Mahakama yamwachia huru Naeem Gire wa Richmond

Another dark hour in Tanzania's horrible justice system! Mnakumbuka huyu JK mwaka 2008 Agosti alikwenda Bungeni kuweka mashitaka na pia kutoa hukumu ya washitakiwa wa EPA? Ilikuwa ni maajabu makubwa katika historia ya nchi hii.
 
Kweli kabisa! Iko mifano mingi ya unachokisema. Kesi dhidi ya waliotaka kumuuwa/kumpofua macho Kubenea ilianguka kwa sababu serikali haikuwa na nia ya kuona watuhumiwa hasa waliopanga shambulio hilo wangejulikana. Hivyo Tibaigana aliagizwa kuivurunda kwa kufanya upelelezi wa h
ovyo na pia kupeleka washitakiwa siyo na mashahidi siyo.

Yote hii ilimuradi tu serikali ionekane imetimiza jukumu lake la kuwapeleka wahalifu wote mahakamani!

Mfano mwingine ni ile kesi ya mauaji dhidi ya Wahindi wawili waliowachoma moto Waafrika wawili katika miaka ya tisini. Washitakiwa waliachiliwa na jaji alisema kuwa hajawahi kuona ushahidi mbovu iliopelekwa kuhusu kesi ya mauaji kama wa kesi hiyo.

kUMBE HAWA WALIACHIWA? KWA NINI NDUGU ZAO WASIWAHUKUMU NA WENYEWE?
 
mimi nikisema habari hizi zote zilitengenezwa na kina 6 mnakataa sasa mnaona sasa ngoja adai fidia mtaanza kusema ni ufisadi!!
 
Gire akitoka
makamani leo

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mjini Dar es Salaam, imemwachia huru Naeem Gire aliyekuwa akikabiliwa na kesi ya kughushi na kuwadanganya serikali kuwa mitambo ya Richmond ina uwezo wa kufua megawati 100 za umeme.

Gire ametoka kizimbani akichekelea baada ya hakimu wa mahakama hiyo, Waliarwande Lema , kutamka kuwa anamuona hana kesi ya kujibu kutokana na ushahidi uliofikishwa mahakamani na serikali kushindwa kumridhisha ili amuone kuwa na kesi ya kujibu.

"....Baada ya kupitia ushahidi katika vipengele vyote nimeona kuwa hakuna ushahidi wa kutosha uliowasilishwa kuridhisha kumuona mshitakiwa ana kesi ya kujibu...kesi hii ni miongoni mwa kesi kadhaa ambazo huletwa mahakamani na kisha kuitwisha lawama mahakama", alisema Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Waliarwande Lema."
Maghamba's in action 28th July 2011, kesi uchwala wananchi changa la macho, hiyo ndiyo TZ yako ilipofikia!!!!!!!!!! Kwani Rich Mond ni Gire peke yake????????????????
 
mimi nikisema habari hizi zote zilitengenezwa na kina 6 mnakataa sasa mnaona sasa ngoja adai fidia mtaanza kusema ni ufisadi!!

Wewe mgumu sana kufahamu yoote ambayo yameshatolewa na wachangaji hadi sasa. Serikali ilikuwa haina nia ya kuona yoyote anafungwa kuhusu Richmond kwa sababu kulinda masilahi ya EL, RA na JK watu hasa behind Richmond. Hivyo Gire alikuwa kama kafara tu.

Nikuulize? Hivi unakubali kabisa kosa (shitaka) aliloshitakiwa Gire ndilo hasa wananchi walitarajia kuona linatumika kuhusu sakata ya Richmond?
Yaani kwa ushahiudi wa kijinga uliopelekwa na serikali pale mahakamani, hakimu yoyote asingeweza kumuingiza Gire hatiani.

Kwa hiyo siyo suala la Sitta au nani, ni suala la serikali yenyewe kutotaka kupeleka mahkamani wale hasa waliohusika kwa kutumia ushahidi madhubuti.
 
"kesi hii ni miongoni mwa kesi kadhaa ambazo huletwa mahakamani na kisha kuitwisha lawama mahakama",

Kuna siri kubwa, nyuma ya sentensi hiyo ya Mheshimiwa Hakimu.

Hakimu kashituka kuna uchafu umefichwa makusudi ili mahakama kutoa maamuzi dhaifu kisha kukosa heshima machoni pa jamii
serikali bana
wanajifanya wana uthubutu kumbe legelege na geresha
 
Ingawa habari hii inakera, wala hainishangazi sana ninapofikiria seriousness ya Viongozi wetu kwenye Issues.

Hivi nani kawaroga Viongozi wetu???

Hii tabia ya kushindwa shindwa kesi itaisha lini?
 
Gire akitoka
makamani leo

 Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mjini Dar es Salaam, imemwachia huru Naeem Gire aliyekuwa akikabiliwa na kesi ya kughushi na kuwadanganya serikali kuwa mitambo ya Richmond ina uwezo wa kufua megawati 100 za umeme.

Gire ametoka kizimbani akichekelea baada ya hakimu wa mahakama hiyo, Waliarwande Lema , kutamka kuwa anamuona hata kesi ya kujibu kutokana na ushahidi uliofikishwa mahakamani na serikali kushindwa kumridhisha ili amuone kuwa na kesi ya kujibu.

