zomba
JF-Expert Member
- Nov 27, 2007
- 17,240
- 3,910
Jana, (ingawa sikusikia jibu lote) kipande kidogo nilichokisikia kinanifanya ni sadiki kuwa Mheshimiwa Waziri Mkuu Mizengo Kayanza Pita Pinda alipokuwa akijibu hoja za bajeti jana jioni kaonesha kuridhia kwa Serikali kuanzishwa tena kwa Mahakama ya Kadhi baada ya kufungiwa kwa muda mrefu na aliyekuwa Rais wa kwanza wa Tanganyika (na baadae Tanzania) Julius Kambarage Nyerere.
Tunawapongeza Watanzania wote kwenye haya maamuzi mazuri yaliyofanywa na Serikali ya Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete. Kuwarudishia Waislaam Kadhi na mahakama ya Kadhi ni katika kuwapa uhuru wao wa kuabudu uliodhulumiwa na utawala wa awamu ya kwanza.
Tunatumai mchakato wa kuzirudisha mahakama za kazi utakuwa wa kasi zaidi.
Hongera Waislaam, Hongera Kikwete, Hongera Pinda, Hongera Watanzania.