Mahakama Kuu yafuta kesi ya madai dhidi ya Askofu Kakobe kwa kukosa mashiko

gumegume

JF-Expert Member
Jun 29, 2011
1,063
617
Juzi, Alhamisi 1.12.2016, Jaji Mwandambo wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Dar-Es-Salaam; alifuta kesi ya madai Na.79 ya mwaka 2011 dhidi ya Askofu Mkuu Zachary Kakobe wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF), kwa kuona kwamba haina mashiko.

Wadai katika kesi hiyo walikuwa watatu, Dezydelius Patrick, Angelo Mutasingwa, na Benedict Kaduma, ambao hapo zamani walikuwa Wachungaji wa Kanisa hilo. Katika kesi hiyo, wadai hao, pamoja na mambo mengine, walidai kwamba Askofu Kakobe alifanya ubadhirifu wa zaidi ya shilingi 14 bilioni.

Katika utetezi, Miriam Majamba ambaye ndiye alikuwa Wakili wa Askofu Kakobe, aliwasilisha vielelezo na kueleza kwamba, Bodi ya Wadhamini ya Kanisa hilo la FGBF, iliwafukuza wadai hao, katika Uchungaji na ushirika wa Kanisa hilo, mwaka 2010. Dezydelius alifukuzwa tarehe 10.9.2010, kutokana na matukio mengi ya utapeli na ubadhirifu, katika Kanisa la FGBF MAFINGA, alilokuwa akiliongoza, na pia utapeli alioufanya kwa waumini wa Kanisa la FGBF Dar-Es-Salaam, Wynn-Jones Kapaliswa na Rhodius Nsaro, aliowatapeli zaidi ya shilingi 34 milioni.

Angelo aliyekuwa Mchungaji wa Kanisa la FGBF NZEGA, alifukuzwa Uchungaji, tarehe 6.7.2010, kutokana na ukosefu wa maadili, na vilevile Benedict aliyekuwa Mchungaji wa Kanisa la FGBF BABATI, alifukuzwa Uchungaji, tarehe 23.3.2010, kwa ukosefu wa maadili.

Baada ya Wachungaji hao kufukuzwa katika Kanisa hilo, walishirikiana na kupanga mkakati wa kumgeuzia kibao Askofu Kakobe, kwa kutunga madai ya uongo dhidi yake, ili kumchafua; na hatimaye kufungua kesi hiyo ya madai tarehe 26.5.2011.
 
Juzi, Alhamisi 1.12.2016, Jaji Mwandambo wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Dar-Es-Salaam; alifuta kesi ya madai Na.79 ya mwaka 2011 dhidi ya Askofu Mkuu Zachary Kakobe wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF), kwa kuona kwamba haina mashiko. Wadai katika kesi hiyo walikuwa watatu, Dezydelius Patrick, Angelo Mutasingwa, na Benedict Kaduma, ambao hapo zamani walikuwa Wachungaji wa Kanisa hilo. Katika kesi hiyo, wadai hao, pamoja na mambo mengine, walidai kwamba Askofu Kakobe alifanya ubadhirifu wa zaidi ya shilingi 14 bilioni.

