Mahakama Kuu yaamuru madaktari kusitisha mgomo

BORNCV

JF-Expert Member
Oct 11, 2011
242
46
Nimesikia taarifa ya habari tbc taifa (radio ya magamba) ya saa 0:00 kwamba ma-doctor wameamrishwa na mahakama kusitishe mgomo wa kuwashinikiza waziri na naibu waziri wa afya wajiuzuru.

Hii maana yake nini?

Barua toka Ofisi ya Waziri Mkuu kwenda kwa vyombo vya habari:

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Mahakama Kuu, Divisheni ya Kazi, leo (Alhamisi Machi 8, 2012) imetoa uamuzi wa kusitishwa mara moja kwa mgomo wa Madaktari ulioitishwa nchi nzima tangu jana (Jumatano Machi 7, 2012).

Katika amri yake ya pili, Mahakama Kuu pia imekitaka Chama cha Madaktari Tanzania na Jumuiya ya Madaktari kuwatangazia wanachama wao mara moja kupitia Vyombo vya Habari kusitishwa kwa mgomo huo nchi nzima kama walivyowatangazia wakati wanauitisha mgomo wenyewe.

Mahakama Kuu pia imeamuru pande zote mbili, yaani Serikali kwa upande mmoja na Chama cha Madaktari na Jumuiya ya Madaktari, kwa upande mwingine, kutumia fursa zilizopo katika kutatua mgogoro wa kikazi uliopo kati yao kwa haraka.

Uamuzi huo wa Mahakama Kuu imetolewa na Jaji R.M. Rweyemamu, baada ya kusikiliza ombi la Mwanasheria Mkuu wa Serikali dhidi ya Chama cha Madaktari na Jumuiya ya Madaktari kuitaka itoe zuio kwa mgomo huo.

Akitoa uamuzi huo, Jaji Rweyemamu alisema anazingatia madhara ambayo mgomo huo ungeleta kwa jamii kwa vile huduma za tiba ambazo madaktari walitaka kugoma kuzitoa ni miongoni mwa huduma muhimu zilizotajwa kwenye Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini, Namba 6 ya Mwaka 2004.

Uamuzi huo, ni kama ifuatavyo:

Leo, tarehe 8, Machi 2012, Mahakama Kuu, Divisheni ya Kazi, mbele ya Jaji R.M. Rweyemamu, baada ya kusikiliza Ombi No. 24 la 2012 lililowasilishwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (Mwombaji) dhidi ya Chama cha Madaktari Tanzania na Jumuiya ya Madaktari (Walalamikiwa), imetoa uamuzi ufuatao:

i) Chama cha Madaktari Tanzania na Jumuiya ya Madaktari pamoja na Wanachama wao, kusitisha Mgomo waliouanzisha rasmi tarehe 7 Machi 2012 nchi nzima na kurejea kazini mara moja kwa kuendelea na kazi zao kama kawaida, mara tu Amri hii itakapowafikia. Aidha, waombaji watatakiwa kutoa Kiapo cha kuthibitisha kwamba wamewasilisha Amri hiyo kwa Walalamikiwa na kuwasilisha Kiapo hicho Mahakama Kuu – Divisheni ya Kazi kesho tarehe 9, Mach 2012.

ii) Mara baada ya Amri hii kuwasilishwa kwa Walalamikiwa (Chama cha Madaktari Tanzania na Jumuiya ya Madaktari) watatakiwa kuwatangazia Wanachama wao kupitia Vyombo vya Habari kusitishwa kwa Mgomo huo Nchi nzima kama walivyowatangazia wakati wa kuitisha Mgomo huo;

iii) Mahakama inaamuru pande zote mbili (Serikali na Chama cha Madaktari Tanzania pamoja na Jumuiya ya Madaktari) kutumia fursa za Kisheria zilizopo katika kutatua Mgogoro wa Kikazi uliopo kati yao kwa haraka.

Imetolewa na:

Ofisi ya Waziri Mkuu,
S.L.P. 3021
DAR ES SALAAM.
Alhamisi Machi 8, 2012
 
This is one of the most aoutregeous statements I have ever heard. Mahakama kuu inaingilia vipi mgomo wa madaktari? Mtoa mada, rudi shule ujifunze kuandika . Kumbukeni hawa wanagoma kudai madiliko ya kiutendaji.

Ni kweli hii serikali ya kikwete kila kitu kinawezekana. Jembe apone arudi nyumbani kuiongoza nchi
 
He!Kweli hili?Ebu toa ufafanuzi!Yaani kuanzia kesho kunamadoc watalala segerea!
 
Nani alifungua kesi na kesi iliendeshwa wapi, karibu vitisho vyote mtamaliza imebaki kusikia jeshi limesema, kinachotakiwa ni very simple waziri na naibu wake watoke pale ili mazungumzo yaendelee na si vitisho.
 
Mahakama zetu kama za kichina vile! Kesi imeendeshwa gizani, hukumu wameitangaza!
 
Nadhani sasa wanataka kutumia mbinu za "mahakama imeamuru hawajatii sheria".. what is wrong with this people? Wanazo jela za kutosha? Hivi kweli 2 wawili kuondolewa kunasababisha kutumia nguvu hii yote? Kwanini basi wasitume Jeshi la Wananchi na POlisi kwenda kwenye nyumba za madaktari na kuwalazimisha kurudi kazini?
 
Waziri mponda mbishi, anasema mbona waziri wa ulinzi na JKT ameshakutwa na mabalaa mara nying tu, yakiwemo ya gongolamboto na mbagala, pia waziri wa mambo ya ndani, polis wake wanaua raia kila kukicha, yeye kutofautiana na madaktar imekuwa nongwa!
 
Cha kushangaza zaidi huyo Hakimu aliyetoa hiyo Hukumu wiki ijayo nae anagoma kudai maboresho ya maslahi ya kazi yake. Nadhani wote tumeskia juu ya Mgomo wa Mahakimu jamani!
 
Kwani mahakama ndio mwajiri wa madokta.
ndio maana limeletwa hapa ili lijadiliwe mkuu !
Watakuja wataalam wa mambo na watafafanua zaidi lakini mtizamo wangu lazima kuna k2 jk amefikili ndio maana ameamua kutumia mahakama hebu ngoja 2subili iyo hotuba yake.
Maana jambo lenyewe limeanzwa kutangazwa usiku huu !
Sasa sijui iyo mahakama imeamua saa ngapi !
 
Hii hali ilipofikia sasa ni wanataka kuanza kutuchekesha tu....
Haya hii mahakama imetokea wapi??
Anhaa wanaandaa cushion za JK kuangukia kesho mbele ya vile vizee!
 
Achana nawanamtandao!Eti oooh wanamtandao wameachana namambo yamtandao!!Kesho madoc wanafukuzwa kazi,wakikaidi keko nasegerea inawangoja!Nchi yakusadikikaa....bwana!Doc unamlazimisha kurudi kzn?Akianza kutoa poor treatements kwawagonjwa?Kisa waziri na naibu wake!
 
...This can't be true. In maana kila njia imeshindikana kutatua tatizo hili?

...Kila mmoja kuja na kauli yake juu ya huu mgomo ni KIAMA. Are we really in deep shit or is it just being hyped?


problem solved..

mengine wanatafuta tu pakutokea sasa..

a lot of speculation and spinning (especially) media attention
 
Back
Top Bottom