Mahakama nchini Zimbabwe imesitisha harusi ya Waziri Mkuu wa Zimbabwe Morgan Tsvangirai

R.B

JF-Expert Member
May 10, 2012
6,296
2,573
Mahakama imesema kuwa Tsvangirai tayari ana mke.
Lakini sasa Hakimu amekubaliana na Locadia na kuamuru harusi iliyopangwa kufanyika siku ya Jumamosi haitafanyika tena.
Hii ni licha ya baadhi ya viongozi wa nchi mbali mbali walioalikwa kwa harusi kuwasili nchini humo.
Mawakili wa Tsvangirai wanataka mahakama kutoa amri ya dharura na kuruhusu harusi hiyo kuendelea kama ilivyopangwa.
Kesi nyingine ambayo mahakama ilisikiza leo dhidi ya Tsvangirai ni ya mwanamke mmoja kwa jina Nozipho Shilubane aliyesema kuwa Waziri Mkuu huyo aliahidi kumuoa.
Baadhi ya wadadisi wanasema kuwa kesi hiyo ni dalili ya njama za kisiasa kumpaka tope waziri mkuu kabla ya uchaguzi mkuu utakaofanyika mwaka ujao. Tsvangirai atatoana jasho na rais Robert Mugabe katika uchaguzi huo.
Lakini wengine wanasema kuwa Tsvangirai hana wa kulaumu ila yeye mwenyewe kwani amejihusisha na wanawake wengi baada ya mke wake kufariki katika ajali ya barabarani mwaka 2009 baada ya waziri mkuu kuchukua wadhifa wake.
Mwandishi wa BBC Brian Hungwe mjini, Harare, anasema kuwa harusi hiyo ilipangwa kufanyika katika mtaa mmoja wa kifahari mjini Harare.
Rais Mugabe anatarajiwa kuandaa dhifa maalum kwa viongozi wa nchi za kiafrika walioalikwa kuhudhuria.
 
Umenikumbusha kitu,ivi ile ya Slaa ilifanyika? Maana nayo niliishia kusikia imewekewa pingamizi mahakamani kisha ikawa kimyaaaaa! Pia nina swali:serikali ambayo haina dini inapata wapi power ya kuzuia ndoa inayofungiwa kanisani ?na hali ya kuwa ilipaswa kufanywa kanisani.
 
Umenikumbusha kitu,ivi ile ya Slaa ilifanyika? Maana nayo niliishia kusikia imewekewa pingamizi mahakamani kisha ikawa kimyaaaaa! Pia nina swali:serikali ambayo haina dini inapata wapi power ya kuzuia ndoa inayofungiwa kanisani ?na hali ya kuwa ilipaswa kufanywa kanisani.

Swali la pili...... Ndoa zote hata zikifungwa kanisani au msikitini ni lazima ziwe na kibali cha serikali. Kwa maana nyingine wachungaji au padri n.k wanafungisha ndoa kama tu wamepewa mamlaka na serikali...mambo mengine yanayoongezeka huwa ni imani tu.
 
Back
Top Bottom