Mahakama ya Bima kuanza kazi soon

NgomaNzito

JF-Expert Member
Jan 10, 2008
559
26
Mahakama ya Bima inatarajiwa kuanzishwa nchini wakati wowote kuanzia sasa. Katika mahakama hiyo, wateja watafungua kesi iwapo hawataridhika na malipo mbalimbali ya bima wanayolipwa na kampuni husika. Kwa sasa, Afrika Kusini ndiyo pekee yenye mahakama ya aina hiyo barani.

Akizungumza na waandishi wa habari jana kuhusu mkutano mkuu wa mwaka wa Umoja wa Watendaji wa Bima barani Afrika utakaofanyika Dar es Salaam mwezi ujao, Kamishna wa Bima nchini, Israel Kamuzora, alisema katika mahakama hiyo haki itakuwa inatolewa siku hiyohiyo baada ya Jaji kusikiliza malalamiko yaliyowasilishwa na mteja.

Kamuzora alisema katika Afrika, asilimia tano hadi sita ya wananchi ndio wanaopata huduma ya bima na kuongeza: “tena wanaoishi mijini na wanakata bima ya magari na nyumba, lakini hawakati ya maisha ambayo ni muhimu”.

Duh!! hii itakuwa bomba sana yaani siku hiyohiyo hukumu saafi sana tutapata fidia zetu wanazotudhulumu wadhulumati hao
 
Back
Top Bottom