Mahakama yaamuru Mbowe akamatwe mara moja

Utawala wa sheria lazima ufuatwe. Na amri za mahakama ni lazima zitekelezwe na kuheshimika.

hakuna siasa katika sheria kwani sheria ni msomeno.

Mbowe acha dharau
 
Ndugu Wana JF,

Hakimu kutoa arrest warrant sio jambo geni wala sio issue kuubwa na sio lazima Mh. Mbowe akamatwe, kinachotakiwa ni kuwasilisha utetezi kwa nini yeye au mdhamini wake alishindwa kufika mahakamani.

Nakumbuka wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu october 2010, Endrew Chenge ambaye ni mbunge wa bariadi marufuu kama mzee wa vijicenti alikuwa anatakiwa kuhudhuria mahakamani kwenye kesi yake ya mauji lakini hakuweza kuhudhuria mahakamani kwa sababu JK alikuwa jimboni kwake anampigia kampeni siku hiyo

Hakimu Sundi Fimbo alitoa arrest warrant kwamba Endrew chenge akamatwe kwa kutohudhuria mahakamani na kudharau mahakama! sisi sote mashahidi, je amri ya mahakama ilitekelezwa? kama alivyoagiza hakimu sundi fimbo? Chenge hakuwa na sababu yoyote ya msingi ya kutohudhuria mahakamani kwani alionekana jukwaani na JK akimpigia kampeni! Je ni kwa nini chenge hakukamatwa na ni sababu ipi ilimlidhisha hakimu Sundi Fimbo na ku withdraw arrest warrant wakati ni kweli chenge alidharau mahakama na kuona kampeni yake ni muhimu kuliko kuhudhuria mahakamani?

Nitashangaa sana kama hakimu Magesa atatumiwa kisiasa na kupuuza utetezi wa bwana mbowe au mdhamini wake wakati kuna watu kama Endrew Chenge ambae ni AG mstaafu na anaijua sheria vizuri alipuuza mahakama na hakimu fimbo let him go unpunished, Uwezo wa hakimu kufanya maamuzi ni pamoja na kutumia busara mbowe ana majukumu mengi ya kitaifa ikiwa pamoja na kujiandaa na bunge la bajeti yeye akiwa kama waziri mkuu kivuli bungeni. Hivyo ni matumaini yangu hiyo arrest warrant will not hold water for the sake of court credibility.

Nimeikubali mkuu
 
Makahama mjini Arusha imetoa arrest warrant ili Mh. Freeman Mbowe akamatwe. Mbowe hakuwepo mahakamani na wala mdhamini wake hakuwepo. Ndesamburo kaponea chupuchupu kutokana na mdhamini wake kuwasili mahakamani.

Dr. Slaa alikuwepo mwenyewe na Lema alikuwepo mwenyewe pia.

===========
UPDATES:

From AFP:

Tanzania judge urges arrest of opposition leader

A Tanzanian judge on Thursday urged police to execute an arrest warrant issued last week against the country's opposition leader in parliament, lawmaker Freeman Mbowe.

Mbowe, who is president of the main opposition Chadema party, and 18 others are being prosecuted in an Arusha court for conspiracy to commit an offence, unlawful assembly and rioting.

Judge Charles Magesa issued arrest warrants for Mbowe and six others on May 27 when they failed to appear in court for a hearing on their case, which has been repeatedly delayed.

Magesa withdrew the warrants for everyone but Mbowe after the others appeared in person or sent representatives to explain their failure to show up for the previous hearing.

"The arrest warrant has not been executed and (Mbowe) did not come to explain why he was absent," Magesa said at an open hearing on the case.

He then instructed "the police to ensure that he be arrested."

The charges stem from a January 5 opposition rally in Arusha that was dispursed violently by police where three people were killed by gunfire.

Chadema Secretary General Wilbrod Slaa, a loser in the country's October presidential election and a Chadema lawmaker face additional charges for demanding that President Jakaya Kikwete resign

Nimeshangazwa sana Mbowe kutojua sheria kiasi hiki, hivi kweli hawa ndio tuwape mamlaka ya dola kweli aisee. Kwenye hili aiombe tu mahakama radhi , na kuwa hatarudia tena . Huku ni kuidharau mahakama wazi wazi asitafutwe mchawi kabisaa, hata kama ni mbunge hana kinga ya kutofika mahakamani yeye pamoja na mdhamini wake
 
Kumtukana Hakimu pia ni kosa la jinai kama hukubaliani na uamuzi wake njia sahihi ni kuukatia rufaa katika ngazi ya juu. Mbowe anaweza kweli akawa na shughuli muhimu iliyomzuia asifike Mahakamani lakini taarifa lazima ipelekwe Mahakamani.

Hii inaonyesha hata akija kuwa Rais kama mnavyomtaka atakuwa tayari kufuata utawala wa sheria?

Au anataka kutuambia hatambui taratibu za Mtuhumiwa kufika Mahakamani?

Tuache ushabiki wa kijinga kwa hili halijakaa vizuri mpaka hapo tutakapopata maelezo mengine na naamini Mbowe atakuja na maelezo ya kumsafisha.

si akimu 2 mtuyeyote hasitaili kumtukana ukijiangalia kwenye kiokichafu utajiona mchafu kamaunataka kuelimisha jam jielimishe mwenyewe kwanza unakataza matusi uku unaenzi matusi tujifunze nini? Toka kwako
 
ipo siku hii nchi hapatakuwa na mahakama wala magereza kwa sababu ya upuuzi kama huu unaoendelea sasa na ndugu yenu mwenye kilema cha kuchekacheka. Tutafika kipindi itakuwa zaidi ya somalia kwa sababu ya upuuzi wa ZZM
 
Mahakama za kitanzania vituko tu hiyo kesi ya kinambowe mpaka lini, mwisho wake tutasikia hawana hatia muda mwingi unapotea hakuna lolote la maana.
 
Back
Top Bottom