Mahakama nchini Zimbabwe imeamuru wapinzani waendelee na maandamano leo

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,557
21,511
Mahakama ya kuu nchini Zimbabwe imeamua kuwa maandamano ya ya makundi ya upinzani yanaweza kuendelea hii leo, kuanzia saa sita mchana.

Jana polisi walionya kuwa maandamano yoyote ambayp hayajaidhinishwa hayatakubalika.

Polisi kikosi cha kutuliza ghasia tayari wametumia gesi za kutoa machozi dhidi ya makundi madogo ya watu waliokuwa wakijiandaa kwa maandamano.

Maandamano ya leo yameandaliwa na makundi kadhaa ya upinzani yaliyo katika muungano unaojiita NERA - unaodai mageuzi ya sheria za uchaguzi - wanaosema wanataka kufana maandamano ya amani kutoa wito wa kufanya mabadiliko ya sheria ya uchaguzi .

Zimbabwe imekua ikishuhudia maandamano makundi makubwa ya umma katika kipindi cha miezi kadhaa, zaidi yakielezea kutoridhishwa na hali ya uchumi wa nchi yao uliodidimia.

Chama kikuu cha upinzani cha MDC na upinzani mpya unaoongozwa na makamu rais wa zamani Joice Mujuru wa chama cha Zimbabwe People First,ni miongoni mwa makundi yanayoshiriki maandamano ya leo.

Chanzo: BBC Swahili
 
Why not Tanzania?!!! Come on UKUTA
wenzenu wamefata utaratibu unaokubalika ambao ni mahakamani nyinyi mnataka kutumia nguvu pamoja na kujifanya chama cha wasomi na mabigwa wa sheria mnavuja sheria kwa kulazimisha maandamano yaliopigwa marufuku na vyombo vnavyohusika na ulinzi na usalama wenu wakat mnafanya ayo maandamano cdhani kama maandamano ya amani yanakuwaga na maneo hatukubali,lazima,aiwezekani,tuafanya tu na maneno mengi yanayo hamashisha uvunjifu wa amani sasa ni hv kama mnadhani mtaitwa ikulu kunywa juice nadhani sehemu inayowafaa ni hospital na segerea kwa watakao kamatwa cku hyo
 
Why not Tanzania?!!! Come on UKUTA

Jirani Kenya muungano wa vyama vya upinzani wa CORD walitumia mahakama zao wakaruhusiwa kuandamana, Zimbabwe ndi hiyo leo, kwani sisi hapa Tz kwa nini wasitumie mahakama kulinda haki ya kikatiba?!
 
Mahakama Gani Mkuu?? Hizi hizi au kuna ingine?
 
wenzenu wamefata utaratibu unaokubalika ambao ni mahakamani nyinyi mnataka kutumia nguvu pamoja na kujifanya chama cha wasomi na mabigwa wa sheria mnavuja sheria kwa kulazimisha maandamano yaliopigwa marufuku na vyombo vnavyohusika na ulinzi na usalama wenu wakat mnafanya ayo maandamano cdhani kama maandamano ya amani yanakuwaga na maneo hatukubali,lazima,aiwezekani,tuafanya tu na maneno mengi yanayo hamashisha uvunjifu wa amani sasa ni hv kama mnadhani mtaitwa ikulu kunywa juice nadhani sehemu inayowafaa ni hospital na segerea kwa watakao kamatwa cku hyo
Baada ya polisi kuzuia ndio wakaenda mahakamani.
 
Jirani Kenya muungano wa vyama vya upinzani wa CORD walitumia mahakama zao wakaruhusiwa kuandamana, Zimbabwe ndi hiyo leo, kwani sisi hapa Tz kwa nini wasitumie mahakama kulinda haki ya kikatiba?!
mahakama ishapiga chini kesi yao
 
Back
Top Bottom