Mahakama Kuu yaamuru madaktari kusitisha mgomo

Inaokana Mwanasheria Mkuu alitumia hati ya dharura kuiomba mahakama kutoa zuio la mgomo!
 
waziri mkuu zamu yako sasa kujiuzulu umezoea kutudanganya watanzania Ulisema serekali imejipannga vizuri na Mgomo, Je mmejipanga kuendelea kuua watanzania wasiyo na hatia au? hueleweki leo siku ya 3.Tupatie ufafanuzi hapo
 
sijui wanakuja au ilikuwa danganya toto.
nasijui Baba Riz1 atalonganini leo

Atawaambia madaktari za mbayuwayu wachanganye na za kwao,alafu atawapiga mkwara,ila madaktari sio sawa na walimu
 
kwani mahakama inashindwa kumwambia waziri madaktari hawana imani naye ili awajibike?
 
Kenya imewafukuza madakatari waliogoma Jk fumba macho fukuza wauaji hawa

Kweli wewe "mama porojo" hebu nenda kajipange upya urudi tena hapa ,nani ana jeuri ya kuwafukuza Madaktari? wamewafukuza wafanyakazi wengine wa sekta ya Afya na sio MADAKTARI.
 
Serikali imeamua kutumia sheria ya kazi no. 6 (FORCED LABOUR)
section 6-(1) Any person procures, demands or imposes forced labour, comits an offence.
(2) For the purposes of this section, forced labour includes bonded labour or any work exacted from a person under the threat of a penalty and to which that person has not consented but does not include
a) Any work exacted under the National Defense Act, 1966 for work of a purely military character;
b) Any work that forms part of the normal civic obligations of a citizen of the United Republic of Tanzania;
c) Any work exacted from any person as a consequence of a conviction in a court of law, provided that the work is carried out under the supervision and control of a public authority and that the person is not hired to, or placed at, the disposal of private persons;
d) Any work exacted in cases of an emergency or a circumstance that would endanger the existence or the well-being of the whole or part of the population;
e) Minor Communal services performed by the members of a community in the direct interest of that community after consultation with them or their direct representatives on the need for the services.

My Take:
Ni aibu kwa Serikali kuogopa na kuona haya kukaa na madaktari kumaliza huu mgogoro kwa amani. huu ubabe wa serikali hautamaliza mgogoro zaidi ya kupalia moto. Kikwete ameshindwa kuongoza nchi.

Lakin hapa mkuu sheria ya forced Labour inaingiaje?
 
Doc halazimishwi kurudu kazini,lakini,as one simple person was saying yesterday, hawa madaktari wanafanya kazi kwa kodi zetu.kwa nini wasiagizwe kuja kututibu. Kumbe hata hawa simple folk can say something clever. Hawa madaktari wamesomeshwa bure na Serikali,kwa nini Serikali isiweze kuwa na nguvu ya kuwathibiti kwa kiasi fulani? Haya matatizo ya Madakatari na Wizara yameanza zamani,siyo leo. Yanakwenda nyuma awamu nyingi,madaktari wanalalamika kuhusu Wizara.
 
Mgomo wa Madaktari haupo kisheria. Serikali inachofanya ni kupinga huu mgomo kwa kutumia sheria ili iweze kutumia njia za kisheria kuwaadhibu wale ambao hawatarudi kazini. Pia kuna uwezekano mkubwa MAT na Chama cha madaktari wakachukuliwa hatua za kisheria kama havijaandikishwa.
Drs wasipoangalia watakosa platform ya kuzungumzia shida zao. Wanaweza pia wakapewa contract mpya.
 
Kama kina Mponda wangekuwa wanajali wananchi kweli wangejiuzulu. Lakini wanajali maslahi yao wala hawana utu.
 
Ofisi ya Waziri Mkuu inafanya propaganda hapa.
Hukumu inatolewa na mahakama,na katika hukumu ilitakiwa ionyeswe kwamba Mwanasheria Mkuu katika shauri lake alikuwa alifikisha kwa nguvu ya sheria gani na vifungu.
Hukumu hii pia inatakiwa ionyeshe wao uamuzi wao umefuata vifungu gani vya sheria,ambavyo madaktari wamevivunja.
Sikatai kuwa kuna hukumu ya Mahakama kuu,lakini si kazi ya Ofisi ya Waziri Mkuu kutangaza hukumu ya mahakama,bali ni kazi ya mahakama yenyewe.Na pia kama Ofisi ya waziri Mkuu inaona umuhimu wa kutangaza hukumu hiyo basi inatakiwa kuiweka hukumu hiyo kama ilivyotolewa na mahakama kuu,na sio kuiweka hivi kichakachuaji,kwani kwa jinsi ilivyotangazwa ipo zaidi kimfumo wa kutishiia.Nadhani kuna akifungu cha sheria ambacho kinakataza uchakachuaji wa namna hii wa maamuzi ya mahakama.
Nawakilisha..........
 
