Mahakama Kuu ya Tanzania yaamuru DOWANS kulipwa!

Oooooooooh operation kata umeme,mgao wa umeme na kukusanya madeni kuwalipa Dowans
Cccm oyeeeeee!
 
Hii ni silaha nyingine ambayo Chadema wanatakiwa kuitumia kuitungua CCM kwenye uchaguzi Igunga.

Watanzania sasa twahitaji kuamka kwa vitendo, halipwi mtu iwapo wananchi tukiamua hivyo.
 
I hereby declare ROSTAM AZIZ as the MOST POWERFUL MAN in Tanzania. He can do ANYTHING he wants with The U.R.T. He got the POWER. He owns this country.
 
I hereby declare ROSTAM AZIZ as the MOST POWERFUL MAN in Tanzania. He can do ANYTHING he wants with The U.R.T. He got the POWER. He owns this country.

Sbb ya ujinga Wa Watanzania waliowengi anaweza pia kununua mkoa wowote hapa Tz
 
Kumuachia Mjinga afanye atakavyo nao ni Ujinga pia...

Zamani sie tukifanya ujinga tulikuwa tunachapwa haswa na haturudii tena ujinga.

Chumeni fimba watajirekebisha hawa Sijui niwaite Mafedhuri? Kunaumuhimu kuchunguza uraia na asili za watu wanaotaka kuongoza nchi hii ishakuwa too much
 
nashindwa hata nichangie nini hapa,natamani kuuwa isingekuwa kosa kisheria au dhambi. hawa jamaa wa dowans tungenyonga kabisa
 
ni nani alitegemea dowans itashindwa? Mlalamikaji ndo huyohuyo mshitakiwa! Sasa wewe unadhan kesi ingeishaje? Ni wakati wa kuingia barabarani sasa!
 
Kama kuna mtu anafuatilia timeline ya matukio hapa Tz atagundua mpangilio wa matukio ambayo kwa namna hali ilivyo yatakuwa designed na Grand Architect- "The Mastermind himself"

Kwa sasa macho na masikio ya watanzania wengi yapo igunga, halafu hukumu ndio inatolewa! Tena ya malipo! WHY NOW?

Hakika wajinga ndio waliwao. But kwa kuwa sasa ujinga umetutoka hatuwezi kukubaliana na hii dhuluma iliyosababishwa na siasa chafu, na za makundi ndani ya CCM.

Hongera CDM kama mtakuwa mmeliona hili na kuwasha moto huko huko kwenye uwanja wa mapambano. Bahati nzuri ni kwamba, dhuluma hizi na hila za namna hii zinaweza kugeuzwa kuwa opportunity zenu kisiasa na kuwaongezea karata zenu za mwisho. They didn't see you coming
 
Jaji Mhe. Emilian Mushi, hukumu yako hii imewakandamiza Watanzania wote Maskini wa Nchi hii, kwani pamoja na sheria zenu kujifanya mnafata sana sheria, kwa hili umechemka.

Wewe unajua kuwa toka utoaji wa zabuni kwa kampuni hii feki, uligumikwa na ukiukaji wa Haki za Binadamu kwa kutumia kodi ya walalahoi wa Tanzania kwa ajili ya kujinufaisha watu wachache, Au hilo hulijua? Sasa wewe unasema sheria za Kimataifa, sisi zinatuhusu nini kwa maisha yetu? Iandike siku hii ya leo, nina uhakika utakujua kuijutia. Take My Word.

Mkuu mahakama haifanyi kazi kwa hisia. Mahakama inafanya kazi kwa ushahidi uliowasilishwa mezani. Wanasheria wote mahiri including AG walijua kuwa hii kesi iko wazi kabisa na TANESCO walivunja mkataba.

Wale waliosema mkataba uvunjwe bila kuzingatia sheria ndio wametufikisha hapa na wala siyo huyu Jaji. Jaji amehakikisha tu kwamba haki inatendeka na haki ikitendeka lazima mjoja aumie ndio haki yenyewe hiyo!!
 
Siasa uchwara ktka mambo ya kitaalam ndi zimetumaliza na zitaendelea kutumaliza eti kwamba wabunge wana akili kuliko proffessionals! Haiwezekami hata kidogo!
 
Hakika Andrew Chenge atakuwa amefurahi sana Dowans kulipwa. Hivi alitoa msaada ya kisheria kama alivyoahidi kuisaidia ili ilipwe baada ya kushinikizwa kujivua gamba?
 
Ni dawa chungu kumeza, lakini Dowans ilishashinda kwenye int courts, parties walikubaliana mashauri yoyote ya kimkataba yaasisiwe na kusimamiwa na tribunal za nje....

Kwaajili ya pressure za hapa na pale ndio maana tukaipinga hii hukumu locally, cha msingi kuangalia na kuupitia upya mikataba ambayo iko current, ambayo tunaweza kuirekebisha...

Yaliyopita si ndwele...

Nsiande usitake kuwaaminisha watanzania kiraisi namna hiyo!

Hapa pana hoja ya kujibu serikali, yaani wewe unaona ni jambo rahisi lakini elewa serikali yetu hiana fedha ya kulipa na hivyo itakimbilia kukopa nje ya nchi na kuongeza deni la nje jambo ambalo mwanao na vizazi vyake ndiyo watakuja kutaabika! Kiukweli kwa hili serikali imechemka.
 
quote_icon.png
By Izack mwanahapa

Mahakama kuu ya Tanzania kupitia Jaji Emilian Mushi imeiamuru Tanesco kuilipa mabilioni ya fedha kampuni ya dowans kwa kigezo kuwa mahakama ya Tanzania haiwezi kupingana na Mahakama ya kimataifa, lakini pia mahakama imeiamuru Tanesco kulipa gharama zote za kesi hiyo ambazo bado hazijafanyiwa tathmini.

Majaji wa Tanzania ni sehemu ndogo ya mtandao wa maadui wa Muumba...................hi dhuluma wanayotufanyia kamwe Mwenyezi Mungu kwenye utukufu wake hatakubali kukaa kimya...........................wote hawa wadhalimu kiama chao kipo karibu....................haingii akilini kuwa mahakama yetu pamoja na kulindwa na sheria ijione sasa imekuwa ni butu kutanzua dhuluma.............................kwa lugha nyingine mahakama zetu zinatawaliwa na mahakama za kikoloni kule uingereza......................hivi uhuru tuliutafutia nini kama lengo ni kuwarudishia tawala walewale wakoloni........................shame on on us including me..............................
 
Back
Top Bottom