Mimi nauelewa wangu mdogo wa sheria sijawahi ona na sitaraji kuona hukumu yoyote dunia ambayo haiwezi kupitiwa upya au kupitiwa upya, hata iran na sheria zao za kiislamu lakini bado tunaona kuna hukumu za kifo/ kupigwa mawe zinapitia na kutolewa uamuzi upya.Hapo bado sijakuelewa. Mahakama Kuu itawezaje ku annul kitu ambacho yenyewe haikuwa privy? Ninachoweza kuelewa ni kama watakataa kuiandikisha na kuitarifu International Court of Arbitration kuhusu sababu zao, ambao kama watakubaliana nao, ndio watakaoweza ku-set aside award. Na mahakama yetu itatoaje uamuzi kuhusu kuweko kwa rushwa wakati haina mandate ya kuchunguza? Watasemaje kuwa pana rushwa hapa bila prosecutors kuwapelekea ushahidi wa kitendo hicho kuwepo? Hapa si Spain au Italy ambako Mahakama wana madate ya kuchunguza. Halafu hilo la public interest/policy litakuwa gumu mno kulitetea maana wengi wametumia kama fig leaf ya kuwadhulumu wengine.
Wanasheria wa Tanesco walikuwa na uwezo wa kukataa hiyo provision maana si lazima iwepo. Lakini ukweli ni kuwa hakuna mtu ambaye anaingia katika mkataba wa kimataifa atakayekubali kuwa dispute ziwe resolved kwa litigation au arbitration laws za upande mmoja. Tanesco wangekataa , wangeonyesha bad faith.
Mimi naamini gharama kubwa zaidi ya kutoheshimu uamuzi huu si kukamatwa kwa asset zetu bali ni kupoteza credibility duniani. Kwa kufanya hivyo, gharama za kufanya biashara na wenzetu zitapanda sana. Au mbaya zaidi, wafanyabiashara wwale wanaojiheshimu watatukwepa na kutubakiza na matapeli.
Tulipe na tujifunze kutokana na hili. Mikataba si lele mama.
Amandla......
sasa tukija katika suala la dowans na icc, bado naamini kuna njia za kuweza kulirejea jambo hilo kwa mfano kama alivyo sema fareed kwamba ppa haikutumika ipasavyo, kulikuwa na issue of fraud or even rushwa katika kuingia kwa mkataba huo, sasa sema kwa kuwa gt ndio watoaji rushwa wenyewe hawawezi kutumia kifungu hiki kujishtaki.
na kuhusu mambo ya abitration ni njia mbadala ambayo inakuwa encourage kufwatwa katika commercial issues, lakini upande moja ukishindwa kuridhia then case inaweza kwenda kwenye full hearing iwe costa rica au tanzania.
sasa mtu unapo sema wanaweza kuattach mali yetu , watakuwa wametumia amri ya mahakama ipi? mahali ambapo mali ya tanzania inaweza kuattach labda amri itoke kwenye mahakama huko costa rica/tanzania ambapo hawa jamaa wakiweza kusajili huu uamuzi na mahakama hiyo itoe uamuzi huo ku-enforce icc ruling.
mahali ambapo mali ya tanzania iliwahi kushikwa ni pale mwl alipo taifisha mali ya muholanzi moja steyn aliyekuwa na mashamba huko arusha na kuchukuliwa na nafco, nakumbuka kwa mbali walizuia meli ya mafuta iliyo kuwa inakuja bongo.
kuhusu suala la reputation hatuta poteza reputation yoyote kwa kushindwa kutekeleza amri ya kuilipa kampuni ya kitapeli-costa rica? ingekuwa bae system , airbus, boeng, gm etc ningekuelewa lakini kampuni ya costa rica iliyo tumia rushwa au fraud kupata contract. basi mambo ya fair trade , or equal playing field lingekuwa halizungumziwi.
rejea weakleaks ya airbus vs boeing na rejea hukumu dhidi ya bae system usa na uk.
halafu pia rejea case kama ya micro soft walivyo pigwa faini kwenye mahakama za eu, halafu uende kwenye case ya toyota wanavyo nyanyaswa huko usa.
ni sisi kusi mama kama nchi na kunyongana na mtu kwa sheria zetu.