Kwa hiyo mkwara wote wa pinda....kwamba tumejiandaa vya kutosha kumbe amejiandaa kwenda mahakamani.!!
 
Mar 9th 2012, 05:55
Kwa: Wahariri wote;
TV,
RADIO,
MAGAZETI,
BLOGU,


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Mahakama Kuu, Divisheni ya Kazi, leo (*Alhamisi Machi 8, 2012) *imetoa uamuzi wa kusitishwa mara moja kwa mgomo wa Madaktari ulioitishwa nchi nzima tangu jana (*Jumatano Machi 7, 2012).

Katika amri yake ya pili, Mahakama Kuu pia imekitaka Chama cha Madaktari Tanzania na Jumuiya ya Madaktari kuwatangazia wanachama wao mara moja kupitia Vyombo vya Habari kusitishwa kwa mgomo huo nchi nzima kama
walivyowatangazia wakati wanauitisha mgomo wenyewe.

Mahakama Kuu pia imeamuru pande zote mbili, yaani Serikali kwa upande mmoja na Chama cha Madaktari na Jumuiya ya Madaktari, kwa upande mwingine, kutumia fursa zilizopo katika kutatua mgogoro wa kikazi uliopo kati yao kwa
haraka.

Uamuzi huo wa Mahakama Kuu imetolewa na Jaji R.M. Rweyemamu, baada ya kusikiliza ombi la Mwanasheria Mkuu wa Serikali dhidi ya Chama cha Madaktari na Jumuiya ya Madaktari kuitaka itoe zuio kwa mgomo huo.

Akitoa uamuzi huo, Jaji Rweyemamu alisema anazingatia madhara ambayo mgomo huo ungeleta kwa jamii kwa vile huduma za tiba ambazo madaktari walitaka kugoma kuzitoa ni miongoni mwa huduma muhimu zilizotajwa kwenye Sheria ya
Ajira na Mahusiano Kazini, Namba 6 ya Mwaka 2004.

Uamuzi huo, ni kama ifuatavyo:

Leo, tarehe 8, Machi 2012, Mahakama Kuu, Divisheni ya Kazi, mbele ya Jaji R.M. Rweyemamu, baada ya kusikiliza Ombi No. 24 la 2012 lililowasilishwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (Mwombaji) dhidi ya Chama cha Madaktari Tanzania na Jumuiya ya Madaktari (Walalamikiwa), imetoa uamuzi ufuatao:

i) Chama cha Madaktari Tanzania na Jumuiya ya Madaktari pamoja na Wanachama wao, kusitisha Mgomo waliouanzisha rasmi tarehe 7 Machi 2012 nchi nzima na kurejea kazini mara moja kwa kuendelea na kazi zao kama kawaida, mara tu Amri hii itakapowafikia. Aidha, waombaji watatakiwa kutoa Kiapo cha kuthibitisha kwamba wamewasilisha Amri hiyo kwa Walalamikiwa na kuwasilisha Kiapo hicho Mahakama Kuu – Divisheni ya Kazi kesho tarehe 9, Mach 2012.

ii) Mara baada ya Amri hii kuwasilishwa kwa Walalamikiwa (Chama cha Madaktari Tanzania na Jumuiya ya Madaktari) watatakiwa kuwatangazia Wanachama wao kupitia Vyombo vya Habari kusitishwa kwa Mgomo huo Nchi nzima kama walivyowatangazia wakati wa kuitisha Mgomo huo;

iii) Mahakama inaamuru pande zote mbili (Serikali na Chama cha Madaktari Tanzania pamoja na Jumuiya ya Madaktari) kutumia fursa za Kisheria zilizopo katika kutatua Mgogoro wa Kikazi uliopo kati yao kwa haraka.
(mwisho)

Imetolewa na:

Ofisi ya Waziri Mkuu,
S.L.P. 3021
DAR ES SALAAM.
Alhamisi Machi 8, 2012

Ofisi ya Waziri Mkuu inafanya propaganda hapa.
Hukumu inatolewa na mahakama,na katika hukumu ilitakiwa ionyeswe kwamba Mwanasheria Mkuu katika shauri lake alikuwa alifikisha kwa nguvu ya sheria gani na vifungu.
Hukumu hii pia inatakiwa ionyeshe wao uamuzi wao umefuata vifungu gani vya sheria,ambavyo madaktari wamevivunja.
Sikatai kuwa kuna hukumu ya Mahakama kuu,lakini si kazi ya Ofisi ya Waziri Mkuu kutangaza hukumu ya mahakama,bali ni kazi ya mahakama yenyewe.Na pia kama Ofisi ya waziri Mkuu inaona umuhimu wa kutangaza hukumu hiyo basi inatakiwa kuiweka hukumu hiyo kama ilivyotolewa na mahakama kuu,na sio kuiweka hivi kichakachuaji,kwani kwa jinsi ilivyotangazwa ipo zaidi kimfumo wa kutishiia.Nadhani kuna akifungu cha sheria ambacho kinakataza uchakachuaji wa namna hii wa maamuzi ya mahakama.
Nawakilisha..........
 
MaDaktari wasome na fani nyingine kama sheria, menejimenti na utawala ili nje ya chumba cha kutibu watumie weledi huu wa ziada kufanya maamuzi yanayoendana na hadhi, heshima inayoendana na TAALUMA yao. Niulize kidogo: MAT inaweza kushtaki au kushtakiwa?
 
Madaktari walisha resolve kugoma hata angeondoka Pinda madarakani, kwahiyo hamna jinsi ni vizuri waendelee na mgomo kwakuwa hamna tatizo ambalo halina utatuzi.
 
Cha kushangaza zaidi huyo Hakimu aliyetoa hiyo Hukumu wiki ijayo nae anagoma kudai maboresho ya maslahi ya kazi yake. Nadhani wote tumeskia juu ya Mgomo wa Mahakimu jamani!

Inawezekana hakimu kalazimishwa na boss wake kutoa hukumu ya namna hiyo ilihali na wao mahakimu wanampango wa kugoma!!! Kichekesho kingine.

Tunangoja kusikia cha saa kumi jioni ya leo!!1
 
Madaktari walisha resolve kugoma hata angeondoka Pinda madarakani, kwahiyo hamna jinsi ni vizuri waendelee na mgomo kwakuwa hamna tatizo ambalo halina utatuzi.
Wakipuuza amri hii halali ya mahakama itakula kwao sana tu. Nawahurumia zaidi ma-Interns ambao hata ajira rasmi hawana.
 
Kuna swala moja ambalo inabidi tulielewe,ambalo linahusu umuhimu wa kuijua sheria.Serikali inaonekana wameona kuna pengo kisheria katika swala zima la mgomo kama ulivyoitishwa na madocs,na wanataka kutumia loop-hole hiyo ili wawe covered kisheria watakapokuja kutoa maamuzi yao hapo baadae.
Inabidi sasa tuangalie,madoc wameitisha mgomo kupitia kwa vyama gani,maana juzi niliona kiongozi mmoja wa chama kimoja cha madaktari akisema mgomo huo umeitishwa na wao madokta kama madokta,na wala sio kupitia chama chao kinachowawakilisha.Sasa hapa ndipo madaktari watakapokuja kushindwa kama kweli hawakuitisha kupitia vyombo vyao vya uwakilishi vinavyotambuliwa kisheria.
MIGOMO INALINDWA NA SHERIA NA NI HAKI YA WAFANYAKAZI na kuna vigezo vinavyotolewa katika sheria ambavyo ndivyo inabidi vifuatwe ili mgomo uwe wa halali,la sivyo mgomo huo utakuwa haramu.Na hapa ndipo inaonekana serikali wamepata upenyo,na ndipo wanapotaka kuwabania madaktari,na madaktari wasipooangalia,kama hawakuwashirikiisha wanasheria kuwaweka sawa kisheria kabla hawajaitisha mgomo,basi itakuwa imekuula kwao.hukumu hii ya mahakama inaipa serikali jukwaa la kusimamia na kutoa maamuzi yake,kwa kadri watakavyoona inafaa,na watakuwa wapo-covered kisheria,provided kwamba itathibitika kuwa mgomo huu haukuwa halali.INABIDI PIA TUONE NAKALA YA HUKUMU YA MAHAKAMA (NA SIO TAMKO LILILOTOLEWA NA OFISI YA WAZIRI MKUU) ILI TUJUE HASA KITU CHA KUJADILI KWA UFASAHA ZAIDI.
Na hii lazima itupe alarm,inaonyesha kwamba serikali inajiandaa kutoa maamuzi magumu kufuatana na sakata zima la mgomo wa madaktari,ngoja tuone muheshiimiwa Presidaa ataongea nini,kama hatatuyeyusha tena kama kawaida yake.
 
Back
Top Bottom