Mahakama Kuu yaamuru madaktari kusitisha mgomo

Nadhani sasa wanataka kutumia mbinu za "mahakama imeamuru hawajatii sheria".. what is wrong with this people? Wanazo jela za kutosha? Hivi kweli 2 wawili kuondolewa kunasababisha kutumia nguvu hii yote? Kwanini basi wasitume Jeshi la Wananchi na POlisi kwenda kwenye nyumba za madaktari na kuwalazimisha kurudi kazini?

Wanaogopa kushangwazwa na jinsi watakavyokuta madaktari wanakaa vichochoroni, maana wataumbuka!
 
Nimesikia taarifa ya habari tbc taifa (radio ya magamba) ya saa 0:00 kwamba ma-doctor wameamrishwa na mahakama kusitishe mgomo wa kuwashinikiza waziri na naibu waziri wa afya wajiuzuri.
Nawasilisha!
Hii maana yake nini?


Huyu aliyeleta hii topic ametumwa atest zali kama wakiingia na hiyo singo ya mahakama, madaktari watakuwa wamejipangaje?

Madaktari na nyie kama hamjajipanga na hili, hakikisheni mnakuwa hatua mbele yao. Watafuteni watu kama kina Tundu Lisu wasiohongeka ili wawashauri.
 
Mahakama ina mamlaka gani kutoa amri kama hiyo?

Nadhani wamewahi kufanya hivyo kabla kwenye sakata la mgomo wa walimu, kama kumbukumbu zangu ziko sahihi walitoa zuio la mahakama (court injunction) jioni ya kuelekea mwisho wa juma ili lisikatiwe rufaa na wagomaji watarajiwa
 
NANUKUU...
mahakama kuu kitengo cha kazi imewaamuru Madaktari kurudi kazini mara moja na kutoa ufafanuzi kuwa majadiliano ya haraka yanatakiwa kufanyika kati ya upande wa serikali na upande wa madaktari ili kuweza kumaliza tofauti zilizopo...
MWISHO WA KUNUKUU...
 
Mahakama ina mamlaka gani kutoa amri kama hiyo?

mamlaka wanayo; tatizo ni kuwa wanayo kwenye issue hii? wanamuamuru nani hasa? Chama cha Madaktari au madaktari mmoja mmoja au chama cha wafanyakazi madaktari? Ikumbukwe walipotoa amri kama hii miaka michache iliyopita ilikuwa ni kwa chama cha wafanyakazi kuzuia kuanza kwa mgomo; lakini huu ni mgomo ambao tayari umeanza na haujaitishwa na chama cha wafanyakazi cha madaktari bali chama cha madaktari (professional association)..
 
NANUKUU...
mahakama kuu kitengo cha kazi imewaamuru Madaktari kurudi kazini mara moja na kutoa ufafanuzi kuwa majadiliano ya haraka yanatakiwa kufanyika kati ya upande wa serikali na upande wa madaktari ili kuweza kumaliza tofauti zilizopo...
MWISHO WA KUNUKUU...

Tamko linasemaje wasipo rudi? Tamko linasema nani amepeleka kesi mahakamani? Sheria zinasemaje kama madaktari watakataa amri ya mahakama? Je kwani mfanyakazi akiamua kugoma au kuacha kazi anashtakiwa kama mwajiri ameshindwa kutimizi masharti ya makubaliano ya kazi wakati wa kuajiriwa? Je hizi mahakama ziko kwa ajili ya haki au ya serikali???
 
This is one of the most aoutregeous statements I have ever heard. Mahakama kuu inangilia vipi mgomo wa madaktari? Mtoa mada, rudi shule ujifunze kuandika . Kumbukeni hawa wanagoma kudai madiliko ya kiutendaji. Ni kweli hii serikali ya kikwete kila kitu kinawezekana. Jembe apone arudi nyumbani kuiongoza nchi

Uliandika vizuri sana lakini sentensi yako ya mwisho imechafua maana nzima, nimekudharau sana! hivi nchi hii yenye wakaazi zaidi ya milion 44 haina watu wengine wanoweza uongozi zaidi ya kutegemea mafisadi walishindwa kuongoza wakalazimishwa kujiuzulu, mbona kuna vijana wengi tu wenye uwezo na upeo na makini wasio na chembe za ufisadi na wizi?? Think twice before you put your rubbish here!!
 