Katika utetezi, Miriam Majamba ambaye ndiye alikuwa Wakili wa Askofu Kakobe, aliwasilisha vielelezo na kueleza kwamba, Bodi ya Wadhamini ya Kanisa hilo la FGBF, iliwafukuza wadai hao, katika Uchungaji na ushirika wa Kanisa hilo, mwaka 2010. Dezydelius alifukuzwa tarehe 10.9.2010, kutokana na matukio mengi ya utapeli na ubadhirifu, katika Kanisa la FGBF MAFINGA, alilokuwa akiliongoza, na pia utapeli alioufanya kwa waumini wa Kanisa la FGBF Dar-Es-Salaam, Wynn-Jones Kapaliswa na Rhodius Nsaro, aliowatapeli zaidi ya shilingi 34 milioni. Angelo aliyekuwa Mchungaji wa Kanisa la FGBF NZEGA, alifukuzwa Uchungaji, tarehe 6.7.2010, kutokana na ukosefu wa maadili, na vilevile Benedict aliyekuwa Mchungaji wa Kanisa la FGBF BABATI, alifukuzwa Uchungaji, tarehe 23.3.2010, kwa ukosefu wa maadili. Baada ya Wachungaji hao kufukuzwa katika Kanisa hilo, walishirikiana na kupanga mkakati wa kumgeuzia kibao Askofu Kakobe, kwa kutunga madai ya uongo dhidi yake, ili kumchafua; na hatimaye kufungua kesi hiyo ya madai tarehe 26.5.2011.
*****************************************************************************************************
Siku zote ukweli unapopambana na uongo, ukweli hushinda!Kama ilivyo ngumu giza kuishinda nuru.Nuru siku zote lazima ilishinde giza.Madai yote ya hao watu yalikuwa ni ya uongo na ya uzushi,hivyo yasingeweza kushinda.
 
Hivi Kuna watu wanakaaa na kujitahidi kudanganya washirika na wengine kwamba kesi hii bado inanguruma ila mwishowe plan zote zitafel tuu
 
1.Mwasisi wa kesi hii alisha kufa na kabla hajafa alijitoa
2.Mtawala aliyetaka kesi hii ametoka madarakani na anaisoma namba
3.Wakiacha kesi hiyo ihukumiwe ni kwamba walioshitaki hawawezi kulipa gharama za kesi!
4.Kutokana na kipengere cha 3 inatakiwa wafungue kesi nyingine ili wapone kulipa gharama
5.Kutokana na Kipengere cha 4.Mwandishi wa habari hii ambaye ni mmoja tu tangia kesi hi ianze atakosa vision hivyo lazina abadili gear angani
6.Matawala aliyepo hataki kesi hizi feki anataka kesi za Mafisadi ili kuleta maana ya hapa kazi
7.Kutokana na kipengere cha 6 sijui kama wanaweza kufungua kesi nyingine ati kufungulia wadhamini
8.Kama watakosea kufungua kesi dhidi ya wadhamini watakuwa wanepoteza lengo la awali la kumushitaki Kakobe!
9.Kumbuka kwamba wadhamini ndo walitakiwa kumshitaki Kakobe kwa wizi na si watu waliofukuzwa kushitaki wadhamini
10.Hata hivyo wakifanikiwa kushitaki wadhamini hilo haliondowi kwamba kesi yao ya awali wameshindwa na sasa wanafungua kesi nyingine ambayo kwao uwezo wa kushinda ni sifuli
11.Watu hawa ambao wanajitapa kuwa watafungua kesi nyingine hata nauli za kwenda mahakamani hawana , na mtawala aliyekuwa anawapa pesa naye anaisoma namba, mtu aliyewapa nguvu alushajitoa kabla hajafa!
12.Ni vigumu sana watu kujua kwamba kesi dhidi ya Kakobe imekufa na Kakobe ameshinda !Hiyo ni aibu kwa wafalme na washauri waliopotosha suala hili hapo mwanzo!
 
Kwanza hawa ni Hatari warudishe kwanza Pesa za wamini waliowaibia.
 
Hivi yule mzee wa konyagi ye hanaga "baraza la wadhamini" pale church kwake.
 
Jamani huyu mtu aitwaye Kakobe yuko hapa nchini???
Yupo mwenge nenda asubuhi hii kanisani kwake pale utamkuta kajaa tele, yeye huwa hana shida na mtu ila ingilia anga zake tu, sasahv katulia tulii rai yangu kwa serikal ya mtumbuaji mkirogwa kumchokoza mtajuta si wa mchezo mchezo yule
 
Mimi sina Imani na vyombo vyetu vya sheria kesi ya 2011 ndiyo wanaifuta juzi muda wote huo ilikuwa figisufigisu tu????
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom