Mahakama mkoani kigoma yatoa hukumu ushindi wa PETER SERUKAMBA

Wa kusoma

JF-Expert Member
Jul 30, 2011
3,454
2,975
Mahakama ya mkoani kigoma imetoa hukumu ya kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi yaliyompatia ubunge ndg. Peter Serukamba wa CCM dhidi ya All Khalfan Mleeh wa CHADEMA. Mahakama imetupilia mbali ombi la mgombea wa cdm na kusema hana vielelezo vya kutosha kumvua ubunge mh. Serukamba kijana mtiifu kwa Lowasa.

Tayari magari ya washawasha na askari wenye mabomu ya machozi na silaha za kivita wanarandaranda mtaani ili kuzima vuguvugu la watu wanaotaka kuandamana.

Source: niko kigoma kikazi.
 
Mhmh, kama ni kweli basi huu utakuwa ni mwaka wa aibu sana kwa uhuru wa Mahakama. Sidhani kama kuna mtu atakayebakia kuwa na imani na hizi mahakamasisiemu. Kama Mahanga naye atashinda sitakuja kwenda mahakamani hadi hapo ccm itakapokufa. Mungu saidia ccm ife 2015 ili watanzania hawa wapate sehemu yenye kutoa haki
 
kama kwa mazingira ya kesi ya lema amevuliwa ubunge unaona ugumu gani kwa mahakamasisiem kumpa ushindi serukamba?
unaona ugumu gani kwa mahakaa sisisem kumpa ushindi mahanga.
ishu ni kua kwa sasa ndo sisiem wanakata roho, kwa hiyo ni kama wapo frustrated, hata aibu hawaoini tena, hata
akili zao katika kufocus zishakua butu sana. manake kwa mtu mwenye akili kesi ya lema angeshinda ingeweka mazingira mazuri ya mahanga na serukamba kushinda bila maswali mengi hata kaa walistahii kushindwa.
lakin wao hawaoni kua kutomtendea lema haki knazidi kuwafungua wengi macho.
 
Hakika CCM ni wasanii sana wacha waendelee na usanii wao kama comedy vile lakini kutahamaki 2015 hiyo ndiyo unakuwa mwisho wao.
 
Mi nipo Kigoma tena baada ya kupata hii habari nimezungukia maeneo ya mahakamani na mwanga sokoni na ila sijasikia kitu kama hicho, hata hao askari sijawaona.
 
Mahakama ya mkoani kigoma imetoa hukumu ya kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi yaliyompatia ubunge ndg. Peter Serukamba wa CCM dhidi ya All Khalfan Mleeh wa CHADEMA. Mahakama imetupilia mbali ombi la mgombea wa cdm na kusema hana vielelezo vya kutosha kumvua ubunge mh. Serukamba kijana mtiifu kwa Lowasa.

Tayari magari ya washawasha na askari wenye mabomu ya machozi na silaha za kivita wanarandaranda mtaani ili kuzima vuguvugu la watu wanaotaka kuandamana.

Source: niko kigoma kikazi.
endeleaga kusoma wa kusoma.:heh:
 
Kwa mahakama za tanzania tusitegemeee hata siku moja CDM kupata ushindi, labda kwa majaji walio watiifu kwa kazi zao. lakini majaji wengi ni vibaraka wa magamba. unategemea serukamba kijana mtiifu kwa lowasa avuliwe ubunge?
 
Wao watatumia polisi, mahakama, jeshi na fedha lakini wananchi tutatumia sanduku la kura kuiangamiza CCM 2015. Kuna kila dalili kuwa wananchi wamechoka na ccm haikubaliki, tushirikiane kuitokomeza
 
Back
Top Bottom