Mahakama mkoani kigoma yatoa hukumu ushindi wa PETER SERUKAMBA

source plz!!!!! maana leo ijumaa kuu public holiday mahakama hazifanyi kazi, au umeota?
 
Siku hizi haki inanunuliwa mahakamani kwahiyo maskini hana haki; mahakama zilikuwa na haki enzi ya chief Justice Barnabas Samatta alipokuwa na makamanda majaji marehemu James Mwalusanya na Lugakingira basi. Majaji wanateuliwa kwa kufuata dini zao na sio ujuzi wa sheria heshima ya mahakama itatoka wapi?
 
nafikiri kuna watu huwa wanakurupuka sana na kujitungia ndo maana baada ya kumbiwa leo ijumaa amekimbia hajarudi tena..sitashangaa serukmba kushinda kesi hiyo ila nitashangaa kama angeshinda siku ya ijumaa kuu ambayo si siku ya kazi
 
CCM haitokufa wewe ila CDM ndio itakufa kifo cha mende 2015. Vijana wa CCM na wanajeshi ndio walioingia vitani kupigana na nduli na kukamng'oa sembuse CDM ? tunaivutia kasi tu
 
CCM haitokufa wewe ila CDM ndio itakufa kifo cha mende 2015. Vijana wa CCM na wanajeshi ndio walioingia vitani kupigana na nduli na kukamng'oa sembuse CDM ? tunaivutia kasi tu

Unajivunia vita iliyotutia umaskini! Mimi nimeshiriki vita hiyo nikiwa 501kj na sina hamu na ccm! Nimeapa kuwa nikiipa kura yangu ccm basi NILAANIWE MIMI NA KITUO CHA KUPIGIA KURA!
 
Haki iko kwa Mungu tu, hapa duniani ni usanii haijalishi amesoma au hakusoma, Na hasa Tanzania,Adhabu ya Mungu juu ya Tanzania iko palepale,
 
Haki iko kwa Mungu tu, hapa duniani ni usanii haijalishi amesoma au hakusoma, Na hasa Tanzania,Adhabu ya Mungu juu ya Tanzania iko palepale,
 
Hii hukumu ya Mheshimiwa Peter Serukamba imetolewa kama wiki moja iliyopita na Jaji Mwanamke katika mahakama ya Kigoma iliyoko karibu na ofisi za mkuu wa mkoa na central polisi lakini mleta uzi anazungumza kana kwamba hukumu imetolewa leo, kwanza mwawakili wa CDM waliambiwa warekabishe charge sheet yaani hati ya mashitaka, mwanzo ilikuwa inamshitaki mbunge pekee kwamba amewaibia kura, Jaji aliwaeleza kwamba mshitakiwa hawezi kuwa mbunge pekee bila ya msimamizi wa uchanguzi yaani Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji Bw. Lewis Kalinjuna( kwa amehamishiwa Korogwe) na vile vile waainishe ni kura kiasi gani wameibiwa. Sasa siku ya hukumu sikupata vizuri ni sababu zipi zilizompa ushindi Serukamba ila nilisilia kwamba picha za video zilizochukuliwa zilikataliwa. Ila cha msingi hukumu hii haijatolewa leo Ijumaa kuu kwani habari hii imshawahi kuwekwa hapa JF. Lakini hata hivyo naona CDM waliweka mawakili ambao ni incompetence, ingawa upande wa washitaki walimkataa Jaji bila ya mafanikio.
 
CCM haitokufa wewe ila CDM ndio itakufa kifo cha mende 2015. Vijana wa CCM na wanajeshi ndio walioingia vitani kupigana na nduli na kukamng'oa sembuse CDM ? tunaivutia kasi tu

Acha ujuha wewe, walioingia vitani kumng'oa NDULI ni Watanzania wote,
Hauna leseni ya kusema ni vijana wa CCM na wanajeshi tu, hata Mgambo, Polisi, Sungusungu, na wananchi walijitolea kushiriki vita hiyo ya kizamani ........
 
Sasa hao majaji na mahakimu wa bongo, si waanze tu kuvaa magwanda ya kijani, wanasubiri nini, na huko Arusha mpelekeeni huyo jaji zawadi ya gwanda la kijani, ili afurahi zaidi.
 
Eti Batilda alitukanwa wapiga kura wake wakachanganyikiwa badala ya kumpigia Batilda wakampigia Lema.
Mahakama feki kabisa pumbavu zao hao! natamani kumla mtu nina hasira sana!
 
Back
Top Bottom