Mahakama ya Rufaa yashtumiwa kujipa mamlaka

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,173
Mahakama ya Rufaa yashtumiwa kujipa mamlaka


Na Makumba Mwemezi

WAKILI Mwandamizi wa Mahakama Kuu Bw. Richard Rweyongeza ameishambulia Mahakama ya Rufaa kwa kujaribu kujipa mamlaka yasiyo ndani ya
sheria, katika kuitisha shauri kutoka Mahakama Maalumu ya Rufaa za Kijeshi kwa ajili ya rejea.

Kwa mujibu wa kanuni za nidhamu za jeshi, Mahakama Maalumu ya Rufaa za Kijeshi ndiyo ya juu na ya mwisho kwa mashauri yote ya jinai.

Katika hali iliyowashangaza wengi na kwa mara ya kwanza katika historia ya usimamizi wa sheria na utoaji haki nchini, mwishoni mwa wiki Mahakama ya Rufaa iliitisha shauri lililokwisha tolewa maamuzi na Mahakama ya Rufaa za Kijeshi, kwa lengo la kupitia upya uamuzi ulimpa ushindi mrufani.

Kwa mujibu wa Sheria ya Ulinzi wa Taifa (National Defence Act) No.192 ya 2002) na Kanuni za nidhamu za jeshi (The Code of Service Discpline), mashtaka yoyote ya jinai katika masuala ya kijeshi, huamuliwa na Mahakama za Kijeshi (Court Martial) na rufaa zake hupelekwa Mahakama Maalumu ya Rufaa za Kijeshi (Court Martial Appeal Court) na si Mahakama ya Rufaa.

Hatua ya Mahakama ya Rufaa inatokana na uamuzi wa Mahakama Maalumu ya Rufaa za Kijeshi, kumfutia mashtaka na adhabu mrufani P9219 LT Abdon Rwegasira ambaye awali alionekana kuonewa na Mahakama ya Kijeshi iliyomkuta na hatia na kumuhukumu kifungo cha mwaka mmoja jela na kumwachisha kazi kwa kosa la kukiuka kanuni za nidhamu za jeshi.

Akitoa hoja za pingamizi dhidi ya mamlaka ya Mahakama ya Rufaa kurejea shauri hilo, Wakili Rweyongeza anayemtetea LT Rwegasira, alidai kuwa kifungu cha 153C cha Kanuzi za nidhamu za jeshi, zinatoa Mamlaka kwa Mahakama Maalumu ya Rufaa za Kijeshi kuwa mahakama ya juu na ya mwisho kwa rufaa zote kutoka Mahakama ya Kijeshi.

Alisema Mahakama ya Rufaa imekosea na haina mamlaka ya kusikiliza rufaa au rejea kutoka Mahakama Maalumu ya Rufaa ya Kijeshi kwa kuwa imepewa mamlaka ya kusikiliza rufaa kutoka Mahakama Kuu tu, na kuwa Mahakama Maalumu ya Rufaa za Kijeshi si sehemu ya Mahakama Kuu.

"Ibara ya 117(3) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na kifungu cha 4(2) na (3) cha sheria ya Mamlaka ya Mahakama ya Rufaa, vinaeleza wazi kuwa majukumu na mipaka ya Mahakama hiyo itakuwa kusikiliza na kuamua shauri lolote kutoka Mahakama Kuu, na tafsiri ya mahakama Kuu haijumuishi Mahakama maalumu ya Rufaa za kijeshi," alidai Bw. Rweyongeza.

Alisema Sheria hiyo pamoja na katiba ya nchi zimekuwa zikifanyiwa marekebisho mara kwa mara wakati Mahakama ya kijeshi ikiwepo, lakini hakuna mabadiliko yaliyoitaja Mahakama Maalumu ya Rufaa za Kijeshi kuwa sehemu, au na hadhi sawa na Mahakama Kuu, hivyo kuiomba Mahakama ya Rufaa kulitupilia mbali ombi la upande wa waombaji.

Kabla ya kukata rufaa katika Mahakama Maalumu ya Rufaa za Kijeshi P9219 LT Rwegasira, alikutwa na hatia na kuhukumiwa kifungo cha mwaka mmoja katika jela za kiraia kwa kukiuka kanuni za nidhamu za jeshi, jambo ambalo ni kosa la jinai kwa taratibu za jeshi.

Upande wa waombaji rufaa wakiongozwa na LT Kanali Fransis Mbindi, walisema pamoja na ukweli kuwa hakuna sheria inayoipa mamlaka Mahakama ya Rufaa kusikiliza rufaa au rejea kutoka korti za kijeshi, lakini inayo mamlaka yasiyo na mipaka kuamua jambo lolote linalohusu uvunjifu wa sheria na wa amani katika nchi.

Wakiahirisha kesi hiyo iliyovuta usikivu wa raia wa kawaida na waandishi wa habari, Jopo la majaji wa rufani wanaosikiliza kesi hiyo wakiongozwa na Jaji Eusebia Munuo, walisema kutokana na uzito wa kesi na hoja za pande zote mbili, kesi itaahirishwa ili wapitie hoja hizo na itapangiwa tarehe ya kutoa hukumu na pande zote zitafahamishwa.

 
PHP:
Kwa mujibu wa kanuni za nidhamu za jeshi, Mahakama Maalumu ya Rufaa za Kijeshi ndiyo ya juu na ya mwisho kwa mashauri yote ya jinai.

Nchii hii inaongozwa na kanuni au katiba?

kwenye katiba yetu Mahakama ya Rufaa ndiyo muhimili wa mwisho................sasa kanuni za mahakama za kijeshi zina ubavu wa kuupindua ukweli huo?
 
Back
Top Bottom