Mahakama yamwachia huru Naeem Gire wa Richmond

Kachanchabuseta

JF-Expert Member
Mar 8, 2010
7,270
675
Gire akitoka makamani leo

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mjini Dar es Salaam, imemwachia huru Naeem Gire aliyekuwa akikabiliwa na kesi ya kughushi na kuwadanganya serikali kuwa mitambo ya Richmond ina uwezo wa kufua megawati 100 za umeme.

Gire ametoka kizimbani akichekelea baada ya hakimu wa mahakama hiyo, Waliarwande Lema , kutamka kuwa anamuona hana kesi ya kujibu kutokana na ushahidi uliofikishwa mahakamani na serikali kushindwa kumridhisha ili amuone kuwa na kesi ya kujibu.

"....Baada ya kupitia ushahidi katika vipengele vyote nimeona kuwa hakuna ushahidi wa kutosha uliowasilishwa kuridhisha kumuona mshitakiwa ana kesi ya kujibu...kesi hii ni miongoni mwa kesi kadhaa ambazo huletwa mahakamani na kisha kuitwisha lawama mahakama", alisema Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Waliarwande Lema."
 
"kesi hii ni miongoni mwa kesi kadhaa ambazo huletwa mahakamani na kisha kuitwisha lawama mahakama",

Kuna siri kubwa, nyuma ya sentensi hiyo ya Mheshimiwa Hakimu.
 
Wamfunge kwa lipi wakati wamarekani wamekuja na wameshasema mitambo ya dowans(richmond) inaweza kufua hizo 100MW. te teeh na badoo jamaa lazima wale tuzo yao 94B.
 
ndio maaana nchi nyingine watu wanaamua kuchukua sheria mkononi-watu kama hawa next time hakuna haja ya kuwafikisha mahakami-ni kuwamaliza huku mtaani tu
 
naye kesho asubuhi anaenda kuifungulia serikali mashtaka na kudai mabilioni ya Shilingi. Mambo ya Vasco Dagama huyo
 
Gire akitoka
makamani leo

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mjini Dar es Salaam, imemwachia huru Naeem Gire aliyekuwa akikabiliwa na kesi ya kughushi na kuwadanganya serikali kuwa mitambo ya Richmond ina uwezo wa kufua megawati 100 za umeme.

Gire ametoka kizimbani akichekelea baada ya hakimu wa mahakama hiyo, Waliarwande Lema , kutamka kuwa anamuona hana kesi ya kujibu kutokana na ushahidi uliofikishwa mahakamani na serikali kushindwa kumridhisha ili amuone kuwa na kesi ya kujibu.

"....Baada ya kupitia ushahidi katika vipengele vyote nimeona kuwa hakuna ushahidi wa kutosha uliowasilishwa kuridhisha kumuona mshitakiwa ana kesi ya kujibu...kesi hii ni miongoni mwa kesi kadhaa ambazo huletwa mahakamani na kisha kuitwisha lawama mahakama", alisema Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Waliarwande Lema."

Yaani jamaa linavyochekelea ni kama linawaona wa TZ wote ni mafara vile.
 
Hilo ni tatizo la kiutendaji zaidi kwa upande wa DPP. Kwanini anapeleka kasi mahakamani bila kukusanya ushahidi wa kutosha ? mimi naona anafanya kazi kisiasa zaidi kwa kutaka kuufurahisha umma wa waTanzania kuwa amemfikisha mahakamani mtuhumiwa wakati anajuwa wazi hana ushahidi madhubuti wa kuweza kumtia hatiani mtuhumiwa na mwisho wa siku ku loose.

Poleni sana waTz
 
Hili ni dili limepangwa ili kesho tuambiwe kua watuhumiwa wa Richmond walifikishwa mahakamani
 
Sishangai sana, this was expected. Bado ya Mramba na wenzie wataachiwa soon kwasababu ya kitu kile kile "Serikali haijapeleka ushahidi wa kutosha" Infact kesi nyingi hizi zinazousisha vigogo wa serikali hufunguliwa kama kiini macho kwa watanzania; lakini ukweli ni kwamba serikali haipeleki ushahidi wowote mahakamani; ikijitahidi sana itapeleka weak evidence hivyo hakimu/jaji analazimika kumuachia mshtakiwa.
 
Its amazing how the so called GREAT THINKERS wa Jamii Forum wanavyotaka utekelezaji wa MOB JUSTICE

Kesi zote hizi za rushwa zilizopelekwa Mahakamani zimejaa uonevu INCLUDING ile ya jengo la BOT

kwa sababu upande wa mashtaka uko bize kutoa leaks after leaks kwa media sasa hata kama kungekuwa na kesi ya kujibu lakini katika hii hali ya mob mentality walionayo media in Tanzania na sasa hii cancer ishaspread humu JF kusingekuwepo kwa utowaji wa haki.

I agree na jaji aliyetoa hii hukumu
 
Serikali yetu kama inataka mhalifu wao alindwe wana mbinu nyingi sana, kwani system yetu ya sheria ni kwamba serikali ndiyo mshitaki mkuu kwa kesi zote za jinai.

Hivyo basi kwa kutimiza uminywaji huo wa haki wanapeleka mahakamani mshitakiwa siyo, au mashitaka siyo, au mashahidi siyo, au ushahidi siyo!

Mara nyingine hata mahakimu wawe waadilifu namna gani -- wanachezewa tu na serikali katika kamchezo ka namna hiyo! Serikali inayo uwezo wa hata kuiondoa kesi iwapo itaona mhalifu wao anaelekea kwenda na maji.
 
Kweli kabisa! Iko mifano mingi ya unachokisema. Kesi dhidi ya waliotaka kumuuwa/kumpofua macho Kubenea ilianguka kwa sababu serikali haikuwa na nia ya kuona watuhumiwa hasa waliopanga shambulio hilo wangejulikana. Hivyo Tibaigana aliagizwa kuivurunda kwa kufanya upelelezi wa h
ovyo na pia kupeleka washitakiwa siyo na mashahidi siyo.

Yote hii ilimuradi tu serikali ionekane imetimiza jukumu lake la kuwapeleka wahalifu wote mahakamani!

Mfano mwingine ni ile kesi ya mauaji dhidi ya Wahindi wawili waliowachoma moto Waafrika wawili katika miaka ya tisini. Washitakiwa waliachiliwa na jaji alisema kuwa hajawahi kuona ushahidi mbovu iliopelekwa kuhusu kesi ya mauaji kama wa kesi hiyo.
 
maigizo yanaendelea

Yees, yanaendelea! Nauliza -- hivi yule Muhindi wa radar -- Vithlani aliyewahi kukamatwa na kufikishwa mahakamani aliachiliwa kwa misingi gani? Nachokumbuka ni kwamba hakushitakiwa kwa kosa la kuwaingizia Watz hasara ya mabilioni -- ila alishitakiwa kwa kusema uongo kwa wachunguzi wa kesi hiyo!

THIS IS A REAL B.F. COUNTRY!!
 
Gire akitoka
makamani leo

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mjini Dar es Salaam, imemwachia huru Naeem Gire aliyekuwa akikabiliwa na kesi ya kughushi na kuwadanganya serikali kuwa mitambo ya Richmond ina uwezo wa kufua megawati 100 za umeme.

Gire ametoka kizimbani akichekelea baada ya hakimu wa mahakama hiyo, Waliarwande Lema , kutamka kuwa anamuona hana kesi ya kujibu kutokana na ushahidi uliofikishwa mahakamani na serikali kushindwa kumridhisha ili amuone kuwa na kesi ya kujibu.

"....Baada ya kupitia ushahidi katika vipengele vyote nimeona kuwa hakuna ushahidi wa kutosha uliowasilishwa kuridhisha kumuona mshitakiwa ana kesi ya kujibu...kesi hii ni miongoni mwa kesi kadhaa ambazo huletwa mahakamani na kisha kuitwisha lawama mahakama", alisema Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Waliarwande Lema."

Rushwa kila mahali. Tumekwisha, hata mahakama jamani. Na kesi kama hizi sio kuwapa magistrates. Full bench tungeelewa, sio vingine. Utafiti wangu usio rasmi unanionyesha kuwa kesi nyingi zinazoshinda kwa magistrates, Court of appeal huwa zinatupwa and vice versa. Mahakimu msiniue, sijaingilia uhuru wa mahakama. natoa matokeo ya uchunguzi wangu usio rasmi
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom