu haya na viongozi wa Kanisa waonje mgongano wao na wanasiasa; wamekuwa wakikumbatiana sana hadi wengine wamejisahau. Lakini ni nzuri pia kwa sababu inazidi kuwaonesha wananchi maana ya double standard hasa litakapotokea kwa viongozi wa CCM na serikali hasa wale wa ngazi za juu.[/QUOTE]

Mwanakijiji nakupa mfano hai, hapo kwenye red hapo.

Hapa kuna mkanganyiko wa mambo mengi,
Kwanza Askofu huyo hajasimikwa na kuwa askofu wa Dayosisi inayolalamikiwa. Alisimikwa tu kuwa Askofu wa Tanzania - bila dayosisi. Hayo ni malumbano ya wanasheria zaidi and am not a lawyer.

Pili kuna double standard kama alivyosema mwanakijiji. Wilaya ya ilala jimbo la ukonga kata ya Chanika kuna amri halali ya mahakama kuu imevunjwa na viongozi wa serikali akiwepo makamba aliyewaambia wananchi kuwa mahakama kuu ni yao. Mbona mahakama kuu iko kimya? Wananchi walinyang'anywa ardhi wakaenda mahakamani wakashinda kesi. Serikali ikapuuza. Wakafungua tena kesi ya pili mahakama kuu na kushinda tena. Serikali ikapuuza na kuwavunjia nyumba hizo, na wengine wakakosa pa kuishi. Makamba akiwa mkuu wa mkoa huku akiwakilisha maslahi ya mawaziri kadhaa alisimamia suala hilo bila kujali mahakama kuu hadi leo mahakama kimya. Mbaya zaidi, wananchi waliojifanya kukaidi amri ya serikali kwa kushikilia hukumu ya mahakama kuu mikononi mwao walifunguliwa kesi na wengine mpaka leo naandika karibu mwaka moja wako mahabusu. Sakata hili ilianza almost ten years ago.
Nawasilisha.
Swali, hapa hakuna double standard?
Je, hii ya Askofu, Mokiwa na freeman Mbowe ndiyo mahakama inataka kuonesha uwezo wake zaidi?
My take, Mahakama ya Arusha ina harufu ya Siasa.
 
Tatizo la kuwapata viongozi wa dini kwa mtindo wa kupigiana kura hayo ndio matokeo hasi!lzm wataibuka vichwa maji kwenda mahakamani!!sidhani rc kama wanaendekeza haya!mahakama tumia busara ktk hili ni issue tete!
 
Hili linanitatiza kdg kwa sababu mamlaka ya dunia yana nafasi yake hata ktk vitabu vitakatifu, Naogopa kuchanganya mamlaka ya duniani na mbinguni. Tusije tukawa tunaitafuta hasira ya Mungu ilipo. Mbona yametokea baada ya yeye kutoa msimamo wake kuhusu tamko la madawa ya kulevya na uongozi wa kanisa, Mimi naondoa ktk kikombe hiki
 
Back
Top Bottom