"....Baada ya kupitia ushahidi katika vipengele vyote nimeona kuwa hakuna ushahidi wa kutosha uliowasilishwa kuridhisha kumuona mshitakiwa ana kesi ya kujibu...kesi hii ni miongoni mwa kesi kadhaa ambazo huletwa mahakamani na kisha kuitwisha lawama mahakama", alisema Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Waliarwande Lema.
 
Ilikuwa kumfunga paka kengele CCM wanajua vyema kilicho tokea slowly wanaanza kumsafisha Lowasa na wameanzia mbali mwisho mtaona wenyewe .Mie yangu macho haya .
 
Kama ilivyotabiriwa na community pundits wa humu JF kwamba mashtaka dhidi ya Gire yalikuwa ni dhaifu nailikuwa geresha ya serikali, here comes the proof!!!!!!!!!

My Take:
Hii ndiyo serikali mnayofikiria itawaletea umeme wa uhakika????????????? Hahaa ahahaha ahahaha!

Mahakama yamwachia Gire wa Richmond

Thursday, 28 July 2011 21:32
0digg

Nora Damian

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuachia huru mfanyabiashara Naeem Gire aliyekuwa anakabiliwa na kesi ya kughushi na kutoa taarifa za uongo kuhusu kampuni ya Richmond. Uamuzi huo ulitolewa jana na Hakimu Mkazi Wariyalwande Lema aliyekuwa anasikiliza kesi hiyo. Hakimu Lema alisema upande wa mashtaka umeshindwa kuthibitisha kesi dhidi ya mashtaka waliyomshtaki nayo Gire.

Alisema ushahidi wa upande wa mashtaka ulikuwa ni dhahifu na kwamba usingeweza kumfanya mshtakiwa huyo ajitetee. "Naiondoa kesi hii chini ya kifungu namba 230 cha Mwenendo wa Makosa ya Jinai kwasababu upande wa mashtaka umeshindwa kuthibitisha mashtaka dhidi ya mshtakiwa,"alisema Hakimu Lema.

Hakimu Lema alisema hakuna sehemu yoyote ambayo mshtakiwa huyo aligushi na kwamba vitu vyote vilifanywa na Mohamed Gire ambaye ni kaka wa mfanyabiashara huyo.

Baada ya uamuzi huo, upande wa mashtaka kupitia kwa Wakili wa Serikali, Shadrack Kimaro ulisema utakata rufaa kupinga hukumu hiyo. "Tunaomba tupewe nakala ya mwenendo wa kesi na nakala ya hukumu kwa ajili ya kwenda ngazi za juu zaidi,"alisema Kimaro. (Hahah ahahah!!!!!!! rufaa ya Zombe mliishia wapi???)

Gire alikuwa akidaiwa kuwa, Juni, 2006 jijini Dar es Salaam alitoa taarifa za uongo kwa wajumbe wa timu ya majadiliano ya Serikali, kuwa Kampuni ya Richmond LLC ya Texas, Marekani, ina uwezo wa kuzalisha umeme ili apewe zabuni.

Mfanyabiashara huyo pia alikuwa akidaiwa kuwasilisha hati ya nguvu ya kisheria iliyotolewa Machi 3, 2006 ikimuonesha kuwa aliruhusiwa na Mwenyekiti wa kampuni hiyo, Hemed Gire ambaye ni kaka yake kufanya kazi za kampuni hiyo hapa nchini. Mwisho.
 
Naomba niendeleze kicheko ila cha hasira: Ha ha ha haaaaa ... ! Serikali yetu na hoja za mtoto nyamaza nitakuletea pipi bwana. Kazi yote ya kwenda mahakamani ni kuwapumbaza watz kuwa kuna kazi imetendeka. Na hayo ndiyo maamuzi magumu wanayojitapa nayo kila siku. - inatia hasira sana.
 
Yaani acha kabisa mkuu, halafu watu wanakuja hapa kutuambia jinsi gani JK alivyo mkali kuhusu ufisadi!!!
 
naomba tusiweze naimani na mihimili ya dola maana ndio imekuwa sio dola bali ni ushabiki usionamatiki yoyote ndani ya vyombo hivi muhimu ndani ya nchi yetu. kwa hiyo siajabu hata hao kuachiwa tuataona mengi maana sheria zipo kwa ajili ya wizi wa kuku, maskini, wananchi wanyonge tusitegeme jipya kwa hawa wasanii
 
kweli mganga haagizi samaki!
Mtu kama gere ndie mmoja wa wahusika wakuu wa kuiingiza nchi katika mateso ya umeme na leo hii anachiwa huru kama njiwa angani? Yaani tunapoteseka sisi badala ya kutusaidia tutatue tatizo wajanja ndio kwanzaa wanatajirika na mahakama inawaachia huru! HUyu kimaro tafadhali naomba sana aache uchizi wa kutaka kudai kukata rufaa. Tena akiisha nunuliwa makochi tuu basi ataanzanza sheepesh smiles za kitoto.
 
Mkuu yalisemwa haya wakati ule ndio kwanza kesi inaanza, lakini kwa sababu hayo mashtaka dhaifu ndiyo ilikuwa hasa lengo la serikali haishangazi kuona haya matokeo!!!!!!!! kinachosikitisha zaidi kama ulivyo-highlight Gire kushinda hii kesi katikati ya giza nene ni ushahidi mwingine tosha kwamba serikali ya CCM is working against us! na haiwajali wananchi.
 
Sasa Mr Gire aende mahakamani akadai fidia. Things must get even worse before getting better. Waendelee tu kutukera na michezo yao ya kuigiza.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom