Mahakama yaamuru upelelezi kesi nguli dawa za kulevya uharakishwe

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,315
33,111
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imeuamuru upande wa mashtaka kuharakisha upelelezi wa kesi inayowakabili wafanyabiashara wanane wa jijini Dar es Salaam, akiwemo nguli wa biashara ya dawa za kulevya, Mwanaidi Ramadhani, ya kuingiza dawa hizo aina ya Cocaine, kilo 5 zenye thamani ya Sh. milion 225, ili haki iweze kutendeka kwa pande zote mbili.

Mbali na nguli huyo, washtakiwa wengine ni, Sara Daud, Anthony Karanja, Ben Ngare, Almas Said, Yahaya Ibrahim, Aisha Kungwi na Rajabu Mzombe ambao wamefikishwa katika mahakama hiyo, jijini Dar es Salaam.

Hakimu Agustina Mbando alitoa amri hiyo jana baada ya upande wa utetezi kulalamika kwamba upelelezi wa kesi hiyo unachelewa na kwamba washtakiwa wanateseka mahabusi kwa muda mrefu.

Hata hivyo, Wakili wa Serikali, Keneth Sekwao, alijibu hoja hiyo akisema kwamba kama upande wa utetezi umeona upelelezi unachelewa waandike barua Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini (DPP) kueleza malalamiko hayo.

Hakimu Mbando alisema upande wa mashtaka uharakishe upelelezi ili washtakiwa na Jamhuri waweze kupata haki yao katika kesi hiyo.

Mapema mwaka jana Wakili wa Serikali, Patrick Malogoi, alidai kuwa Juni Mosi, mwaka jana, eneo la Mbezi Beach, Wilaya ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam, washtakiwa walikamatwa wakiingiza dawa za kulevya aina ya Cocaine.

Hata hivyo, washtakiwa hawakutakiwa kujibu chochote kutokana na dawa walizokamatwa nazo kuwa na thamani ya zaidi Sh. milioni 10, ambapo mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi yao.

Kesi yao itasikiliza Mahakama Kuu Tanzania, mara upelelezi wake utakapokamilika.
Kesi hiyo itatajwa Februari 14, mwaka huu.



CHANZO: NIPASHE
 
kwangu hilo ni changa la macho.
kesi za dawa za kulevya kwa hii nchi zinaishiaga juu juu tu
 
Mimi nilifikiri huyu mama alisha sepa kumbe bado yuko lupango!!Naona dau lake lilikuwa dogo ama sivyo angekwisha achiwa kama yule Akasha wa Mombasa aliyeachiwa enzi ya Mzee Ruksa!!
 
Back
Top Bottom