Waziri mponda mbishi, anasema mbona waziri wa ulinzi na JKT ameshakutwa na mabalaa mara nying tu, yakiwemo ya gongolamboto na mbagala, pia waziri wa mambo ya ndani, polis wake wanaua raia kila kukicha, yeye kutofautiana na madaktar imekuwa nongwa!
Kuna harufu ya POINT japo haina mantiki sana.
 
Polisi, risasi na maji ya kuwasha vimeshindikana this time? Prezidaa jasho litamtoka, anangojea akadanganye wazee wa ccm leo! Wonders will never cease!
 
ni kweli mtoa mada yuko sahihi.Serikali imepeleka maombi ya upande mmoja(exparte) ya kuiomba mahakama kuu kitengo cha kazi kubatilisha mgomo wa madaktari.Maombi haya yamefanyika chini ya hati ya Dharura(certificate of urgency)matokeo ya amri hii ni kwamba,serikali inatafuta uhalali wa kuwafukuza wale watakaoshindwa kutii amri ya mahakama.Hali sijui itakuwaje!!
 
Mahakama zetu kama za kichina vile! Kesi imeendeshwa gizani, hukumu wameitangaza!

Achana na mahakama za china kwani zipo makini kwenye hukumu zinazo husu taifa lao. Mahakama ya tz ni mahakama ya kipuuzi au kijinga au ya kitahila ulitakiwa kusema hivyo
 
ni kweli mtoa mada yuko sahihi.Serikali imepeleka maombi ya upande mmoja(exparte) ya kuiomba mahakama kuu kitengo cha kazi kubatilisha mgomo wa madaktari.Maombi haya yamefanyika chini ya hati ya Dharura(certificate of urgency)matokeo ya amri hii ni kwamba,serikali inatafuta uhalali wa kuwafukuza wale watakaoshindwa kutii amri ya mahakama.Hali sijui itakuwaje!!
na kama watagoma wote na wakatae kurudi, watawafukuza kazi wote?
 
wazee wanu na watanzana kwa ujumla kuna huyu sijui wana mwita dr ulimboka hata udr wenyewe sijui kaupata wapi eeh si doc huyu ni kanjanja tu kaja hapa anawapotosha madr ooh tugome huyu ana sababu zake za KISIASA sintoweza kuliongelea hili sana kwanh lipo mahakamani.WADAU NAJARIBU KUWAZA JK ATAKAVYO ONGEA NA TAIFA KUPITIA WACHUMIA TUMBO WA MAGAMBA KWA JINA LA WAZEE WA DAR
 
kinachonitisha hasa ni kuwa suala hli ambalo kwa kweli ni la kisiasa lingeweza kumalizwa nje ya mahakama. Kuiingiza mahakama kwenye hili ni kutaka kuleta matatizo kwa mahakama vile vile. Hivi, madaktari wakiamua kudharau amri hiyo ya mahakama kwa sababu wanaamini siyo halali nini kitafanyika? Well, inaweza kuwasaidia serikali kufanya mambo fulani fulani "kwa sababu madaktari wamekataa amri halali ya mahakama" lakini haiwezi kufanya serikali ionekane kuwa inahoja. Kwa kukimbiliaa mahakamani imeonesha tu kuwa serikali imeshindwa hoja ya kushawishi.

Ndio uzuri mmoja wa migomo kama hii kwani hapa POlisi au FFU hawawezi kutumika. Hawawezi kwenda kwenye nyumba za madaktari na kuwaburua kwenda hospitali! Hawawezi kutumia vikosi vya jeshi kuwalazimisha madaktari kuandika tiba na kufanya uchunguzi. Njia pekee ni kuwashawishi. Sasa hata tukiassume kuwa madaktari - technically - wanarudi kazini kutii amri ya mahakama je mahakama inaweza kuwalazimisha kufanya kazi? Itakuwaje kama madaktari wote as strategic move wanaamua kurudi kazini lakini hawafanyi kazi mahakama itawaagiza nini "watibu"?
 
Waziri mponda mbishi, anasema mbona waziri wa ulinzi na JKT ameshakutwa na mabalaa mara nying tu, yakiwemo ya gongolamboto na mbagala, pia waziri wa mambo ya ndani, polis wake wanaua raia kila kukicha, yeye kutofautiana na madaktar imekuwa nongwa!

hapa bila shaka ni kauli yake ya kikuda aliyotoa dhidi ya madokta. Yeye watu wake ni wanajimbo na wakulima. Utadhani vile vyandarua alivyokuwa akiandikia kila mada vinafunika mazao
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom